Msaada: Toka May 2023 hadi sasa sijapata passport, nimeambiwa mimi sio mtanzania

Wewe utakuta ndio hao wanao watafuna watanzania masikini. Mtu hana kazi anatapatapa na maisha vipi atapata hela za kuhonga apewe haki yake?
Kama wabasema sio mtanzania wamwambie kwa maandishi kitu gani kimepungua kuonesha yeye sio mtanzania.
Hawa nguchiro ndio wanao rudisha hili taifa gizani
 
Mbona mimi huu upuuzi sikumbani nao? Yaani mjinga mjinga fulani kwa upuuzi wake aniambie mimi sio mTz.
Wanaweza na unaweza usifanye chochote pana mtu walimwambia aonyeshe kaburi la nyanya yake yeye aliwajibu waanze wao kwanza ni Dr Bagonza usipopata matatizo ni kushukuru tu mkuu sio Ujanja wowote mimi kuna siku hapo KIA bwana mdogo aliniuliza maswali mengi kipindi cha Magu wakati nimeshuka nilimjibu kwa ustaarabu saana mpaka wenzie wakamwambia achana nae aende tu baadae nilikuja kumtafuta Chuga Uhamiaji nikaambiwa kapelekwa mipakani hawa vijana wakiamua wanafanya chochote kwa mtu yeyote ili mradi wapate rushwa au sifa..naumia kuona Mtanzania akipata hayo matatizo kwenye Nchi yake labda asiwe Mtanzania kweli..
 
Mkuu nenda kaonane na Boss wao hata wakitaka kuandika barua andika usitoe rushwa kwenye haki yako mimi katika vitu sijawahi kutoa rushwa ni Passport ya Tanzania maana ni haki yangu kabisaa nimetoa karibu passport zaidi ya 8 zile za zamani kabla ya hii mpya toka nianze kuchukua ila nachukua kwa pesa ile ile tu...
 
Hawawezi ndio maana mpaka leo hakuna aliejaribu. Mimi ni Mtanzania tena Mtanganyika hakuna anaeweza kubadili hilo. Hakuna.
 
Sasa unamwambia aende kufanya nini wakati unasema mtu anaweza kuamua tu kuwa wewe sio mtz na hakuna kitu unaweza kufanya?
 
Pole sana mkuu
Umeombea passport ofisi za mkoa gani kama hutojali?
 
Nadhani na kuamini kuwa kuna kasoro kwenye nyaraka ulizowasilisha kama vielelezo vya kupata pasi ya kusafiria. Pasi hutolewa baada ya kuhakiki uraia. Umesema unatoka Kigoma na kabila lako ni muha. Lakini umesema pia kuwa wazazi wako walihamia Morogoro tangu 1992 na wewe hukuzaliwa Kigoma.

Kwa kuwa wazazi wako walizaliwa Kigoma na baadaye kuhamia Morogoro, unapaswa kupeleka vyeti vya kuzaliwa wazazi wako, vyeti vya darasa la saba/chuo/ubatizo au cheti cha kiapo kutoka mahakama za Kigoma walipozaliwa mmoja wa wazazi wako au wote.
Kwa maneno mengine wazazi wako wanatakiwa kupitia mchakato wa uhakiki uraia wao kabla ya wewe kupata pasi ya kusafiria. Mchakato mzima unatakiwa uanzie uhamiaji kitengo cha uraia na huchukua muda mrefu kidogo.

Kusanya nyaraka zote muhimu, futa kabisa mawazo ya kutoa rusha kisha kapige kambi ofisi za uhamiaji hadi kieleweke..... Kila aina ya kheri kwako!.
 
 
Wewe siumunganishe sasa unamwambia amtafute mtu wakati wewe pia una conmection bora hata usinge comment tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…