Msaada: Toka May 2023 hadi sasa sijapata passport, nimeambiwa mimi sio mtanzania

Msaada: Toka May 2023 hadi sasa sijapata passport, nimeambiwa mimi sio mtanzania

Hivi unavyoita watu Waheshimiwa hata mimi naona kabisa wewe siyo m Tanzania.

La maana kabla ya yote huko wanataka pesa mbele kama tai usiende na lugha laini ukajua watakuogopa.

Tafuta kishoka hivi hivi utaishia kuita Mheshimiwa hapq hapa bongo
Hahahahhah Mamndenyi umeua... sema hata kama una hela ukienda kizembe unaweza sumbuliwa hata kidogo kwasababu na wao sio mafala wanakuwa wana kauoga fulani kwenye ishu za rushwa. Ila ukielewa Codes zao basi hiyo passport ni chini ya wiki umepata.
 
Hawawezi ndio maana mpaka leo hakuna aliejaribu. Mimi ni Mtanzania tena Mtanganyika hakuna anaeweza kubadili hilo. Hakuna.
Haujakutana na maswahiba acha ubishi brother pana dogo mmoja ni Dereva wa Taqwa miaka nenda rudi anachukua mkwaju akakutana na hiyo kadhia kuwa sio mbongo na ni Mtanzania alipeleka vielelezo wakampa mkwaju wake na sio passport ya kwanza ilikua sijui ya tatu nakumbuka...
 
Sasa unamwambia aende kufanya nini wakati unasema mtu anaweza kuamua tu kuwa wewe sio mtz na hakuna kitu unaweza kufanya?
Brother nakwambia hawa watu wa chini wakishika faili lako hautawafanya kitu mpaka upande ngazi ndio utafanikiwa na pia wao sio kosa kumshuku mtu yeyote ndio maana boss wao hatamuona aliemshuku ana kosa hayo mambo yapo Uhamiaji kila kukicha hasa kwa wanaochukua passport ingine wakati ya kwanza alikua nayo hivi vitu kwa Wasafiri wengi wanakutana navyo brother usiwe mbishi kama vitu huvijui..
 
Hapa ndipo tunapofeli. Vijana wetu wanamaliza chuo hatuwapi ajira wanarundikana tu ili waendeshe boda. Badala ya kuwafungulia njia ili waende huko wakapambane, kupata exposure na kuona dunia inavyokwenda, tunawafungia ndani. Mataifa mengine wanawafungulia vijana wao sisi ndiyo kwanza tunawazuia. Kuna shida mahali!
 
Hapa ndipo tunapofeli. Vijana wetu wanamaliza chuo hatuwapi ajira wanarundikana tu ili waendeshe boda. Badala ya kuwafungulia njia ili waende huko wakapambane, kupata exposure na kuona dunia inavyokwenda, tunawafungia ndani. Mataifa mengine wanawafungulia vijana wao sisi ndiyo kwanza tunawazuia. Kuna shida mahali!
Mzee Kikwete kwenye hili alifungua sana njia kutoa Passport kipindi chake ilikua sio Big ishu na pia watu wengi walisafiri sana..
Kuwapa passport Watanzania sijui wanaona kitu gani daah imefikia mtu akipata Passport anashukuru kweli hata waliompa msaada hawasahau wakati SA ukiwa na ID unaweza kuomba uchukulie popote pale hata Bank wanaweza kuipokea sisi tuna mambo ya kijima mno..
 
Pole sana, mimi nilihangaika sana kupata hapa Mwanza nikaombwa hadi rushwa ya ngono nikakataa, nikasema kama kupata passport ni kazi hivi basi siitaki.

Nikapata kazi Dodoma nikaomba migration ya Dodoma nikaunganishwa na baba mmoja hivi hapo Migration hakuniomba chochote niliombwa Doc za sababu ya kusafiri, G akanitumia barua ya mwaliko na passport copy yake ndani ya wiki mbili nikapata passport, nikasema nimpe asante yule baba aliikataa kata kata akasema nimekusaidia tu.

Tafuta mtu akuunganishe utaipata haraka tu
Yaani ni rushwa tu pale migration au umjue mtu baasi
 
Tanzania rushwa haikwepeki, hizo gharama ulizotumia kusafirisha wazazi mpaka Dar ungezitumia kuhonga, issue Yako ingekuwa solved.

Tafuta afisa mmoja hapo uhamiaji, muelezee scenario Yako omba akusaidie issue Yako, huku uliahidi kumlinda.

Passport huwa haizidi siku 21, na upo uwezekano wa kuipata ndani ya wiki 1, itategemeana na mazingira Yako.
Zote hizi nyingi sanaaa broo ndani ya siku Moja passport inapatikana,nshawafanyia watu mipango humu
 
Uhamiaji wana vituko sana. Nilikua nafuatilia NIDA wakaniuliza bibi yangu kazaliwa wapi na kasoma shule gani. Bahati nzuri hiyo siku nilikua nimeongozana na bibi yangu halafu wanamjua.
 
Uhamiaji wana vituko sana. Nilikua nafuatilia NIDA wakaniuliza bibi yangu kazaliwa wapi na kasoma shule gani. Bahati nzuri hiyo siku nilikua nimeongozana na bibi yangu halafu wanamjua.
Wazazi wangu sijui shule walizosoma, sembuse babu na bibi? Hao kweli wazinguaji
 
Back
Top Bottom