Hongera Kwa ujasiri.
Kujichua mara nyingi hutokea mtu awapo peke yake na hufanya jambo hili Kwa Siri katika mazingira ya upekee. Mojawapo ya njia za kuzuia hii Hali kama upo kwenye ndoa ni
1. kujaribu kuwa na ukaribu na mwenza wako. Mfano, wakati wa kuoga unaweza kwenda kuoga nae pamoja. Kama ni nyakati za mapumziko nyumbani, jitahidi sana kuwa karibu nae. Usijikalie peke yako.
2. Punguza matamanio yako ya kingono Kwa watu wengine. Kujichua huchukua taswira ya picha ya mtu alielengwa katika matamanio na Kisha mhusika hujaribu kuboresha Ile taswira kwenda kwenye mahitaji yake. Ikiwa Kuna Jambo unaona mwenzi wako analikosa, ni muhimu kuliboresha ili matamanio yako yawe kwake. Mfano: usafi, kuwa romantiki, sura ya kutabasamu na upole nk.
3. Kujichua ni kitendo kisicho Cha kiungwana na hakikupi Raha kama ambayo ungeipata kutoka Kwa mwenza wako. Badili muelekeo wa fikra zako na kukuona kama kitendo kichafu kisichofaa. Kujichua ni ubinafsi uliopitiliza. Ikiwa unampenda mwenza wako, dhamiria kukamilisha nae tendo la ndoa Kwa ufanisi mkubwa mno. Ondoa hayo mapicha picha kichwani na uanze kumpenda mmeo.
3. Mwisho, kuzuia Tabia mbovu kama hiyo, inahitaji ujasiri wa kuamua kuacha. Dhamiria kuacha. Fanya mazoezi, mweke mwenza wako karibu, muone kama yeye pekee ndo anaweza kutimiza haja yako ya Hilo tendo. Acha kuwa mbinafsi.
Mimi ni Dad165-Dingi mchanga, Father, mme ajae!