Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 51,453
- 41,274
Gentleman,Ndugu zangu, usiku wa kuamkia leo nimeota ndoto ambayo imenifanya nibaki na maswali mengi sana.
Katika ndoto hiyo, Freeman Mbowe alikuwa amefiwa na ndugu yake wa kiume, lakini sikufahamu kama alikuwa kaka yake au mdogo wake. Sina taarifa kwamba jambo hili limetokea kweli au kama Mbowe ana kaka au ndugu yake wa kiume; ninasimulia nilichokiona katika ndoto tu usiku wa kuamkia leo.
Nilienda msibani, na katika ndoto hiyo, jirani wa karibu kabisa wa Mbowe alikuwa Bwana Kishimba, yule mbunge machachari wa Kanda ya Ziwa. Hata hivyo, Kishimba hakufika kutoa pole na wala hakuchangia chochote katika msiba huo ingawaje alikuwa karibu sana na nikaona ni jiani yake Mh. Mbowe.
Mbowe mwenyewe alichangia shilingi milioni 500, huku sisi waombolezaji wengine tukichangia jumla ya shilingi milioni 424. Kwa hiyo, michango yetu yote kwa pamoja ilikuwa chini ya mchango wake binafsi.
Katika ndoto hiyo, Mbowe alionekana kulalamika kwamba alikuwa amechangia fedha nyingi kuliko waombolezaji wengine wote kwa pamoja. Nikabaki nikijiuliza: Kwa nini alalamike kwamba waombolezaji wamechangia kiasi kidogo kuliko yeye mwenyewe? Hivi, hata kwenye msiba kuna mashindano ya michango?
Ndoto ikaishia hapo.
Naomba msaada wenu kuelewa ndoto hii inaweza kuwa na maana gani. Asanteni, ndugu zangu.
Acheni Mizaha ni ndoto niliyoota... wanajimu wa kutafsiri waje watoe muongozo...
kwanza kabisa hiyo ni arlet na signal muhimu sana kwako binafsi, familia yako, ndugu, jamaa na marafiki zako wa karibu, kwamba kuna roho ya mauti inazengea zengea miongoni mwenu. Njia ya uhakika kuiepusha raho hiyo ni kuzama kwenye maombi na kuikemea sana roho hiyo ya mauti, na pakifanyika mzaha, basi ni wazi miongoni mwenu kuna atakae r.i.p as soon as possible.
Gentleman,
Mwenyezi Mungu huwasiliana, kuwaonya au kuwajulisha waja wake mambo mbalimbali yanayokuja mbele yao kwa namna nyingi, na ndoto ni moja wapo. Lakini tumekua na kiburi kuzingatia tahadhari hizo na wakati mwingine kuzipuuzia na kuzifanya porojo za kisiasa.
Gentleman,
lakini pia kupitia ndoto yako,
jambo lingine muhimu sana unaloarifiwa hapo ni kwamba, ikiwa patatokea msiba miongoni mwenu, basi suala la kiuvhumi, yaan pesa litakua changamoto kubwa na litaibua malalamiko na pengine mgogoro wa kifamilia, kwasabubu inaonyeha kuna baadhi ya family members watachanga zaidi na wengine hawatachanga kabisa na hapo ndipo mzozo wa kusimangana utaibuka na kuzua taharuki na timbwili msibani.
Gentleman,
hao wahusika ulioonyeshwa katika ndoto yako ni watu tu ambao wamekaa zaidi kwenye fikra zako za karibu, ndio maana wameonekana kirahisi kwenye ndoto yako ya msiba, but walengwa wa ndoto hiyo ni wewe binafs, members wa familia wako ,ndugu jamaa na marafiki zako wa karibu.
Ni kusali, kukemea na kuomba neema na baraka za Mungu bila kuchoka wala kukata tamaa gentleman🐒