Msaada: Tairi zipi ni Bora na Imara?

Kaka Kapo

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2012
Posts
547
Reaction score
344
Wasalaam!
Heri ya mwaka mpya 2018.
Ninampango wa kubadilisha tairi kwenye kigari changu ninaomba ushauri wenu kwa wenye ufahamu zaidi je ni tairi zipi bora na imara kati ya Michellin, Kumho na BF Goodrich? Je wanapatikana wapi dealers wa hizi brands. Je gharama zake zikoje. Maamuzi yangu yanategemea sana ushauri wenu wakuu.
Ahsanteni
 
chukua Michelin, zinapatikana kwenye petrol stations kubwakubwa na kwa wakala wao, kama upo dar nenda pale Victoria petrol station
Ahsante sana mkuu. unaweza kuwa unakumbuka bei ikoje
 
Mkuu, budget ndio itakayo sema. Kuna tyre size 14" zinauzwa hadi 85,000Tsh Kariakoo, wakati kuna brands size hiyo hiyo zinauzwa 450,000Tsh.

Me nadhani tungeanzia budget kwanza.

Kama budget sio issue basi Michelin ndio kila kitu.
 
Nimekupata mkuu budget yangu ni 200K@ ambayo ni 800K kwa zote nne. kwa bajeti hii naweza pata aina ipi kati ya hizo tatu.
 
Kama ww ni mtu wa rough road chukua bf Goodrich, kama ni wa lami sana chukua Michelin. Nenda Superdoll pale pugu road ndio dealer mkuu kwa tz, tena wana offer ukinunua tairi nne unapata moja ya bure
 
Kama ww ni mtu wa rough road chukua bf Goodrich, kama ni wa lami sana chukua Michelin. Nenda Superdoll pale pugu road ndio dealer mkuu kwa tz, tena wana offer ukinunua tairi nne unapata moja ya bure
ahsante boss, ngoja nitawatembelea the coming weekend.
 
Mzee baba chukua LingLong....hautajutia. Michelin ilikuwa zamani asaivi zinauzwa zikiwa mbichi sana. Ukitaka nalikupe number za FUNDI mtaalamu wa kuchagua tairi na atakusaidia sana. Mi nipo Dom ila yeye yupo dar
 
Vipi kuhusu ubora wa tairi aina ya Infinity na Goodride ...?
 
MKuu Kuna tairi wanaita YANA. Nilifunga kwenye Gari Mwaka 2011 nilipiga safari DAR - Dom hadi 2015 Tairi moja saizi 15 ni kati ya 350,000- 450000(stand to be corrected)
 
ungeweka matumizi ya gari pia ingerahisisha wewe kupewa ushauri mzuri.
kama gar linatumika kwa safari ndefu mara kwa mara, au ni la kutembelea tu, barabara unazotumia muda mwingi ni lami au vumbi, n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…