Planet FSD
JF-Expert Member
- Oct 24, 2019
- 455
- 948
Wakuu habari za muda huu? Miezi kama 6 iliyopita, nilinunua benz kwa mtu. Gari ni Mercedes E280. Nilikagua chassis number vizuri na kujiridhisha umiliki wake. Nimekaa nayo vizuri bila tatizo.
Siku chache zilizopita nikashauriwa niibadilishe umiliki. Katika kuiangalia vizuri kadi ya gari nikagundua model iliyoandikwa ni E250 badala ya E280. Kwa kweli nilishtuka sana. Nadhani nilikuwa na furaha sana wakati nanunua kiasi kwamba sikuona hiki kitu.
Nikamtafuta aliyeniuzia, naye akasema alinunua hivyo hivyo na alikaa nayo miaka miwili bila shida kwa hiyo kwake hakuona kama ni jambo kubwa. Kwa ufahamu wangu kuna vitu haviwezi kubadilishika kirahisi kwenye kadi ya gari kama chassis number.
Nahitaji msaada kujua je, nikibadilisha umiliki naweza kubadilisha na hiyo model isomeke E280 badala ya E250? Maana naona kama ni kitu kinachoweza kuniletea matatizo baadae.