GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kuna mdada mmoja anatakiwa saa 10 hii awe ameshaamka ili ajiandae kwani anasafiri na basi la saa 11 na nusu kwenda mkoani kagera na kibaya zaidi ni mke wa mtu na tokea saa 9 kengele ya kumwamsha " alarm " imekuwa ikilia tu na yeye nadhani sijui ni kwa usingizi mtamu au " majamboz " ya mumewe anaizima na mpaka muda huu naandika uzi huu bado hajaamka na kujiandaa na imebaki saa moja tu basi analopanda lianze safari. nasikia uchungu sana kwani jana usiku aliniaga kuwa leo anasafiri na mpaka sasa bado hajaamka na napatwa na hamu ya kwenda kumuamsha ila kuna kizingiti kikubwa ambacho ni mumewe ambaye ni " mkorofi "na ana " wivu " balaa na ni mcheza " karate " maarufu tu haa mtaani kwetu hivyo naogopa! akili inanituma nijitolee nikamwamshe ila mwili unakuwa mzito kutenda na unasita sita. nawaombeni ushauri members wenzangu je nifanyeje ili niweze kumsaidia huyu dada jirani yangu aamke na awahi usafiri wa kwenda kagera? nipeni majibu ya haraka na upesi ili fasta fasta nimsaidie mwenzetu huyu. mama yangu kengele imelia tena sasa hivi jamaa namsikia anamwambia " zima na lala ". madirisha yetu hayapo mbali kivile!