Kama waislam mnampenda YESU na kumfuata mafundisho yake, [HASHTAG]#swali[/HASHTAG],
Ni muislam yupi duniani amewahi kumpokea na kumkiri YESU kuwa mwokozi wa maisha yake? Sasa mwampendaje au mwamfataje pasipo kumpokea, au unamaanisha kusoma mafundisho yake kama gazeti,?
YESU unampendaje pasipo kupenda anayoyaagiza uyatende? Kama ungelikuwa unafuata mafundisho yake haikuwepo haja ya kupost, OK mmshindwa kujua Kama ni mwana wa mungu, kwanni hamsomi habar za manabii waliotabiri ujio wa YESU, miaka million kabla yake.
YESU alibatizwa, YESU alishiriki meza ya bwana
YESU alimpokea roho matakatifu, mna sababu gani za kutotimiza hayo yote kama mnampenda, sisi kwa jina la YESU tunatoa mapepo, tunaachilia uponyaji kwa wagonjwa, tunawafungua waliotekwa na nguvu za giza kwa jina na damu yake YESU, nyinyi mna nni juu ya jina lake, au walio watafsria kitabu kitakatifu ndio waliowakosesha neema hii?
Kwa Quran mnampiga mtu mapepo, sisi kwa Bible tunayatoa kwa jina la YESU. Jina leny mamlaka, uponyaji, nguvu, uzima na lililobeba utukufu wa MUNGU.
Ukielewa hii wala husijibu chochote
Ni vema umeuliza hayo yote.
Labda nianze kwa kukupa pole kwa kuhisi unampenda Yesu haliyakua haufati lolote katika mafundisho na matendo yake. Na kwa bahati mbaya unajiona unafata.
1. Tuanze na suala lako la kumpokea kua mwokozi wa maisha yetu.
Sidhani kama hauyafahamu maneno ya Yesu mwenyewe aliposema.
"BABA HATOBEBA MZIGO WA MWANA NA WALA MWANA HATOBEBA MZIGO WA BABA. KILA MMOJA ATABEBA MZIGO WAKE MWENYEWE. "
Yesu kasema hivyo na sie waislamu tunaamini hivyo. Hatudanganywi na kina Paulo wanaobadili na Kusema amini na uokoke.
Sasa nani anamfata na nani hamfati?
2. Kuhusu suala la kusema tunampenda na hatufati maagizo yake pia unakosea.
YESU alisema Muabudu Mungu Baba Pekee. Na ndivyo tunavyofanya Waislamu wote. YESU ALISALI Kwa kusujudu na akasema MSUJUDIE BABA MUNGU WAKO PEKEE. nadhani imeshafahamu kua waislamu ndio Tunasali kwa kusujudu na wakristo kwa kukaa juu ya mabenchi.
3. Suala la Yesu kua mwana wa Mungu nalijibu pia kwa maandiko ya biblia yasemayo:-
"Msihuzunike kwa maana naenda Kwa Baba yangu ambae NI BABA YENU. na kwa MUNGU WANGU AMBAE NI MUNGU WENU.
hivyo Yesu kishasema baba yake ni baba yetu. Hivyo hata sie sote mimi na wewe ni wana wa Mungu. Na neno "wana wa Mungu" limetumika sana.
4.Suala la wewe kusema unatoa mapepo kwa Jina la Yesu.
Nalijibu pia kwa Maneno ya YESU yanaosema
Watakuja manabii wengi wa uongo. Watafanya miujiza mingi na WATAPOTOSHA WENGI.
PIA Naomba nichomekee kaswali kangu hapa. KANISA NI ENEO TAKATIFU? Kama ni eneo Takatifu HAYO MAPEPO machafu yanayotolewa ndani ya makanisa Yameingiaje humo ndani? Maana pepo chafu haliwezi kuingia eneo takatifu. Au labda sio Patakatifu?
Baada ya hayo nadhani utakua umeelewa kwamba waislamu ndio Tunafata maamrisho na makatako ya Manabii wote ikiwemo Yesu.
Soma vizuri kuna maswali pia nimeyauliza hapo na nitahitaji majibu.