Kwamba!!:
Mi ntakubaliana na wewe kwamba hiyo sio sababu(cause/reason) ya mtu kunuka mdomo.✅
Lakini nitaendelea kushikilia hapohapo kuwa hii ni mojawapo ya kisababishi(factor) cha watu kunuka mdomo.
Tunaongelea kuchanganya maji na chakula bado
Unajua brother shida ya matatizo mengi ya afya ya siku hizi hayana msababishi mkuu mmoja (main causative agent). Lakini yanakuwa yanajengwa na vitendo na tabia kibao za kwenye mtindo wa kawaida wa maisha (lifestyle factors)
Basi hili la kunuka mdomo ni mojawapo!
Na matibabu yake yatahusisha kubadilisha mambo mbalimbali, tabia za ulaji zikiwamo. So nnamshauri mleta mada achambue mantiki ya kupewa ushauri fulani kisha afanyie kazi zoote zinazoendana na mantiki ya kurudisha afya ya tumbo (gut health)
Akiniuliza sababu majinachakula wakati mmoja ni tatizo nitamjibu kwamba: kitendo hiki hupunguza nguvu ya juisi za kumeng'enya chakula hicho chakula kutomeng'enywa vizuri na kinachacha.
Cheki madini hapa: (kama huna bando, maelezo ndo hayohayo)
View: https://youtu.be/-dVbfpXMmuk?si=s0OoMNwoFGa0uZX_