Msaada wa haraka unahitajika ili ndugu yangu apate haki yake

Msaada wa haraka unahitajika ili ndugu yangu apate haki yake

Ndugu yangu halazimishi kuendelea kuishi pale anachotaka ni alipwe kiasi cha pesa ili ahame shambani maana miaka yote alikuwa akifanya kazi ya kulitunza shamba la baba yao bila malipo yeyote.
Sasa watoto wa marehemu wanataka kutumia nguvu ya pesa na elimu zao kumuaondoa kwa nguvu bila kumpa chochote.
Hana ushahidi wowote wa maandishi toka kwa marehemu ila majirani wa shambani wanamjua kubwa yeye ndio mtunza shamba kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Kama alikuwa anaishi kweye hilo shamba malipo yake ni kukaa hapo bure
 
Unasemaje apate haki yake, haki Gani? Hebu tokeni kwenye shamba la watu, sawa?

Ushakaa Bure miaka 10 unataka Nini Tena? Shida mnajisahau sana nyie, mkadhani lishakuwa lenu. Eti kapanda mazao ya kudumu, Sasa si alikuwa anakula mwenyewe hayo machungwa?

Acheni ujinga, tokeni Kwa wenyewe
 
Wewe na ndugu yako wote matapeli.
Sasa unakaa shambani kwangu bure?
Unataka hapo nani akufanyie usafi?
Umesitirika wewe na mke na watoto kwa miaka yote 10.
Unataka ulipwe nini na hakukuwa na makubaliano?
Kama unabusara kamtoa ndugu yako akae kwako.
Waache watoto wa marehemu na shamba lao.
Tunajua kuwa kuna sehemu watu wanakaa mashambani na kila mwezi wanalipwa lakini hayo hayakuwa makubaliano kati ya marehemu na ndugu yako.
Na usikute yeye ndo alisitirika na familia yake maana pa kukaa walikuwa hawana, kajiliza kwa marehemu wee marehemu kamuonea huruma, kampa eneo asitirike na familia.
Watu dizaini ya ndugu yako na wewe ndo nyie mnaowaua wenye mashamba au nyumba ili mzitaifishe.
Au mnawaroga wasahau maeneo yao.
Eti ndugu yako apate haki yake.
Haki ya nyoko [emoji57][emoji57][emoji57]
Bora umemwambia ukweli aachie shamba la watoto wa Marehemu
 
MAHAKANI NI UWE NA VIELELEZO, USHAHIDI
KINYUME NA HAPO UNAONEKANA MVAMIZI.
USHAHIDI PEKEE NI MAREHEMU AITWE, AULIZWE! AKISHINDWA HILI, ASICHINDWE KUBEBA VILIVYO VYAKE NA KWENDA KUANZA PENGINE.
MPAKA WATOTO KUJA KUVUNJA NA KUMTOA KWA NGUVU, NI ISHARA YA KUSHINDWA KWA MAZUNGUMZO.
USISHAU KWENYE ARDHI KUNA USHIRIKINA SANA WA KUWAPUMBAZA WATU WASAHAU MAENEO YAO.
 
Asante kwa kuandika.
Ndugu yangu alikuwa ana litunza shamba lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 5 kwa makubaliano ya malipo sio kwamba alikosa eneo la kuishi.
Na kama unasema suala la kufanya usafi wewe kwa akili yako ekari 5 ni eneo la mtu akufanyie usafi bure kwa zaidi ya miaka 10? (Kukata miti,kufyeka na kupanda mazao ya kudumu vyote vifanyike bure kwa kuwa tu ndugu yangu alikuwa anaishi hapo??)
Hayo mambo ya kuroga mwenye shamba ni imani na mawazo yako tu hakuna ukweli hata kidogo.
Mm nimeleta hapa ili kupata msaada hata wa mawazo sio kubishana na mtu.
Mkuu Huyo ndugu yako aliwezaje kupanda mazao ya kudumu kwenye shamba ambalo syo lako bila maandishi au Shahid ili Hali unajua mtu anafamilia
 
Ndugu yangu halazimishi kuendelea kuishi pale anachotaka ni alipwe kiasi cha pesa ili ahame shambani maana miaka yote alikuwa akifanya kazi ya kulitunza shamba la baba yao bila malipo yeyote.
Sasa watoto wa marehemu wanataka kutumia nguvu ya pesa na elimu zao kumuaondoa kwa nguvu bila kumpa chochote.
Hana ushahidi wowote wa maandishi toka kwa marehemu ila majirani wa shambani wanamjua kubwa yeye ndio mtunza shamba kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Hao majirani ndio ushahidi mzuri zaidi.

Kazeni buti mtashinda mkiona kunaviashiria vya rushwa waoneni takukuru andikeni barua mkieleza suala zima na jinsi mnaona haki yenu inapindishwa kwa nguvu inayoonekana ni ya kiburi cha rushwa, hao madogo hawana utu wala uungwana kabisa.
 
Hao majirani ndio ushahidi mzuri zaidi.
KAZENI BUTI MTASHINDA MKIONA KUNAVIASHIRIA VYA RUSHWA WAONENI TAKUKURU ANDIKENI BARUA MKIELEZA SUALA ZIMA NA JINSI MNAONA HAKI YENU INAPINDISHWA KWA NGUVU INAYOONEKANA NI YA KIBURI CHA RUSHWA, HAO MADOGO HAWANA UTU WALA UUNGWANA KABISA.
Huyo ndugu yenu ni trespasser.
Atakuwa kaandikiwa notice ya kuondoka akakataa, bila kuhusisha vyombo vya sheria.
Huo tu, kwanza ni mwanzo mbaya.
 
Huyo ndugu yenu ni trespasser.
Atakuwa kaandikiwa notice ya kuondoka akakataa, bila kuhusisha vyombo vya sheria.
Huo tu, kwanza ni mwanzo mbaya.
Kama alijulishwa na kupewa notsi na akaikubali bila kuweka dai lake itakuwa shida kidogo!
 
kwa hyo ndugu yako akajenga na kujenga?na mazao akapanda[emoji16][emoji16][emoji16]
Akajua wenyewe hawatokuja?
Mwambie ndugu yako awaombe namna nzuri ya KUMTOA.
Hana chake hapo.
inanikumbusha Kuna watu uwa wanaenda kwa waganga kuwapiga kiatu mabosi zao.yaani bosi anasahau Kama Ana shamba au kiwanja
 
Kaka msaada wa mawazo.
Wafuate hao watoto muwaombe wawape japo kaheka kamoja.
Tena tafuteni na watu wakubwa muende au muwaombe wawalipe fidia . vinginevyo mkienda mahakamani mtashindwa tu.
Hilo eneo sio LENU
Asante kwa kuandika.
Ndugu yangu alikuwa ana litunza shamba lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 5 kwa makubaliano ya malipo sio kwamba alikosa eneo la kuishi.
Na kama unasema suala la kufanya usafi wewe kwa akili yako ekari 5 ni eneo la mtu akufanyie usafi bure kwa zaidi ya miaka 10? (Kukata miti,kufyeka na kupanda mazao ya kudumu vyote vifanyike bure kwa kuwa tu ndugu yangu alikuwa anaishi hapo??)
Hayo mambo ya kuroga mwenye shamba ni imani na mawazo yako tu hakuna ukweli hata kidogo.
Mm nimeleta hapa ili kupata msaada hata wa mawazo sio kubishana na mtu.
 
Mambo ya ardhi sio ya kuyaletea masikhara, kipindi mzee yupo hai kama hakuacha maandishi popote huyo ndugu yako akubaliane na hali halisi hapo sio kwake aachie eneo au itokee tu hao watoto kumuhurumia wamgawie chochote vinginevyo aache kabisa.
 
Hapo wakae chini tu wayamalize wampe kiasi kidogo akaanze maisha mapya.
 
Habari zenu?

Kuna ndugu yangu alikuwa analinda shamba la mtu kwa muda wa zaidi ya miaka 10(bila malipo) mwenye samba ameshafariki.

Watoto wa mwenye shamba wanataka kumtoa kwa nguvu huyo ndugu yangu ambaye alikuwa anaishi hapo kwa miaka yote huku akiwa na familia yake hali kadhalika alipanda mazao ya kudumu kama michungwa,minazi nk kwa idhini ya mwenye shamba amabaye ameshafariki.

Watoto walitaka kumuondoa kwa nguvu mara kadhaa na kumuweka ndani/polisi bila mafanikio.

Jana walimkamata ndugu yangu na kumuweka kituo kikuu cha polisi(alipata dhamana jana usiku)

Leo hao watoto wa mwenye shamba wameleta vijana toka mtaani na kuja kuvunja vyumba na vibanda vote vya ndugu yangu hapo shambani huku mke na watoto vitu vikiwa nje hadi muda huu ambao giza linaingia.
Sasa mume yupo polisi mke na watoto wapo nje bila sehemu ya kulala.

Wenye mamlaka tunaomba msaada wa kupata haki ya ndugu yetu aliyopo mahabusu hadi muda huu.

Kwa mtu anayehitaji maelezo zaidi naomba aje PM nimpe namba.

Asanteni.
ushahidi muhimu kwanza wa idhin ya marehem je n kwel alimuweka... km ushaidi hakun hapo inaesabika km alivamia tu eneo
 
Ndugu yangu halazimishi kuendelea kuishi pale anachotaka ni alipwe kiasi cha pesa ili ahame shambani maana miaka yote alikuwa akifanya kazi ya kulitunza shamba la baba yao bila malipo yeyote.
Sasa watoto wa marehemu wanataka kutumia nguvu ya pesa na elimu zao kumuaondoa kwa nguvu bila kumpa chochote.
Hana ushahidi wowote wa maandishi toka kwa marehemu ila majirani wa shambani wanamjua kubwa yeye ndio mtunza shamba kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Kwanza kwanini afanye kazi bila malipo aliwezaje kumudu gharama za maisha wakati wote huo? Hii huwa hivi mara nyingi anakuja mtu anaomba akae shambani huku akilima na kujilisha huo ndo ujira wake wakati kazi yake inakua ni kuangalia shamba na hapo kiungwana mwenye shamba anakua anampa vi tip ambavyo si haki maana makubaliano ni wewe ishi hapa fanya mambo yako niangalizie shamba na wakati wowote nikihitaji kupaendeleza basi utaondoka uyu ndugu yako kuona mwenyewe kafa anataka kujihesabia haki na kujifanya analijua sana shamba mwamba sio sawa wenyewe hawamtakki aende tu heri nusu shari hapo kwenye akili yake anajiona anastaafu anastahili kiinua mgogo au anataka akatiwe shamba hii case ilitutokea nazifahamu sana
 
Kwa nilivyoelewa mim wale watoto wa marehem waitakiwa wawe waungwana hata kwa kumpa eneo dogo la kujihidhi au wakamnunulia sehem nyingine akaishi na familia yake,ni kumpa kama shukran kwa kuwatunzia hilo shamba maana wengine wangelikuta lishauzwa na kasepa
Tatizo letu watz huwa hatujui kuappriciate na kutoa shukrn sijui tupoje yaan roho mbaya tu
 
kwa hyo ndugu yako akajenga na kujenga?na mazao akapanda[emoji16][emoji16][emoji16]
Akajua wenyewe hawatokuja?.
Mwambie ndugu yako awaombe namna nzuri ya KUMTOA.
Hana chake hapo.
inanikumbusha Kuna watu uwa wanaenda kwa waganga kuwapiga kiatu mabosi zao.yaani bosi anasahau Kama Ana shamba au kiwanja

Na mara nyingi hawa watu wa kulinda linda huwa wanadhulum sana maeneo wenye nayo wakifariki
Sisi kuna watu walikaa kwenye nyumba yetu siku ya kuja kuwaondoa ilikuwa balaa hawataki kuondoka [emoji3][emoji23][emoji23][emoji23] na walipewa tu wajihifadhi
 
Back
Top Bottom