Msaada: Tatizo la harufu mbaya kinywani

Dah kumbe sipo pekeangu kama umefanikiwa nijuze dawa na Mimi kak.
 

Vp kaka.
 
kinywa chako kinatoa harufu mbaya sana, ni kali mno inatia kinyaa, inaleta kichefuchefu.

hivi ni kweli huhisi hali hiyo, hujishtukii au ndio maana wala huoni soni mdomo unatoa harufu mbaya halafu wewe ndio kwanza muongeaji mkuu hadi mate yanarukia watu πŸ’

tunaweza kusaidianaje kwenye hili, wengine mabosi kabisa ofsini πŸ’
 
Nimeenda kila hospitali ! Mwananyamala , Albert Kairuki, RABININSIA, Almandari posta na pharmacy ndo usisemeee! I’m totally tired of living!πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”
Nenda na muhimbili, na pia siku ukisikia madaktari bingwa kutoka nje wamekuja tafadhali kawaone

Bila kusahau jatibu na hizi hospitali za kichina/korea huwa wana matibabu ambayo unaweza kustaajabu kwa mafanikio lakini kwao kawaida sana
 
Sayansi ya hivi imepitwa na wakati
Kwamba!!:

Mi ntakubaliana na wewe kwamba hiyo sio sababu(cause/reason) ya mtu kunuka mdomo.βœ…

Lakini nitaendelea kushikilia hapohapo kuwa hii ni mojawapo ya kisababishi(factor) cha watu kunuka mdomo.

Tunaongelea kuchanganya maji na chakula bado

Unajua brother shida ya matatizo mengi ya afya ya siku hizi hayana msababishi mkuu mmoja (main causative agent). Lakini yanakuwa yanajengwa na vitendo na tabia kibao za kwenye mtindo wa kawaida wa maisha (lifestyle factors)

Basi hili la kunuka mdomo ni mojawapo!

Na matibabu yake yatahusisha kubadilisha mambo mbalimbali, tabia za ulaji zikiwamo. So nnamshauri mleta mada achambue mantiki ya kupewa ushauri fulani kisha afanyie kazi zoote zinazoendana na mantiki ya kurudisha afya ya tumbo (gut health)

Akiniuliza sababu majinachakula wakati mmoja ni tatizo nitamjibu kwamba: kitendo hiki hupunguza nguvu ya juisi za kumeng'enya chakula hicho chakula kutomeng'enywa vizuri na kinachacha.

Cheki madini hapa: (kama huna bando, maelezo ndo hayohayo)

View: https://youtu.be/-dVbfpXMmuk?si=s0OoMNwoFGa0uZX_
 
Kula huku unakunya maji kunarahisisha mmeng'enyo wa chakula na kubance kiwango cha chakula unachokula katika uwiano sahihi.
 
Kula huku unakunywa maji kunarahisisha mmeng'enyo wa chakula na kubance kiwango cha chakula unachokula katika uwiano sahihi.
Maji hayo yanatakiwa yaachiliwe kutoka mwilini (kuta za tumbo, kongosho na utumbo) yakiwa na uwiano sahihi wa vimeng'enya vya chakula na utindikali/besi.

Ukiyanywa wewe kama wewe wakati huo yanaenda kudhoofisha utindikali/besi ambao mwili ulishafanya hesabu kuwa unafaa kulingana na chakula husika.

Basi yanywe mapema ya kutosha kama dakka 30-40 kabla ya chakula. Halafu mwili wenyewe ndio utajiamulia uloweshe chakula kwa kiwango gani.

Sio mbaya, kwa vyakula vikavu sana (mfano) ukapata na maji kiasi kusaidia umezaji lakini kuna kiwango stahiki
 
Endelea kufanya tafiti zaidi , sayansi hubadilika mkuu.
 
Hili jambo unacheka tu ila lilisha kuwa debate kubwa sana kwa maprof nguli kwa chuo nilichosoma ndio maana nmekuambia fanya tafiti upya.
 
Hili jambo unacheka tu ila lilisha kuwa debate kubwa sana kwa maprof nguli kwa chuo nilichosoma ndio maana nmekuambia fanya tafiti upya.
Ndiyo nasikia mara ya kwanza kuwa kunywa maji wakati wa chakula siyo vizuri. Mbona duniani kote ndiyo utaratibu? Sijaona watu wenye culture ya kula bila maji pembeni.
 
Ndiyo nasikia mara ya kwanza kuwa kunywa maji wakati wa chakula siyo vizuri. Mbona duniani kote ndiyo utaratibu? Sijaona watu wenye culture ya kula bila maji pembeni.
Ni kweli ila kuna Prof niliona anaelezea ni vizuri kiafya kwanza unapunguza kiasi cha chakula unacho kula na inasaidia mmeng'enyo vizuri zaidi.
 

Bad breath caused by tonsil stones Kuna mabaki ya chakula huwa yakwama kwenye sehemu/ chemba/ vyumba ndani ya mdomo ambavyo ni ngumu kuvitoa kwa kutumia mswaki (tradition) au kwa kusukutua.

Hizo chemba hukusanya mabaki ya chakula na bacteria tofauti tofauti ndani ya kinywa. Na mara nyingi mdomo unapopata bacteria wabaya husababisha tonsils glands kuvimba kuleta maumivu wakati wa kumeza au kinywa na sio kwa kunywa vitu vya baridi kama tulivyohaminishwa.

Unaweza kuwa na hizo tonsils stone bila tonsils glands kuvimba na kuuma. Tonsils glands kuvimba na kuuma zaidi husababishwa na bacterial infections (Bacteria wabaya) wanazofuata mabaki ya vyakula kwenye hizo tonsils stone kinywani.

Mkusanyiko huo wa mabaki ya chakula hujitengeneza kama vimawe (calcite) ndani ya chemba za kinywa kama inavyoonekana kwenye picha.

Hivyo vimawe kikiwa ndani ya kinywa chako huwezi jisikia inatoa harufu mbaya kinywani.

Kuthibitisha kuwa unanuka au unaharufu mbaya mdomoni, chukua kioo jimulike mdomoni na ukiweza kutoa Kijiwe hata kimoja. Ukikinusa ndio utajua harufu iliyopo kwenye mdomo wako.

Njia za kuondoa tonsils stone

Kuna njia kadhaa za kuondoa mawe ya tonsils (tonsil stones). Hapa kuna baadhi ya njia hizo:
  1. Kusafisha kwa kutumia maji ya chumvi: Osha kinywa chako kwa kutumia maji ya chumvi ili kuondoa mawe ya tonsils. Unaweza kutumia suluhisho la maji ya chumvi ya joto na kuosha kwa upole eneo la tonsils.
  2. Kupiga dawa ya kusafisha kinywa: Matumizi ya dawa ya kusafisha kinywa yenye viungo kama chlorhexidine au maji ya mkunjo (peroxide) yanaweza kusaidia kusafisha na kuondoa mawe ya tonsils.
  3. Kuondoa kwa kutumia vidole au toothbrush: Kwa uangalifu, unaweza kutumia vidole au brashi ya meno ili kuvuta au kusukuma nje mawe ya tonsils. Hakikisha usifanye hivyo kwa nguvu ili usisababishe madhara kwenye tishu za tonsils.
  4. Kunyoa tonsils (tonsillectomy): Kwa watu wenye matatizo ya mara kwa mara ya mawe ya tonsils au hawajapata mafanikio na njia nyingine, daktari anaweza kupendekeza kuondoa tonsils kwa njia ya upasuaji.
Ni muhimu kuzungumza na daktari wako ikiwa una matatizo ya mara kwa mara ya mawe ya tonsils au kama njia hizi hazisaidii, ili upate ushauri wa kitaalamu na matibabu sahihi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…