Msaada wa haraka kuhusu tatizo la nyufa ukuta wa nyumba

Asante kwa ushauri nitaufanyia kazi
Itasaidia,fanya hvyo
Uko katavi sehem gan?,
Niko Nsemulwa
 
Hii ndio hasara ya Ujenzi wa JF wa kuulizana nina milioni 5 naweza kujenga nyumba ya vyumba vitatu? Na watu wanashabikia inawezekana.
Akina Mshana Jr wakamjibu tena hiyo ni kubwa.
Hata ukiwa 3.5m uchanganye na chumvi ghorofa tayari🤣🤣🤣🤣
 
Duh!Sasa nini kifanyike?Mbona nimechanganyikiwa
Unataka kuirekebishia nyumba jf kama ulivyoijengea jf?
Tafuta mtaalam huko huko.
Kwa ujenzi huo huwwzi kumudu mjenzi makini tafuta hukohuko
 
Vitu inavyoelekeza havijui mkuu hiyo ni nyumba ya matofali ya udongo halafu karashia lipu ya chokaa
 
Yaani unajua kabisa huko kuna matetemeko halafu unajenga "kimasikini" bila hata "lenta".

Vipi na majengo ya serikali yana nyufa huko hasa ya 2005 kurudi nyuma? Siyo haya majengo ya wananchi kujitolea.

Huko inahitajita lenta za kusuka nondo nne (12mm) kwenye msingi na juu ya madirisha siyo kulaza nondo moja tu tena 8mm.
 
Nitaufanyia kazi huu ushauri!
 
Hapo n pakuhama kabisa uza hiyo nyumba ukajipange upya

Sent using Jamii Forums mobile app
Nashukuru kwa ushauri!Hiyo ni nyumba ya uani pamoja na kwamba Ina vyumba vinne vya kulala!Inamaana hakuna marekebisho yoyote yanayoweza kufanyika hata Kama ni makubwa?Kwa mfano nikianza kufumua kuta za juu na kumwaga lenta haitasaidia?Pia nikifumua huku chini kwenye msingi na kumwaga lenta ya chini hakusaidii?
 
Samahani,
1.Prince beam ndiyo nini?
2.Chicken wire kwenye jengo ambalo tayari kuna settlement tofauti ,itasaidiaje...?
 
H
Hebu kuwa serious,,gharama ya kufanya vipimo vya udongo unadhani kila mwananchi anaweza kumudu, hapo unaongelea kuita Mwana Jiolojia na si Mhandisi....

Hii ilikuwa kazi ya Mpango mji ,walitakiwa wafanye survey ya meneo yote...
na kuweka mapendekezo ya namna bora ya kujenga jengo kwa maeneo husika.

Halafu data zipatikane Manispaa
 
Tatizo lipo kwenye Msingi ,so markebisho yanaanzia kwenye Msingi, ambapo ni ngumu na Gharama sana.

Next time,uende Mipango mji wa Mji wako, Kule wana data za maeneo yote na kuna wataalam husika, wata kushauri ni aina ipi ya Ujenzi uufanye.

Usiogope gharama,kwani ni sehemu ya majukumu yao, fika ofisi zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…