Msaada wa chakula toka USA ni kuichafua Tanzania

Marekani iliwahi kulisha chakula shule zote za Tanzania, hawakuishia hapo tu, wakatulisha yanga watanzania wote.
 
Ndio ukiongozwa na mtu mwenye utumwa wa kifikra ndo madhara yake haya
 
Je, unadhani USA iliota? Au kuna watu walienda kulialia njaa,wakidhani watapewa pesa! Msemo wa mtu hapa wanunulie ma Bus na vitu vingine! Hao hao mngewaachia stoo zao wapeleke majumbani kwao.
 
Mm nadhani tujikite kuipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya mama hodari Samia kufanikisha mlo.
2025 mama apite bila uchaguzi
Vijana wa siku hizi hawawezi kujua. Miaka ya nyuma hii misaada kutoka Marekani ilikuwepo sana mashuleni. Kulikuwa na shayiri, unga wa njano na mafuta ya karanga. Yote yalikuwa yamechorwa hiyo lebo ya watu wanapeana mkono. Hili siyo jambo jipya.
 
Marekani iliwahi kulisha chakula shule zote za Tanzania, hawakuishia hapo tu, wakatulisha yanga watanzania wote.
Ewaa. Wewe unajua. Nakumbuka dada na kaka zangu kula hivyo vyakula. Kuna mjomba wangu alikuwa ni mpishi wa shule na walikuwa wanagaiwa hiyo misaada. Nakumbuka kulikuwa na galoni za mafuta ya karanga, vigunia vya unga wa njano na shayiri (nafaka kama mchele lakini ina rangi ya brown)
 
Vijana wa siku hizi hawawezi kujua. Miaka ya nyuma hii misaada kutoka Marekani ilikuwepo sana mashuleni. Kulikuwa na shayiri, unga wa njano na mafuta ya karanga. Yote yalikuwa yamechorwa hiyo lebo ya watu wanapeana mkono. Hili siyo jambo jipya.
Si vyema lakini watu kuzoezwa kupewa tu bule
 
Virutubisho vyenye chembechembe za upinde hatutaki!
Uyu Bibi bila kufanya utaratibu wa kumuondoa kwenye kiti Kuna siku tutajuta!
 
Hivi,hiyo marekani watu wake wote wanajitosheleza,kiasi cha kulima au kununua vyakula,na kusafilisha bule kuja Afrika? Wema gani? Huruma gani!
Dunia hii,marekani tu ndo inazalisha chakula kingi na kusaza kwa ajili ya wa Afrika?
Russia na Ukraine mbona ngano zao hawatoi bure?
Mbona hawawapelekei wakimbizi na nchi zenye shida ya chakula!!
 
Moja; Beggars are not Choosers
Mbili: Duniani hakuna cha Bure hata ukikipata kuna mtu anakilipia....; Hivyo katika mchakato mzima kuna watu wanapiga pesa either NGO fulani huko USA ambapo hii ni kuonyesha kwamba tumefanya hiki au kile
Tatu: Huenda huko kuna surplus hivyo kuliko kuoza ni bora leo wawape misaada ili kesho na wao wakija kuomba / au kuwaambia hiki au kile mikatae (leo nikikupa Chumvi kesho ni vigumu kuninyima sukari au Milo)
Nne: Unasema kuichafua ni bora watu wachafuke wakiwa matumbo yameshiba au wafe njaa wakiwa wasafi (Kwahio lawama zako ziwafikie Serikali na si vinginevyo)
Tano: Siku hizi Miradi ndio MIRADI, hivyo hapo kuna wanaofaidika USA pesa ikiwepo inakatwa Kodi ila ukiipeleka kwenye Charity zako inaweza ikawa deducted kwenye Kodi - Hivyo ni Bora utoe ufadhiri sehemu na kupata good publicity...
Mwisho: Swali zuri ni kweli tuna njaa au hatuna njaa kujifanya tuna shibe wakati watu tuna njaa pia itakuwa uzezeta (Kwahio tupunguze Uchawa na kuishurutisha Serikali ifanye kazi yake)
 
Na kile kinachopelekwa Gaza? Wazungu siyo wachawi km nyie
 
Thats a fact!

Na kuongeza matusi kwenye kidonda, taarifa ya Marekani imesema ni "mchele ulioongezwa virutubisho."

Translation: Genetically Modified Foods

Wamarekani wanajua Samia Suluhu is a lightweight, hana uwezo wa kuchambua pumba na mchele, hana balls and wherewithal za kumhoji Mzungu. Na hakuna kichwa hata kimoja serikalini kitahoji ni lini, toka lini, tumeruhusu mazao yaliyobadilishwa vinasaba ????
 
Lengo kuu la msaada ni kukufanya uwe mzembe na usiweze kujitegemea ili siku moja uje kutawaliwa kwa kuwa hutoweza kujitetea mbele ya mtu anayekulishia familia yako na ukimbishia au kumgomea anachotaka anakunyima chakula sasa hapo lazima upate pressure kutoka kwa famila yako maana wanao pia watakuwa wamelemaa hawajui namna ya kutafuta chakula.
 
Hizo chanjo zimesha anza kufanya kazi.. matatizo kibao.. hormon balance ni issue siku hizi, watoto wa kiume kurembua kama mwanawamali wa pemba sio poa
Labda mtoto wako tu,Mimi watoto wangu wote wamepata chanjo zote zinazotakiwa na wana afya njema sana serikali haiwezi kuruhusu viletwe vitu vinavyoweza kudhuru wananchi wake iwe madawa,chakula nk.na ndio maana Kuna idara au taasisi zinazo shughulika na ukaguzi wa hivyo vitu na hiyo ndio kazi ya serikali yetu pendwa .
 
Njaa Mbaya Sana Viongozi Wamelala Fo~Fo~Fo
Mabeberu Hayatupendi Ndugu Zangu Hata Barakoa Shoneni Za Kwenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…