Msaada wa haraka unahitajika ili ndugu yangu apate haki yake

Kama alikuwa anaishi kweye hilo shamba malipo yake ni kukaa hapo bure
 
Unasemaje apate haki yake, haki Gani? Hebu tokeni kwenye shamba la watu, sawa?

Ushakaa Bure miaka 10 unataka Nini Tena? Shida mnajisahau sana nyie, mkadhani lishakuwa lenu. Eti kapanda mazao ya kudumu, Sasa si alikuwa anakula mwenyewe hayo machungwa?

Acheni ujinga, tokeni Kwa wenyewe
 
Bora umemwambia ukweli aachie shamba la watoto wa Marehemu
 
MAHAKANI NI UWE NA VIELELEZO, USHAHIDI
KINYUME NA HAPO UNAONEKANA MVAMIZI.
USHAHIDI PEKEE NI MAREHEMU AITWE, AULIZWE! AKISHINDWA HILI, ASICHINDWE KUBEBA VILIVYO VYAKE NA KWENDA KUANZA PENGINE.
MPAKA WATOTO KUJA KUVUNJA NA KUMTOA KWA NGUVU, NI ISHARA YA KUSHINDWA KWA MAZUNGUMZO.
USISHAU KWENYE ARDHI KUNA USHIRIKINA SANA WA KUWAPUMBAZA WATU WASAHAU MAENEO YAO.
 
Mkuu Huyo ndugu yako aliwezaje kupanda mazao ya kudumu kwenye shamba ambalo syo lako bila maandishi au Shahid ili Hali unajua mtu anafamilia
 
Hao majirani ndio ushahidi mzuri zaidi.

Kazeni buti mtashinda mkiona kunaviashiria vya rushwa waoneni takukuru andikeni barua mkieleza suala zima na jinsi mnaona haki yenu inapindishwa kwa nguvu inayoonekana ni ya kiburi cha rushwa, hao madogo hawana utu wala uungwana kabisa.
 
Huyo ndugu yenu ni trespasser.
Atakuwa kaandikiwa notice ya kuondoka akakataa, bila kuhusisha vyombo vya sheria.
Huo tu, kwanza ni mwanzo mbaya.
 
Huyo ndugu yenu ni trespasser.
Atakuwa kaandikiwa notice ya kuondoka akakataa, bila kuhusisha vyombo vya sheria.
Huo tu, kwanza ni mwanzo mbaya.
Kama alijulishwa na kupewa notsi na akaikubali bila kuweka dai lake itakuwa shida kidogo!
 
kwa hyo ndugu yako akajenga na kujenga?na mazao akapanda[emoji16][emoji16][emoji16]
Akajua wenyewe hawatokuja?
Mwambie ndugu yako awaombe namna nzuri ya KUMTOA.
Hana chake hapo.
inanikumbusha Kuna watu uwa wanaenda kwa waganga kuwapiga kiatu mabosi zao.yaani bosi anasahau Kama Ana shamba au kiwanja
 
Kaka msaada wa mawazo.
Wafuate hao watoto muwaombe wawape japo kaheka kamoja.
Tena tafuteni na watu wakubwa muende au muwaombe wawalipe fidia . vinginevyo mkienda mahakamani mtashindwa tu.
Hilo eneo sio LENU
 
Mambo ya ardhi sio ya kuyaletea masikhara, kipindi mzee yupo hai kama hakuacha maandishi popote huyo ndugu yako akubaliane na hali halisi hapo sio kwake aachie eneo au itokee tu hao watoto kumuhurumia wamgawie chochote vinginevyo aache kabisa.
 
Hapo wakae chini tu wayamalize wampe kiasi kidogo akaanze maisha mapya.
 
ushahidi muhimu kwanza wa idhin ya marehem je n kwel alimuweka... km ushaidi hakun hapo inaesabika km alivamia tu eneo
 
Kwanza kwanini afanye kazi bila malipo aliwezaje kumudu gharama za maisha wakati wote huo? Hii huwa hivi mara nyingi anakuja mtu anaomba akae shambani huku akilima na kujilisha huo ndo ujira wake wakati kazi yake inakua ni kuangalia shamba na hapo kiungwana mwenye shamba anakua anampa vi tip ambavyo si haki maana makubaliano ni wewe ishi hapa fanya mambo yako niangalizie shamba na wakati wowote nikihitaji kupaendeleza basi utaondoka uyu ndugu yako kuona mwenyewe kafa anataka kujihesabia haki na kujifanya analijua sana shamba mwamba sio sawa wenyewe hawamtakki aende tu heri nusu shari hapo kwenye akili yake anajiona anastaafu anastahili kiinua mgogo au anataka akatiwe shamba hii case ilitutokea nazifahamu sana
 
Kwa nilivyoelewa mim wale watoto wa marehem waitakiwa wawe waungwana hata kwa kumpa eneo dogo la kujihidhi au wakamnunulia sehem nyingine akaishi na familia yake,ni kumpa kama shukran kwa kuwatunzia hilo shamba maana wengine wangelikuta lishauzwa na kasepa
Tatizo letu watz huwa hatujui kuappriciate na kutoa shukrn sijui tupoje yaan roho mbaya tu
 

Na mara nyingi hawa watu wa kulinda linda huwa wanadhulum sana maeneo wenye nayo wakifariki
Sisi kuna watu walikaa kwenye nyumba yetu siku ya kuja kuwaondoa ilikuwa balaa hawataki kuondoka [emoji3][emoji23][emoji23][emoji23] na walipewa tu wajihifadhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…