Mambo ya kujiropokesha😀😀pole dyadya...ni hivi waambie mnaniachiaje nipike peke yangu tunapika wote hapa maana hii ni sherehe visipoiva lawama zote kwangu, kwanza kwenye watu wengi Huwa tunapika Kwa ushirika Kila mtu anashika mwiko msinitanie....😀😀😜Guys, msaada wa haraka nipo njia panda, ishu iko hivi nimealikwa na jirani yangu mtoto wake amepata ubatizo sijui kumunio hata sielewi, nikasema ngoja nijichanganye na majirani zangu hawa ndio kimbilio langu la kwanza,
Sasa kama kawaida wanawake tumefika mapema kama kuna vikazi vidogo vidogo vifanywe, baada ya muda mama shughuli kaja uso umemsawajika anasema mpishi alompanga aje apike hapatikani kwenye simu, itakuaje na muda unasogea, basi watu wanajifanya kusikitika hapo,
Mie na kiherehere changu nisiropoke, "jamani kwani pilau tu na rosti tunashindwa kupika chapu hapo watoto wakafurahi hadi tumsubiri mtu tusojua anatokea wapi"
Khe si ndio huyo mama wa kichaga akasimama "halafu kweli tena leo tupikiwe pilau na mpemba, nyie kwa mapishi hamna mpinzani"
Alooo nilisonya kimoyo moyo nikajisemea "mie sio mpemba mpuuzi wewe, alokwambia najua kupika nani nyau weee"
Lakini nje nilionesha tabasamu la unafki wakati nishatoka kumnanga,
Basi kabla hata sijajitetea wamama wasininyanyue wakaanza kunionesha mafiga ya kuni, mwengine kaosha mchele, mwengine kachochea kuni sasa hivi wooooote wamekaa pembeni wanasubiri kupikiwa pilau la kipemba,🙌🏻
Nimewaambia napokea simu mara moja ndio nimekaa kwenye kituta cha viazi naandika huu uzi haraka haraka, sasa kosa langu mie nini hadi kuachiwa kupika jungu la pilau kwenye jiko la kuni,
Nisiwe muongo sijawahi kupika kwenye kuni, sijawahi kupika wali zaidi ya kilo 3 leo napewa mchele wa kilo 20 kweliiiiii, serikali iko wapi wananchi wake wananyanyasika,🥺
Nishaurini guys niache ndala a.k.a kutoka ndukii au nijifanye naumwa jino ghafla? au nijiangushe nijifanye jini makata kapanda anataka 'kiti wake' apewe pepsi baridi na apumzike kivulini?
Nyie jamani huu ni ukatili na unyongeshaji,
Heeeeeeeeeeeeeeelp😭😭😭😭😭
Halafu kilipoiva ulikula 😜Nikiwa ugenini suala la kupika huwa najikausha.
Nilienda ukweni, mama mkwe yupo jikoni nilimute kama sio mimi.
Mama mkwe kwanza age go ila nilitulia tuli kwenye kiti kilipoiva nikala na baadae njaa ikaniuma tena nikala.Halafu kilipoiva ulikula 😜
Chumvi tena, ya nini?pika tu ila hakikisha unamwagia chumvi kwenye moto kabla uanze kupika
Sanaaa hujaona pale juu yule mama nimemnanga kimoyo moyo😆Alaaaa kwahiyo waliokuita mpemba wamekoroga mambo🙄🙄
🙌😅Mama mkwe kwanza age go ila nilitulia tuli kwenye kiti kilipoiva nikala na baadae njaa ikaniuma tena nikala.
We pika tu atakaeona sio kizuri apike yeye 😆Sanaaa hujaona pale juu yule mama nimemnanga kimoyo moyo😆
pika tu ila hakikisha unamwagia chumvi kwenye moto kabla uanze kupika
Macho ya watu....🙃Eh chumvi yasaidia nini?
Nakukodia Chopa Tanga to Kigamboni chapNitakuja na usafiri gani wa chap jamani.
Kama ni Tanga chap naja.
Umenipa nguvu ABJ, ngoja nikawatunishie kifua na mie, tupike wote peke yangu hiyo vipiiiiii!? lolMambo ya kujiropokesha😀😀pole dyadya...ni hivi waambie mnaniachiaje nipike peke yangu tunapika wote hapa maana hii ni sherehe visipoiva lawama zote kwangu, kwanza kwenye watu wengi Huwa tunapika Kwa ushirika Kila mtu anashika mwiko msinitanie....😀😀😜
Muda wote huu bado hujarudi? Kama chakula si kishaunguaUmenipa nguvu ABJ, ngoja nikawatunishie kifua na mie, tupike wote peke yangu hiyo vipiiiiii!? lol
Umenishinda tabia Ephen au ulikua mjamzito???🙌🏻😆Nikiwa ugenini suala la kupika huwa najikausha.
Nilienda ukweni, mama mkwe yupo jikoni nilimute kama sio mimi.
Nitakupikia la nyumban nikuagizie,Likiiva usiache kuniagizia please.
Nina hamu nalo balaa.
Yani hapa mate yananitoka.
Sikua mjamzito! Mqshemeji watatu na watoto wao kama 7 hivi mpishi niwe mimi nikitoa boko je?Umenishinda tabia Ephen au ulikua mjamzito???🙌🏻😆
Hakijapikwa bado, si wananisubiri mpishiMuda wote huu bado hujarudi? Kama chakula si kishaungua