Msaada: Toka May 2023 hadi sasa sijapata passport, nimeambiwa mimi sio mtanzania

Msaada: Toka May 2023 hadi sasa sijapata passport, nimeambiwa mimi sio mtanzania

Izo gharama ulizo tumia kupitia njia sahihi wenzio wana kuonyesha unge zitumia kwa njia isio sahihi ata mwezi usinge maliza hii nchi ni trash
 
Waheshimiwa, habari ya kazi na pole kwa majukumu.

Waheshimiwa, mwaka jana 2023, nilibahatika kupata ufadhili wa kwenda masomoni nje ya nchi hivyo nililazimika kutafuta passport. May 2023, nilifika ofisi za uhamiaji Kurasini na viambatanisho vyangu vyote kufanya ombi la passport. Nilifanikiwa kukamilisha ombi langu na kulipia gharama zote.

Waheshimiwa, toka May 2023, hadi sasa sijapata passport. Nilipojaribu kufatilia niliambiwa siwezi kupata passport kwa sababu mimi sio Mtanzania.

Waheshimiwa, mimi nimezaliwa, kukua na kusoma ndani ya mipaka ya Tanzania kama viambatanisho vyangu vinavyoonyesha. Wazazi pamoja na babu zangu ni watanzania.

Waheshimiwa, nimefanya jitihada zote pamoja na kuleta wazazi kutoka kijijini na kwenda nao uhamiaji bila mafanikio. Nimeingia gharama kubwa sana kufuatilia hili swala ukizingatia mimi ni kijana niliyemaliza chuo na bado sijabahatika kupata kazi. Kadhalika kuna uwezekano nikapoteza ufadhili niliobahatika kuupata kama sitapata passport kwa wakati; ndoto na maisha yangu kiujumla yataharibika kwani elimu ndio tegemeo langu kujikwamua kiuchumi.

Waheshimiwa nimekuwa ni MTU wa mawazo sana pamoja na misongo. Naombeni msaada wenu kutokomeza ukosefu wa haki katika nchi hii.

Ni mimi kijana mwenzenu Mwenyezi Mungu awabariki mnapoendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa.

Mkuu haya ma jamaa ni ya hovyo sana mtafute yerico nyerere atakusaidia
 
Utawala wa KIZIMKAZI ni RUSHWA TU ukitoa ni ndani ya cku 3_5 unapata. Waziri mwenye dhamana ya kupambana na rushwa alisema vitendo vya rushwa Kwa sasa vimeshamili mnoo. Jiongeze tu
 
Hii nchi hi nakumbuka passport nilijaziwa hapo hapo uhamiaji HQ na date of issue ulikuwa ijumaa na sku hyo hyo jion akanitumia picture haijamalizwa printiwa jtatu asubuh nikapewa,

Nb: officer mmoja alijichanganya kutaka kunizoea kunihoji Nika piga simu alitukanwa moja mpaka nikamuona hawez kuniangalia machoni ,,,, et passport unaenda wap? Shenzziiii
 
Haya mambo yanawakuta wengi sana.ila wahusika wakiwa kwenye vyombo vya habari wanaongea upuuzi mtupu hadi unaweza kufikiri nchi imezaliwa upya.Wanachokiongea na yanayofanyika uku maofisini ni mbingu na ardhi.
 
Kwenye vyeti kabila si linaonesha
Ni kwel lakn ingekuwa mwanzo ukasema msukuma na ukawa unajua Cha kuzugia usumbufu unapungua lakn ukisema unatoka kigoma,ngara,kabanga,tunduma,sirari, aiseee utapgishwa route mpka utoe chochote all in all hii nchi jitahidi uwe na connection tu.
 
Ungejaribu kwanza kuondoa mikosi uliyonayo au kupunguza ujuaji au kuacha kutukana mamba kabla hujavuka mto au kujaribu kuwa msiri.
Malizana na hizo au mambo yatakaa sawa usisahau za kuambiwa + na za kuzaliwa.

Ndio maana nasema chuo mnaendaga kusomea. Ujinga mambo ya kutumia akili wewe unaenda vijijini kuleta wazazi. Unatakiwa kusoma upepo .

Ya kaisari mpe kaisari, kuna muda wa kuomba haki na kuna muda wa kudai haki!! Kuna muda unamtongoza mke wako wa ndoa[emoji28][emoji28][emoji28]
Siyo kweli
 
Una sura iliyochongokan kama Kagame? Hiyo inaweza kuwa sababu, otherwaise toa rushwa tu, wanakutemgemezea mazingira ya rushwa hao washenz
 
Pole sana, mimi nilihangaika sana kupata hapa Mwanza nikaombwa hadi rushwa ya ngono nikakataa, nikasema kama kupata passport ni kazi hivi basi siitaki.

Nikapata kazi Dodoma nikaomba migration ya Dodoma nikaunganishwa na baba mmoja hivi hapo Migration hakuniomba chochote niliombwa Doc za sababu ya kusafiri, G akanitumia barua ya mwaliko na passport copy yake ndani ya wiki mbili nikapata passport, nikasema nimpe asante yule baba aliikataa kata kata akasema nimekusaidia tu.

Tafuta mtu akuunganishe utaipata haraka tu
Asante gan mkuu ulitaka kumpatia mbaba wa watu?
 
Back
Top Bottom