Msaada unahitajika maana naona kichwa kinaelekea kupasuka

Unamgawa kisha iweje sasa, kwani ww huna chumba..? Nafuta mdada wa kazi ambae atakuja na kushinda nae mpaka utakapo rudi kutoka katika mizunguko yako mdada anarudi kwao ww unabaki na mwanao. Ufanye hivyo kutokana na kuwa na chumba kimoja cha kuishi.
 
Umenena vyema,huyu inavyoonekana hakuona thamani ya baby mama wake.Inawezekana hata alikua hatoi matumizi na Mama mwenyewe hakua na kipato hivyo kaona ngoja amfunze adabu japo hata mtoto anateseka.Ushauri wangu ,mtafute baby mother wako muongee muyamalize kwa ustawi wa mtoto wenu.
 
Yani huyu mwamba kama anatania vile,Myaani umpe mtu mtoto amchukue moja kwa moja na wewe baba upo kisa huna muda? Huyo mtoto wa kwako kweli au unatania hapa? Kama ni kweli hebu jaribu kuwa mwanamume husiwe mwanaume.
 
Eshimuni mama zenu kenge nyie. Huo ndio msoto huwa wanawake wanapitia mkiwakimbia na kuwaacha na watoto. Pambana tu hadi kieleweke, sio mama kakimbia nawe unataka kumuuza mtoto.
 
Ninakuomba sana usimgawe mtoto. Kuna watu wabaya sana duniani wanaweza wakamchukua wakamtoa kafara. Mungu atakunfungulia milango tu endelea kupambana.
 
Nigawe mtoto hiyo hapana niliwahi kukaa na mtoto wadalasa lapili mchana namwachia.hela kwa mama lishe jioni napika mwenyewe hatujui nn kilitokea lakini wababa tupunguze ubabe haya makitu yanakera ila yanamsaada sana
 
Kwanza wewe mwanaume ni mpumbavu mkubwa mwanao unamuacha kwenye barabara .. useme tuu humtaki mwanao
 
Nimesoma nimeumia sana, Nina watoto wadogo mapacha wa umri huo, nimewawazia jinsi wanavyonipokea nikirudi toka mihangaikoni nikamsikitikia huyo binti yako, na inaonekana mnamchukulia Kama ni mzigo kwenu kwahiyo hata tukikushauri ubaki nae bado atakosa upendo wa wazazi
nichek 0769922210 nimchukue

NOTE: tutakamilisha taratibu zote za kiserikali ili nimuasili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…