Msaada: Toka May 2023 hadi sasa sijapata passport, nimeambiwa mimi sio mtanzania

Msaada: Toka May 2023 hadi sasa sijapata passport, nimeambiwa mimi sio mtanzania

Hapa ndipo tunapofeli. Vijana wetu wanamaliza chuo hatuwapi ajira wanarundikana tu ili waendeshe boda. Badala ya kuwafungulia njia ili waende huko wakapambane, kupata exposure na kuona dunia inavyokwenda, tunawafungia ndani. Mataifa mengine wanawafungulia vijana wao sisi ndiyo kwanza tunawazuia. Kuna shida mahali!
Roho mbaya
 
Waheshimiwa, habari ya kazi na pole kwa majukumu.

Waheshimiwa, mwaka jana 2023, nilibahatika kupata ufadhili wa kwenda masomoni nje ya nchi hivyo nililazimika kutafuta passport. May 2023, nilifika ofisi za uhamiaji Kurasini na viambatanisho vyangu vyote kufanya ombi la passport. Nilifanikiwa kukamilisha ombi langu na kulipia gharama zote.

Waheshimiwa, toka May 2023, hadi sasa sijapata passport. Nilipojaribu kufatilia niliambiwa siwezi kupata passport kwa sababu mimi sio Mtanzania.

Waheshimiwa, mimi nimezaliwa, kukua na kusoma ndani ya mipaka ya Tanzania kama viambatanisho vyangu vinavyoonyesha. Wazazi pamoja na babu zangu ni watanzania.

Waheshimiwa, nimefanya jitihada zote pamoja na kuleta wazazi kutoka kijijini na kwenda nao uhamiaji bila mafanikio. Nimeingia gharama kubwa sana kufuatilia hili swala ukizingatia mimi ni kijana niliyemaliza chuo na bado sijabahatika kupata kazi. Kadhalika kuna uwezekano nikapoteza ufadhili niliobahatika kuupata kama sitapata passport kwa wakati; ndoto na maisha yangu kiujumla yataharibika kwani elimu ndio tegemeo langu kujikwamua kiuchumi.

Waheshimiwa nimekuwa ni MTU wa mawazo sana pamoja na misongo. Naombeni msaada wenu kutokomeza ukosefu wa haki katika nchi hii.

Ni mimi kijana mwenzenu Mwenyezi Mungu awabariki mnapoendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa.

Basi tu umemua kuwa mnyonge, kama wewe sio mtanzania wanatakiwa wa ku arrest, rudi hapo waambie wa ku arrest urudishwe nchi ambayo wanajua wewe ni raia wao, mnakuwa wanyonge ndoo mana haki zenu zinayumbishwa, hamjui ku argue, kubisha au kuhoji....

Angalizo:

- Kama una element ya uraia wa kuunga usithubutu kuhoji, nenda pole pole.
 
Jaribu kumuona MKUU WA MKOA
 
Nikweli wazazi wanatokea kigoma. Mimi nimezaliwa moro
HV kwanin watu wengi kutoka kigoma wamejazana morogoro

Wahaa Ni wengi mno Moro
Hat mm nkngekuwa afsa wa uhamiaji ningekusumbua snaa sna Hadi nijue umetokeaa wapi

Lashvyo waambie Basi wakuambie wewe Ni raia wa nchi gani ili ukaombe passport huko
 
Hii kitu mnajadili sijui Passport ndio nini? Au inatokana na passport size huwa wanatuomba kwa mtendaji wakati unaomba mkopo?
 
Ofisi nyingi za umma kwa sasa ni hivyo hivyo tu.

Mahakamani,alaaniwe aliyeleta utaratibu wa pesa za mirathi kupitia kwenye mirathi accounts za mahakama na wao ndiyo wanaweka kwenye accounts za warithi.

Ni urasimu usioelezeka,km una vipesa vyako bank na hakuna anayejua Password yako siku ukifa utanufaisha watendaji wa mahakama tu.
 
Kule
Sasa hapo ndo shangaa utakuta ambaye sio MTANZANIA na anapewa PASSPORT (mimi namjua mrwanda) alipewa passport na anayo mpaka sasa lakini NIDA walimkatalia kumpa kitambulisho ila PASSPORT anayo ndio jiuilize jijibu mwenyewe.

Sasa hapo MTANZANIA halisi FIGISU kibao dah! ROHO mbaya sana
Kule wizarani kumejaa watutsi na wanyarwanda na wanafahamiana sana na kusaidiana sana. Kwa serikali ya samia huyu, hajui chochote na wanajiimarisha Sana.
 
Brother nakwambia hawa watu wa chini wakishika faili lako hautawafanya kitu mpaka upande ngazi ndio utafanikiwa na pia wao sio kosa kumshuku mtu yeyote ndio maana boss wao hatamuona aliemshuku ana kosa hayo mambo yapo Uhamiaji kila kukicha hasa kwa wanaochukua passport ingine wakati ya kwanza alikua nayo hivi vitu kwa Wasafiri wengi wanakutana navyo brother usiwe mbishi kama vitu huvijui..
Sivijui? Unafikiri sijasafiri? Kwamba sijamiliki passport? Nishabadili passport kuanzia ile ya picha ya kubandika hadi hii ya sasa hivi. Hakuna wa kusema mimi sio mTz kijingajinga. Hakuna. Labda huelewi nasema nin. Ninachosema hakuna ofisa atakaeamua kwa utashi wake kuwa mimi si mTz. Yaani aamke tu huko aseme mimi sio mTz wakati ushahidi wote upo hapo hakuna.
Anacholalamika huyu kijana ni kuwa ana ushahidi wote wa uraia halafu mjjnga mmoja anaamua tu kumsumbua kuwa sio raia haikubaliki.
 
Basi tu umemua kuwa mnyonge, kama wewe sio mtanzania wanatakiwa wa ku arrest, rudi hapo waambie wa ku arrest urudishwe nchi ambayo wanajua wewe ni raia wao, mnakuwa wanyonge ndoo mana haki zenu zinayumbishwa, hamjui ku argue, kubisha au kuhoji....

Angalizo:

- Kama una element ya uraia wa kuunga usithubutu kuhoji, nenda pole pole.
Wadau humu wameshamuelekeza cha kufanya ila jinsi waha walivyo wabishi atajifanya haelewi.
 
Ndio kawaida yao hao jamaa, umezaliwa na kukulia bongo kisha ukapata pasport ya nje ili ukasake maisha kule au kusoma, siku unarudi maskani hawakutambui kama wewe ni raia, na wataendelea kula hela zako mpaka basi. Hao jamaa hawafai hata kidogo.

Katika sekta ambazo nimetokea kuzichukia ni Immigration, TRA na TANESCO

Hata nikisikia mmoja wao amekufa kwa ajali wala siumii/sisikitiki.
 
Ungejaribu kwanza kuondoa mikosi uliyonayo au kupunguza ujuaji au kuacha kutukana mamba kabla hujavuka mto au kujaribu kuwa msiri.
Malizana na hizo au mambo yatakaa sawa usisahau za kuambiwa + na za kuzaliwa.

Ndio maana nasema chuo mnaendaga kusomea. Ujinga mambo ya kutumia akili wewe unaenda vijijini kuleta wazazi. Unatakiwa kusoma upepo .

Ya kaisari mpe kaisari, kuna muda wa kuomba haki na kuna muda wa kudai haki!! Kuna muda unamtongoza mke wako wa ndoa[emoji28][emoji28][emoji28]
Nadhnani umesahau pia kuna muda wa kununua haki
 
Mie passport ilichukua siku 2 tu kupata jaribu kuongea na watu vizuri. Waarabu na wahindi wanazipata sembuse we Mtanganyika?
 
Sivijui? Unafikiri sijasafiri? Kwamba sijamiliki passport? Nishabadili passport kuanzia ile ya picha ya kubandika hadi hii ya sasa hivi. Hakuna wa kusema mimi sio mTz kijingajinga. Hakuna. Labda huelewi nasema nin. Ninachosema hakuna ofisa atakaeamua kwa utashi wake kuwa mimi si mTz. Yaani aamke tu huko aseme mimi sio mTz wakati ushahidi wote upo hapo hakuna.
Anacholalamika huyu kijana ni kuwa ana ushahidi wote wa uraia halafu mjjnga mmoja anaamua tu kumsumbua kuwa sio raia haikubaliki.
Mkuu kwani mimi nimesema inakubalika haikubaliki ila ndio nimesema wapuuzi wengi wanafanya hivyo kuwa na passport sio ndio kujua matatizo ya Uhamiaji ndio maana nimesema labda uwe mgeni ila mfumo wa Uhamiaji sasa hivi yaani ofisa anaweza kublock faili lako lisiendelee na hakuna wa kumhoji ukiruka daraja ndio ataulizwa mimi nilikua sijui kama wewe hivyo ila baada ya vijana wangu wengi tunapakia pakia mizigo na magari kutoka SA baadhi yao wamekumbana na kadhia hiyo kama una Mkwaju na haujapata matatizo unaweza usijue kuwa wengine wanapata matatizo maana hata mimi sijawahi kupata huo usumbufu..Passport zinazosimamishwa kufanyiwa kazi kuanzia Mbeya,Kigoma ,Arusha na Daslm zipo nyingi sana..
 
Back
Top Bottom