Msaada: Tatizo kwenye kadi ya gari

Msaada: Tatizo kwenye kadi ya gari

Planet FSD

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2019
Posts
455
Reaction score
948
Wakuu habari za muda huu? Miezi kama 6 iliyopita, nilinunua benz kwa mtu. Gari ni Mercedes E280. Nilikagua chassis number vizuri na kujiridhisha umiliki wake. Nimekaa nayo vizuri bila tatizo.

Siku chache zilizopita nikashauriwa niibadilishe umiliki. Katika kuiangalia vizuri kadi ya gari nikagundua model iliyoandikwa ni E250 badala ya E280. Kwa kweli nilishtuka sana. Nadhani nilikuwa na furaha sana wakati nanunua kiasi kwamba sikuona hiki kitu.

Nikamtafuta aliyeniuzia, naye akasema alinunua hivyo hivyo na alikaa nayo miaka miwili bila shida kwa hiyo kwake hakuona kama ni jambo kubwa. Kwa ufahamu wangu kuna vitu haviwezi kubadilishika kirahisi kwenye kadi ya gari kama chassis number.

Nahitaji msaada kujua je, nikibadilisha umiliki naweza kubadilisha na hiyo model isomeke E280 badala ya E250? Maana naona kama ni kitu kinachoweza kuniletea matatizo baadae.
 
Wewe hiyo E280 kwenye gari yako imeandikwa wapi?

Maana kwenye gari hawaandiki ila ukitumia VIN decoder unaweza kujua exactly model ya gari lako.

Tumia hii VIN decoder: Free online Mercedes-Benz VIN Decoder : MBDecoder

Hafu E250 na E280 ni gari sawa itategemea na mwaka, coz iyo 2.5L ndio ilikuja kua replaced na 2.8L engine, nimesahau mwaka tu.

Sema ulichopigwa ni kudanganywa umeuziwa cc2800 kumbe cc2500, less HP.

Kama sio case, we kabadirishe tu.
 
E250 na E280 ni gari sawa itategemea na mwaka, coz iyo 2.5L ndio ilikuja kua replaced na 2.8L engine, nimesahau mwaka tu.

Sema ulichopigwa ni kudanganywa umeuziwa cc2800 kumbe cc2500, less HP.

Kama sio case, we kabadirishe tu.
Mkuu kweli nilipigwa lakini nilipewa gari powerful. Nilisearch chassis number yake na ikaja E280, kwahiyo ni kweli gari ni E280 ila nashindwa elewa ilikuaje kadi ikaandikwa E250? Labda ni human error, sasa je naweza kubadilisha hiki kitu?
 
Nime edit hapo juu cheki.
 
Mkuu kweli nilipigwa lakini nilipewa gari powerful. Nilisearch chassis number yake na ikaja E280, kwahiyo ni kweli gari ni E280 ila nashindwa elewa ilikuaje kadi ikaandikwa E250? Labda ni human error, sasa je naweza kubadilisha hiki kitu?
Okay. Huyo mtu alifanya janja janja ili alipe kodi ndogo.

Maana cc2500 na cc2800 kodi tofauti.
 
Okay. Huyo mtu alifanya janja janja ili alipe kodi ndogo.

Maana cc2500 na cc2800 kodi tofauti.
Ohoo! Sasa hii ni shida ndo nilikuwa naiwaza. Kuna chochote naweza kufanya kusort out hili tatizo? Kabla jumba bovu halijaniangukia.Maana gari naipenda kwa kweli.
 
Unaweza badili, jipeleke TRA, things will be sorted out. That is one. Two, uwa naandikaga humu mara kadhaa, usikubali kununua any automobile kwa makubaliano kuwa transfer utafanya wewe. Hakikisha seller amekamilisha na wewe umeenda TRA kuhakiki.
Sema tu wabongo wengi mna akili sawa na za gwajima na polepole.
 
Haha, mkuu sina akili za hao bwana. Ila nashukuru itabidi niende huko nikaonane nao
 
Nishanunua pikipiki kwa mtu nkakutana na ishu kama yako kumbe jamaa alisajili ki ujanja ujanja nkaiuza fasta
 
Back
Top Bottom