Msaada: Tairi zipi ni Bora na Imara?

MKuu Kuna tairi wanaita YANA. Nilifunga kwenye Gari Mwaka 2011 nilipiga safari DAR - Dom hadi 2015 Tairi moja saizi 15 ni kati ya 350,000- 450000(stand to be corrected)
Mbona hiyo miaka ndo expire date kwa tyre zote duniani?
 
nilichukua Linglong kwa shingo upande lakini ni mwaka wa pili sasa hivi ziko vizuri na kila baada ya miezi mitatu au minne natembea si chini ya km 1200 ,NA ninaishi porini lami naionja week end tuu
Wakuu ishu ya wheel alignment inanitesa

Hivi ni kwa muda gani exactly natakiwa kufanya?

Juzi nimetupa tyre mpya kisa hiyo ishu, niliumia hataree
 
Wakuu ishu ya wheel alignment inanitesa

Hivi ni kwa muda gani exactly natakiwa kufanya?

Juzi nimetupa tyre mpya kisa hiyo ishu, niliumia hataree
Pole sana tairi zililiwa upande mmoja?
kila Mara hasa unapoona umetembea safari ndefu au kabla ya safari Fanya wheel alignment,
Pia ukaguzi wa tairi jinsi zinavyolika kila siku ni muhimu jambo nyie wadada mara nyingi hamfanyi
 
Ndio mkuu zililiwa upande mmoja, upande wa kwa ndani ...mi sikaguagi gari niwe mkweli

Yaan tairi ukiendesha mda mrefu inavimba mpaka unatetemeka mwili, nikayavua bado mapya[emoji134]
 
Nimekupata mkuu budget yangu ni 200K@ ambayo ni 800K kwa zote nne. kwa bajeti hii naweza pata aina ipi kati ya hizo tatu.
Utapata Bridgestone,Wrangler labda na Dunlop kwa mbaali kwa kuwa ni size ndogo. Huwezi kupata Michelin wala BF Goodrich.
 
Nakusaidia tu jitahid ujifunze vitu, matusi hayatakusaidia. Huwezi hata sikumoja ujafananisha linglong na michelin yaani ni sawa na kufananisha tecno na iphone
Na huo ndiyo ukweli,ila kwa anaefaham Brand na ubora. Kuna mtu anaweza kuwa na gari Crown kali,akahisi ni saaa na BMW kali,japo kwa macho unaona kama ziko sawa,kumbe kwa vigezo vyote ni mbingu na ardhi,lakini only uwe una uelewa na brand na ubora wake
 
Ndio mkuu zililiwa upande mmoja, upande wa kwa ndani ...mi sikaguagi gari niwe mkweli

Yaan tairi ukiendesha mda mrefu inavimba mpaka unatetemeka mwili, nikayavua bado mapya[emoji134]
Jizoeze kukagua hata vitu vya kawaida,gari ukishaizoea ni rahisi kugundua kitu hata kwa observation tu ,
 
Kuna tairi zinaitwa PRACTIVA za mjapan,zitafute utuletee mrejesho hapa nadhani hutojuta!
 
Wakuu ishu ya wheel alignment inanitesa

Hivi ni kwa muda gani exactly natakiwa kufanya?

Juzi nimetupa tyre mpya kisa hiyo ishu, niliumia hataree
Kila ukibadili taili au ukitembea kilomita elfu kumi 10000
 
Sometime hata ile kanuni ya
High Quality High price itumike
Linglong vs Michellin [emoji16][emoji16][emoji16]
Tuwe serious ila budget ikigoma tutafute ile afadhali
 
kuna hizi za kichina Roadcruza,Wanda na comforser..zijaribuni..hamtojuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…