S.M.P2503
Platinum Member
- Nov 25, 2008
- 3,689
- 7,145
Ndugu zangu, usiku wa kuamkia leo nimeota ndoto ambayo imenifanya nibaki na maswali mengi sana.
Katika ndoto hiyo, Freeman Mbowe alikuwa amefiwa na ndugu yake wa kiume, lakini sikufahamu kama alikuwa kaka yake au mdogo wake. Sina taarifa kwamba jambo hili limetokea kweli au kama Mbowe ana kaka au ndugu yake wa kiume; ninasimulia nilichokiona katika ndoto tu usiku wa kuamkia leo.
Nilienda msibani, na katika ndoto hiyo, jirani wa karibu kabisa wa Mbowe alikuwa Bwana Kishimba, yule mbunge machachari wa Kanda ya Ziwa. Hata hivyo, Kishimba hakufika kutoa pole na wala hakuchangia chochote katika msiba huo ingawaje alikuwa karibu sana na nikaona ni jiani yake Mh. Mbowe.
Mbowe mwenyewe alichangia shilingi milioni 500, huku sisi waombolezaji wengine tukichangia jumla ya shilingi milioni 424. Kwa hiyo, michango yetu yote kwa pamoja ilikuwa chini ya mchango wake binafsi.
Katika ndoto hiyo, Mbowe alionekana kulalamika kwamba alikuwa amechangia fedha nyingi kuliko waombolezaji wengine wote kwa pamoja. Nikabaki nikijiuliza: Kwa nini alalamike kwamba waombolezaji wamechangia kiasi kidogo kuliko yeye mwenyewe? Hivi, hata kwenye msiba kuna mashindano ya michango?
Ndoto ikaishia hapo.
Naomba msaada wenu kuelewa ndoto hii inaweza kuwa na maana gani. Asanteni, ndugu zangu.
Acheni Mizaha ni ndoto niliyoota... wanajimu wa kutafsiri waje watoe muongozo...