Msaada wa haraka unahitajika ili ndugu yangu apate haki yake

Msaada wa haraka unahitajika ili ndugu yangu apate haki yake

Ndugu yangu halazimishi kuendelea kuishi pale anachotaka ni alipwe kiasi cha pesa ili ahame shambani maana miaka yote alikuwa akifanya kazi ya kulitunza shamba la baba yao bila malipo yeyote.
Sasa watoto wa marehemu wanataka kutumia nguvu ya pesa na elimu zao kumuaondoa kwa nguvu bila kumpa chochote.
Hana ushahidi wowote wa maandishi toka kwa marehemu ila majirani wa shambani wanamjua kubwa yeye ndio mtunza shamba kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Nauliza tu je? Malipo hayawezi kuwa hiyo miaka aliyoishi hapo?
 
Kwa nilivyoelewa mim wale watoto wa marehem waitakiwa wawe waungwana hata kwa kumpa eneo dogo la kujihidhi au wakamnunulia sehem nyingine akaishi na familia yake,ni kumpa kama shukran kwa kuwatunzia hilo shamba maana wengine wangelikuta lishauzwa na kasepa
Tatizo letu watz huwa hatujui kuappriciate na kutoa shukrn sijui tupoje yaan roho mbaya tu
Tatizo lipo kwa wazazi waki Afrika Kuto andika wosia na tabia ya kufanya mambo bila kushirikisha watoto, wazazi wengi wanafanya mambo kinyemela, watoto wangekuwa wanajua tokea wapo dogo wala wasinge mfukuza.
 
Asante kwa kuandika.
Ndugu yangu alikuwa ana litunza shamba lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 5 kwa makubaliano ya malipo sio kwamba alikosa eneo la kuishi.
Na kama unasema suala la kufanya usafi wewe kwa akili yako ekari 5 ni eneo la mtu akufanyie usafi bure kwa zaidi ya miaka 10? (Kukata miti,kufyeka na kupanda mazao ya kudumu vyote vifanyike bure kwa kuwa tu ndugu yangu alikuwa anaishi hapo??)
Hayo mambo ya kuroga mwenye shamba ni imani na mawazo yako tu hakuna ukweli hata kidogo.
Mm nimeleta hapa ili kupata msaada hata wa mawazo sio kubishana na mtu.
Alikua analipwa kiasi gani? Je aliekua mmiliki wa sehemu alimtuma apande mazao ya kudumu? Watu wanaosaidiwa kwenye maswala ya ardhi na nyumba kwa muda mrefu hua wanajisahau na kuhisi wameshamiliki hio sehemu na wakitaka kuhamishwa hua ni ngumu sana..mimi nadhani amewatajia hao watoto wa marehemu kiasi kikubwa cha fedha...
 
Na yeye kwa nini akae kwa mtu miaka 10?
Huyo atakuwa mlevi tu yani upewe shamba uliangalie na kuishi miaka 10 na kashindwa kununua shamba kupitia shamba alilopewa kuishi na kulima bure bila kulipishwa pesa.
 
Samahani ndugu mtoa mada lakini nduguyo kuna maelezo ameyaficha kukueleza ili umuone mwenye haki....lakini kimsingi hakuna mtu anayeweza kukaa miaka kumi ya kufanya kazi bila malipo hali ya kuwa walikubaliana.......ni kwamba huyo nduguyo alikuwa ananufaika na eneo Hilo na ndio maana akasahau kudai mshahara wake......uwekezaji alioufanya na manufaa anayopata ndio vinamfanya aone uzito kuhama eneo Hilo.....
 
No inategemea huyo mzee mlinzi aliwaingia vipi hao watoto aa marehemu.
Angeenda kwa gia ya kuwaomba pengine wangemsaidia ila yeye ameenda kwa gia ya kibabe kwa kusema shamba ni mali yake
itakuwa huyo mlinzi alivyo sikia mzee amefariki yeye alikaa kimya hakutaka kwenda kujitambulisha kwa watoto itakuwa watoto walikuwa masomoni nje na walikuwa hawamjui huyo mlinzi na watoto walikuwa hawajai kufika huko shambani na walisikia kwa kuambiwa kuna shamba lenu lipo sehemu fulani na kufatilia wakuta kuna mtu na huyo mtu alikaa kimya tokea mzee wao afariki na siku nyingi zimepita.
 
unajua sisi wabongo tunapenda sana mserereko. kiufupi ndugu yako alishajua kapata eneo ndio maana alibweteka na kuendelea kulinda eneo bila malipo na bila makibaliano yoyote ya msingi.

Namsikitikia kwakua kapoteza 10 good years kisa kuamini ameokota dodo chini ya mkorosho hapo akafanye mipango mingine wenye mali ndo washazinduka sasa.

Nipende kuwapa ushauri ndugu zangu ukiona mali sio yako ww jitahidi utafute chako imagine leo mtu anaenda anza upya ajenge nyumba au apange na maisha yalivyopanda mbona namba zote zitasomeka.
 
Hapo hana haki kisheria, kwasababu hati ya shamba haisomi jina lake pia hana mkataba wa kimaandishi au sauti kutoka kwa marehemu unao onesha kunamakubaliano waliyoyaingia juu ya malipo yake.

Na ikizidi sana ndugu wa marehemu wanauwezo wa kumfunguliwa kesi ya kujimilikisha mali ya watu au utapeli, chamsingi achape mwendo tu
 
Utakuta mtu anapewa nyumba au shamba alinde na kuishi hapo hapo utakuta anaishi miaka mingi anao na kuzaa watoto wanafika mpaka Secondary siku akiambiwa atoke anakuwa mgumu kweli, ushauri tusiweke waangalizi kwenye viwanja, mashamba, Nyumba kwa miaka mingi huwa wana jisahau wanaona kama wamiliki.
Kweli kabisa, na huyu hata mwisho nilituma watu nikaona video anavyoongea kama kwake pale
 
Hapo ni busara kutumika ,inaonekana ndugu yako aliwaletea jeuri watoto wa marehemu...haiwezekani watoto wampeleke polisi na polisi wakamfunga ,hapo kutakuwa na kutishia watoto wa marehemu ,watu wa masaiti nawajua jinsi walivyo.

Hii imewahi nikuta, nilijenga mahali nikaweka mlinzi akawa anaishi na familia yake imefika wakati nataka kuhamia(ingawa hanidai) anagoma kua aende wapi nimpe hela ya kuanzia maisha (sio kwa ombi ila kwa kunilazimisha).

Kwa usalama wake yeye ahame abaki na deni la msingi kua anadai malipo yake (kama haina maandishi ni tatizo) ila
Kugoma kutoka kwenye shamba ambalo hana umiliki nalo na ni mtumishi tu itamgharimu yeye!
 
Hapo ni busara kutumika ,inaonekana ndugu yako aliwaletea jeuri watoto wa marehemu...haiwezekani watoto wampeleke polisi na polisi wakamfunga ,hapo kutakuwa na kutishia watoto wa marehemu ,watu wa masaiti nawajua jinsi walivyo.
Wanajisahau sana.. wakikaa miaka mitatu mtu anaona ni haki yake. Kwa hvyo kama una site bora ujenge kachumba upangishe lakini sio kumweka mtu akae bure huku Kilinda shamba au site
 
Miaka yote alikuwa anakula nini kama alikuwa halipwi? Kama alikuwa ananufaika kupitia hilo eneo, ni sawa alikuwa anajilipa. Wamiliki wakisema, ndugu yako alitaka ajimilikishe eneo, utakataa? Muhimu hapo, aondoke na atumie tu lugha ya ustaarabu, familia itamsikiliza.​
 
Ndugu yangu halazimishi kuendelea kuishi pale anachotaka ni alipwe kiasi cha pesa ili ahame shambani maana miaka yote alikuwa akifanya kazi ya kulitunza shamba la baba yao bila malipo yeyote.
Sasa watoto wa marehemu wanataka kutumia nguvu ya pesa na elimu zao kumuaondoa kwa nguvu bila kumpa chochote.
Hana ushahidi wowote wa maandishi toka kwa marehemu ila majirani wa shambani wanamjua kubwa yeye ndio mtunza shamba kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Maelewano yalikuwa ya baba wa vijana na ndugu yako. Wao hawatakiwi kumfidia chochote ndugu. Ingawaje unasema alikuwa halipwi, lakini alikuwa analifaidi kwa kulilima na kupata mazao..huo ndiyo mshahara. Ila, kama kulikuwa na mapatano ya malipo na kuna ushahidi kuwa mhusika hakuwi kumlipa, basi awasilishe madai yake wakati wa mirathi kugawiwa na ana haki kupewa hata kabla ya wariyhi kupata. Kwa kawaida madeni ya marehemu hulipwa kwanza na warithi hugawana kilichobaki kufuatana na wosia au makubaliano ya mgaso.
 
Habari zenu?

Kuna ndugu yangu alikuwa analinda shamba la mtu kwa muda wa zaidi ya miaka 10(bila malipo) mwenye samba ameshafariki.

Watoto wa mwenye shamba wanataka kumtoa kwa nguvu huyo ndugu yangu ambaye alikuwa anaishi hapo kwa miaka yote huku akiwa na familia yake hali kadhalika alipanda mazao ya kudumu kama michungwa,minazi nk kwa idhini ya mwenye shamba amabaye ameshafariki.

Watoto walitaka kumuondoa kwa nguvu mara kadhaa na kumuweka ndani/polisi bila mafanikio.

Jana walimkamata ndugu yangu na kumuweka kituo kikuu cha polisi(alipata dhamana jana usiku)

Leo hao watoto wa mwenye shamba wameleta vijana toka mtaani na kuja kuvunja vyumba na vibanda vote vya ndugu yangu hapo shambani huku mke na watoto vitu vikiwa nje hadi muda huu ambao giza linaingia.
Sasa mume yupo polisi mke na watoto wapo nje bila sehemu ya kulala.

Wenye mamlaka tunaomba msaada wa kupata haki ya ndugu yetu aliyopo mahabusu hadi muda huu.

Kwa mtu anayehitaji maelezo zaidi naomba aje PM nimpe namba.

Asanteni.
Haki gani labda anayotaka nduguyo, kuendelea kubaki hapo? Au kulipwa?How comes 10 yrs hakudai malipo yoyote aje kudai baada ya mmiliki kufariki? Nikisoma kati ya mistari( btn lines) ni kama vile unataka kusema nduguyo ana haki na mahali hapo maana amepanda mazao ya kudumu hlf aameishi kwa miaka 10.
Mi naona ndugu yako aondoke au kama hataki basi sahihi aondoshwe kwa nguvu maana anang'ang'ania ardhi ya wenyewe.
 
Habari zenu?

Kuna ndugu yangu alikuwa analinda shamba la mtu kwa muda wa zaidi ya miaka 10(bila malipo) mwenye samba ameshafariki.

Watoto wa mwenye shamba wanataka kumtoa kwa nguvu huyo ndugu yangu ambaye alikuwa anaishi hapo kwa miaka yote huku akiwa na familia yake hali kadhalika alipanda mazao ya kudumu kama michungwa,minazi nk kwa idhini ya mwenye shamba amabaye ameshafariki.

Watoto walitaka kumuondoa kwa nguvu mara kadhaa na kumuweka ndani/polisi bila mafanikio.

Jana walimkamata ndugu yangu na kumuweka kituo kikuu cha polisi(alipata dhamana jana usiku)

Leo hao watoto wa mwenye shamba wameleta vijana toka mtaani na kuja kuvunja vyumba na vibanda vote vya ndugu yangu hapo shambani huku mke na watoto vitu vikiwa nje hadi muda huu ambao giza linaingia.
Sasa mume yupo polisi mke na watoto wapo nje bila sehemu ya kulala.

Wenye mamlaka tunaomba msaada wa kupata haki ya ndugu yetu aliyopo mahabusu hadi muda huu.

Kwa mtu anayehitaji maelezo zaidi naomba aje PM nimpe namba.

Asanteni.
Haki gani sasa...mali sio yake. Anapaswa aondoke ama ana mpango wa kuwadhurumu watoto wa mwenye shamba?
 
Back
Top Bottom