Msaada wa haraka: Mke wangu tumegombana usiku, asubuhi hii anatafuta utaratibu wa talaka tugawane mali

Mi mtu akitaka kuachana na mimi simzuii, huwa nawapa utaratibu wa talaka afu nakaa kuisubiria.
Hebu zingatia hii sentence!
Wakuu Naomba mnipe mbinu maana tukigawana ndio mwisho wa kuona humu jf maisha yangu yatakua magumu sana,
 
Brother wewe cha kufanya hapo,Mpe nauli aende akaeleze shida zake . Hapo sioni kama kuna kosa ulilolifanya we jiamini tu vizuri na Ikitokea mkaachana usiogope kuanza upya . We ni Mwanaume Usiogope Kabisa yani . Pia mtegemee Mungu.
 
Wenzako ukisha mtandika makofi kama hivyo kukikaribia kukucha unaanza kumbembeleza ili yaishe,sio tena unaongezea ubabe...
 
Kaa kimya ikiwezekana ondoka nyumbani kwako haraka hata kwa siku tatu na simu uzime na usimuage.
 
Hebu zingatia hii sentence!
Wakuu Naomba mnipe mbinu maana tukigawana ndio mwisho wa kuona humu jf maisha yangu yatakua magumu sana,
Mbinu, ni kama ile waliyoitumia timu ya Yanga, waliyoitumia kumzuia Fei asiwaache!
------
Tunaambia… .WANAWAKE WAWAPENDE WAUME ZAO. Lakini sisi WANAUME tunaambiwa, TUISHI NAO KWA AKILI! Kuishi kwa AKILI, ni pamoja na KUDHARAU mambo, au matendo yao mengine ya KIJINGA JINGA kama hili la 50,000/=!
 
Yaani 50,000/= tu ndio inakutoa wenge na kuwa mkuda hivyo kwa my wife wako?[emoji3061]
 
Wenzako ukisha mtandika makofi kama hivyo kukikaribia kukucha unaanza kumbembeleza ili yaishe,sio tena unaongezea ubabe...
Yaani kama mimi tu. Mie huwa hata sisubiri kukuche. Ni baada ya muda mchache tu naanza kumuomba gemu kama vile hakuna kilichotokea, na lazima agome kutoa gemu, hapo sasa ndio naanza kubembeleza yaishe na tusameheane. Mpaka kufikia asubuhi kila kitu kipo poa.
 

Mke wako ana matatizo, wewe ujielewi, mali inagawanywaje overnight? Msikilize, mpuuze, au ondoka rudi weekend, mambo yatakuwa yametulia.
 
😂😂😂inaonyesha huna kitu ulikuwa unamtegemea manz,sasa kama ulijua ulikuwa unamtegemea mkeo ulikuwa unampiga ili iweje? But pole,ndoa ndivyo zilivyo mkuu
 
Inaonekana unamtegemea mke wako kwa kila kitu na hilo duka sio lako ni lake kulingana na hiki ulichosema na quote
" Wakuu Naomba mnipe mbinu maana tukigawana ndio mwisho wa kuona humu jf maisha yangu yatakua magumu sana"
😂see
 
Je watoto akitaka kuondoka nao nimuache aende nao?

Kama yeye anajikuta mwamba mpe aondoke nae ila kama tu unajua watoto watakua mikono salama na mwanamke anajua kulea na anapenda watoto hilo ni angalizo kama watoto watakua mikono salama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…