Msaada: Nyumba kuwa na matumizi makubwa ya umeme!!!

Kwa mwezi naweka umeme wa elfu 70. Nyumba yangu inakula umeme kama sheikh anacyokula wali kwa mikono. Janga kubwa sana hil...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] daah imebidi nicheke mkuu
 
Mimi nipo kwenye nyumba ya kupanga yenye wapangaji 8 kati ya hao wapangaji saba wapo single na mmoja ndo mwenye mke na anamtoto mdogo muda wa mchana anabaki mkewe na mtoto sisi wengine tunaenda kusaka pesa na huwa tunatoka asubuhi sana kurudi usiku ratiba huwa hazitofautiani sana

Lakini cha kushangaza unit 40 zinaisha ndani ya siku 5 au 6 na kwa mwezi tunatumia unit 200 sijui tatizo ni nini kodi yangu ikiisha nataraji kuhama kwa hii nyumba bili ya umeme inanimalizia pesa
 
Mabachela wanapenda sana rice cooker, itakua wenzo jioni wanapikia rice cooker
 
 
Kaka hapo hua kuna issue kubwa mbili, kwanza ni ile earth rod hua inachoka au hakuiweka vzr, hii ilinilia sana unit kabla haijabadilishwa
Pili ni size ya waya za wiring, ita fundi aangalie vitu hivyo viwili na vingine atakavyoshauri yeye
Shukran!!
Huu ushauri mzuri Sana Anza nao
 
Kitu cha umeme kilichochoka. TV hasa zile za plasma na mafriji ya kizamani.
Au mtu ananunu freezer mtumba..
Freezer jipya Tu linakula zaidi ya unit moja daily......vifaa vibovu na wiring mbovu inakula Sana umeme
 
TV mtumba ,freezer ..vinakula Sana umeme ..na wiring mbovu...
Earth rod na earth wire zikifungwa vibaya...
Au earth rod sio copper original
Mimi tv ndio ya mtumba nifanyeje ase maana now nawashanjioni tu LG
 
Anza na earth rod..tafuta copper original... ukienda dukani wakikwambia original ipo tafuta sumaku iguse...ikinasa ujue hiyo sio original...funga earth rod original...uone
 
mfumo wa earth
je waya toka bodi mpaka kule ardhini alitumia waya wa 4 mm²?
je earth rod ni copper yenyewe ( sio mchanganyiko ) au chuma ?
je earth rod ina unene gani ?
je earth rod imezama yote ardhini ?
je aliweka chumvi na mkaa huko ardhini ?
je sakiti breka ( ile kubwa ) inayopokea umeme, ina kitufe pale mbele, ukikibonyeza, umeme unakata nyumba nzima ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…