Msaada tutani, CCM mna mgombea wa kukabiliana na mabadiliko yanayokuja duniani kupitia Rais Trump?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Hellow Tanganyika,

USAID inadaiwa kufutwa, makampuni Toka nje yanafunga ofisi, misaada ya madawa inaondoshwa nk nk

Nawauuliza swali dogo tu, maana muda Bado upo na uchaguzi haujatangazwa Bado, hivyo kutangaza wagombea sasa Bado Si HOJA sana, mabadiliko yaweza fanyika.

Tujiulize yafuatayo;

1. CCM tunaye mgombea KITI kikuu awezaye kuwasaidia wananchi kujitegemea, kuishi bila kutegemea misaada Toka nje?

2. Mnaye mgombea anayeweza kufidia upungufu wa budget utakaoondolewa na marekani na World bank Kwa Nchi yetu Kwa kujifunga mkanda kubana matumizi ya serikali wakati huo huo akilipa deni linalokatibia Trillion 100?

3. Mnaye mgombea anayeweza kuwatisha wezi wa pesa za umma Ili makusanyo yatoshe maana misaada hamna?

Muda wa kufanya mabadiliko Bado upo, hamjachelewa,

Wakati mkiendelea kujibu maswali hayo, wananchi tunajiuliza,

1. Vyama vya upinzani, je vinaweza kutuletea mgombea ataeendana na mabadiliko yanayokwenda kuipata Dunia?

Niko pale Nasubiri kuelimishwa.

Karibuni πŸ™
 
Kamwe usitegemee waelewe hao kuna anguko kubwa la uchumi linakuja, kuna gonjwa linakuja, sector ya fedha inaenda kuanguka, kwa kifupi mvinyo mpya kiriba kipya ukilazimisha mvinyo mpya kwenye kiriba cha zaman lazima kipasuke na hakika kuna taasisi, vyama, serkali na vingine vingi vinaenda kupasuka asikiaye na afahamu
Mifumo inawekwa tayar tayar kumkaribisha mpinga kristo.
 
mgombea si walishamtangaza dodoma mkuu
 
Mimi siyo mtabiri, lakini katika hili naiona tanzania ikifeli pakubwa sana hasa upande wa afya kwa kukosa vifaa tiba na dawa muhimu za binadamu!! Kwa hivyo mtawala ajeye anatakiwa mtu mwenyew uthubutu mkubwa wa kuitetea nchi yake hata kufa.
 
Mwigulu atakuja na tozo ya viatu sasa maana kwingine kote amemaliza
 
Na mfumo Toka Mbinguni unamtaka Nabii, Mlawi akalie KITI Ili Kupambana na mfumo wa mpinga Kristo unaoandaliwa uanze kufanya KAZI,

Nchi hii ni Makao makuu ya Afrika nzima kama lango,

Hili jambo tumelisema sana mnaziba masikio,

Ni sharti mbadilike au mbadilishwe!!

Niliona kundi kubwa la wananchi wakiwakimbiza wanasiasa wakiwaambia ninyi ndio mmetufikisha hapa,

Muda Bado upo, badilisheni haraka,

Kamwe mwanadamu hawezi kushindana na Mungu akashinda.

Tusubiri πŸ™
 
Hakika USA haieleweki🀣🀣🀣🀣.. Bananchi bamechagua dikiteta na tairant.

Empires zote zilianguka baada ya Viongozi wao kujitutumua na madaraka kama haya tunayoyaona.

Hakuna nchi yeyote ile kwa sasa Duniani inayoweza kukabiliana na ubeberu wa Trump zaidi ya China na Russia. sasa ndio mtajua Dola sio polisiπŸ˜…πŸ˜πŸ˜πŸ˜
DOLLAR ni faranga bana.

"UNACHEZA NA DOLA"
 
Kanuni ya CCM ni moja tu amboyo ni sharti mwanao CCM awe upande wa mwenyekiti. Hata akiwa mwenyekiti kichaa kama Mh. Jiwe wao watamuunga mkono, wataandamana kila siku kumuunga mkono.
Sasa ujio wa Trump unamlazimisha nasi tupate KICHWA aina yake.

Tofauti na hapo,

Tutalimia meno!
 
Samia atawezq tena sana tu ila angekuwa yule bwana tungekwisha
 
Deni la Taifa ni shilingi ngapi sasa?

Mishahara italipika ilhali matumizi ya serikali kwenye anasa yakiwa pale pale?
Jpm kaacha deni la taifa trillion 68 wakati alikuta trilion 40 tu. Halafu alikuwa anakopa kimya kimya na kutipiga fix kwamba anatumia hela za ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…