Hii shida ya punyeto kwa vijana wa sasa ni kubwa sana. Na kuna usiri mkubwa sana katika kuijadili ila ukweli watumiaji ni wengi sana wa huu uraibu na ni kwa rate kubwa sana.
Kimsingi, uwepo wa uraibu(addiction) wa punyeto ( masterbation) katika jamii yetu ya vijana wa sasa ni matokeo ya moja kwa moja ya kukosekana misingi ya kuwaandaa vijana na mabinti kwaajiri ya ndoa.
Maisha ya ndoa huuweka mwili katika hali ya kupambana na vishawishi vya kingono na kuukeep busy na shughuli za kifamilia, kijamii, na pia kutafakari kuhusu uzalishaji wa mali na uwekezaji kwaajiri ya familia na jamii yako.
Sasa haya maisha ya sasa kuna msukumo mkubwa sana wa kuidhoofu taasisi Ndoa na kuifanya ionekane kama kero kwa wahusika yet.... wahusika .... hawa hawa wahusika wanataka kupata benefits zinazopatikana kwenye ndoa kama upendo, kujaliwa, kusikilizwa, mahitaji ya kimwili na akili kama kukumbatiwa, kubembelezwa, kununuliwa Mavazi, kupewa pocket money, etc.
Ni muda sasa viongozi, jamii na taasisi wakatambua madhara makubwa ya kijamii, kisiasa na kiuchumi katika eneo la mahusiano maana miaka hii ya tisini kuja elfu mbili hata watu wenye mfadhaiko na changamoto za kisaikolojia wanaongezeka kwa kasi sana ukilinganisha na miaka ya nyuma huku mitaani.
Unakutana na mtu ila hayupo sawa sawa. Anawasiwasi, ana hasira za hovyo kwenye mambo madogo ya kupuuza tu, ana majibu yasiyo ya heshima, anafanya umalaya kama kitulizo cha akili au kujikimu etc. Haya yote ni matokeo ya msingi mbovu wa eneo la ndoa. Ndoa ndio taasisi nambari moja ya taifa au jamii yoyote Duniani. Ukiidhoofisha jiandae kutengeneza misukule kwenye Jamii na taifa kwa ujumla.
Watoto watakaozaliwa nje ya ndoa au ndani ya ndoa za mifarakano wengi watakuwa na issues mbali mbali za kisaikolojia ikiwemo Traumatized minds ambazo zitawafanya washindwe kuwa sehemu ya raia wazuri wataanza kuishi kwa mifumo yao wanaoijua.
Mfano unakutana na binti anasema mimi sitaki kuolewa ila nataka nipate watoto wangu tu nilee mwenyewe jua tatizo hilo hapo mbele ya macho yako.
Ukiona binti analala na mume wa mtu bila kujali madhara ya kuvunja ndoa za watu shida hiyo hapo mbele yako.
Ukiona kijana anazaa hovyo watoto halafu hataki kuanzisha familia na wanawake ana zaa nao jua shida hiyo hapo.
Ukiona kijana anatesa wanawake zake kwa vipigo, hasira hasira, anabaka au kulawiti watoto wadogo shida hiyo hapo mbele yako.
Ukiona rushwa imejaa kila eneo then jua uozo umeanza ndani ya familia kuwa na misingi ya tamaa katika malezi ya watoto.
So nikirudi kwenye mada na kujikita hapa kwenye eneo la punyeto, ni vema tukafahamu hii ni vita ya akili na roho. Punyeto ni ishara ya kukosekana kwa uwepo wa spirit ya kike katika maisha ya mwanaume.
Unaweza kuoa na ukawa na mke mzuri tu ila ukashindwa kufurahia nae mgegedo sababu ndani ya nafsi, akili na roho yako kuna gepu kubwa sana la kukosekana mwanamke ndani ya maisha yako.
Vijana wengi wanakaa boarding school hadi wanamaliza chuo hii. Muda wote huu wakosa kujenga bondi na kuwalewa wanawake nje ya Sex na ngono.
Mwanamke ni nusu ya mwanaume. Uwepo wake unajaza nafasi ya uhitaji wa kiroho wa mwanaume. Ukiwa na mwanamke ambaye unampenda na anakupenda anakujali na unajua kabisa kiasi kwamba asubuhi ukiwa unatoka kwenda mihangaikoni mkitazamani anakuonea huruma kuwa unaenda kuteseka na wewe unamuonea huruma kumuacha pekee yake kwa masaa kadhaa.
Nafsi yako ikijazwa na mahaba na uwepo wa mwanamke ule muda wa kuwaza ngono, kuwaza kujichua huwa unakosekana maana akikukumbatia upweke na ashiki za kingono zote zinakuachia haraka kama mtu aliyemeza Diclofenac kutibu maumivu ya kichwa na mwili.
Sasa wengi wa vijana wanaupweke sana sababu hakuna mabinti wanaotaka kuja kuishi nao katika nyakati hizi za utafutaji. Sasa spirit ya kujichua inawajaa sababu ya kukwepa misukosuko ya mahusiano maana inawagharimu sana mentally na wao wanataka amani na utulivu wa kufikiria sawa sawa.
Sent using
Jamii Forums mobile app