Msaada wa jinsi ya kusamehe na kuachilia

Noted The Jackal!
 
Uhalisia wa msamaha uanzia ndani ya moyo wako,uwezi kumsamehe mtu kwa kusema tuu "eti nimekusamehe! huo uongo ndio maana maumivu hayaishi ndani yetu kumuachilia mtu si jambo jepes kihivyo.unahitaji msaada wa Mungu ili aweze kukusaidia uweze kumsahau na kumwachilia yule aliyekutenda.
 
Pole sana kwa matatizo ya kiafya,ambayo pengine yamesababishwa na fitna kazini, iwezi kukushauri kitu maana mimi pia wakati huu napitia kipindi kigumu mno kazini.
 

Pole sana mkuu bora ww huyo mbwa ni mtu baki, ngoja niishie hapa
 
Mimi kuna mtu aliwahi kuniumiza sana nikaamua kumpotezea ninaendelea na mishe zangu safi kabisa. Lakini kusema nae nimeshindwa kabisa maana tuko ofisi moja na sina kinyongo nae ila ndio hivyo kinywa kinakuwa kizito kabisa kusema nae.
 
Mimi kuna mtu aliwahi kuniumiza sana nikaamua kumpotezea ninaendelea na mishe zangu safi kabisa. Lakini kusema nae nimeshindwa kabisa maana tuko ofisi moja na sina kinyongo nae ila ndio hivyo kinywa kinakuwa kizito kabisa kusema nae.
Mimi ameniumizaga dada yangu ..nna 2yrs natafuta kisasi km naona vyote vyepesi ..yaan kabla corona haijapita na mimi lazima nimalizane naye kiroho safi kbs..ana kamwili kadogo kama jd bas nawazaga sijui nikambebe tu nilibwage road usk!
 
Mkuu kuna sehemu umeshindwa kujitafsiri na kujiwekea mipaka isivyokuwa na ulazima, unaupapasa uwezo wako na kujilinganisha sana na wengine (hili ni tatizo).

Kumbuka wewe ni wa pekee sana na hayupo kama wewe ila siyo lazima ujilinganishe na wengine ili kuuona upekee wako.

Tenga muda wa kutosha kwa ajili ya kujisikiliza wewe tu na siyo sauti za wengine. Kama unaweza kufanya meditation fanya.
 
Pamoja na maelezo yako marefu, mimi nimegundua kuwa hujui kutofautisha kati ya neno "kusamehe" , "kinyongo" na "kupuuza" na binafsi naomba nikujuze maana ya maneno hayo mawili kwa jinsi ninavyoyafahamu kimwili na kiroho:-

Kusamehe ni hali ya kuachilia jambo fulani lenye kuumiza au kukwaza pale unapokuwa umekosewa na mtu kisha mtu huyo akatambua kosa lake na akaja kukuomba msamaha, hivyo ukaamua kumsamehe au kutomsamehe (maana kusamehe siyo lazima). Sasa unapoamua kumsamehe mtu aliyekukosea/kukukwaza hakikisha msamaha huo umetoka ndani ya roho yako (usisamehe kwa mashinikizo ya viongozi wa dini au mtu yeyote yule, itakugharimu kiroho). Ukisamehe kutoka rohoni, haitakuumiza.

Kinyongo Ni hali ya kulimbikiza chuki moyoni kwa mtu aliyekukosea au kukukwaza na ukashindwa kumwambia pengine kwa kuwa ni mkubwa kwako au unamuogopa, hali hii hupelekea kujihaidi kulipa kisasi bila kujali kama unauwezo wa kulipa kisasi hicho au la, hali hii hupelekea kuhatarisha afya ya mwenye kinyongo jambo ambalo siyo zuri hasa pale kisasi kinaposhindikana.

Kupuuza ni hali ya kuachilia jambo fulani lenye kukuumiza au kukukwaza pale unapokuwa umekosewa na mtu kisha ukagundua mtu huyo hajielewe wala kujitambua kama amekukwaza, au jambo lenyewe siyo la kukupotezea muda wako maana pengine ni dogo hivyo unaamua kuliacha lakini kwa tahadhari ya kumuepuka mtu huyo bila kumsahau na kutomuhusisha tena kwenye mambo yako muhimu (hasa kama alikuwa mtu wa karibu kwa namna yoyote)

Hivyo basi kwa usalama wa afya ya mwili na roho yako, ikiwa mtu amekukosea na akakuomba msamaha siyo vibaya ukimsamehe . Ila kabla ya kumsamehe chambua faida na hasara za kutoa msamaha na hakikisha mkosaji ameonyesha kujutia kosa lake na ameomba huo msamaha (Usisamehe eti kwa kuwa YESU alisamehe maana YESU ni YESU na WEWE ni WEWE, kila mmoja ana changamoto zake na kwa wakati wake na makosa hayafanani).

Ukiona huwezi kusamehe mchukulie hatua za kisheria utakazoona zinafaa kwa muda huo, kamwe epuka kusamehe kwa kufurahisha watu maana tunatakiwa kuwapenda wenzetu kama tunavyopenda nafsi zetu (inaanza na kujipenda sisi) na umwambie kwa uwazi kamwe usimfiche kama ni deni alipe na kama ni kosa kazini awajibishwe kwa faida yako na ya umma.

MWSHO JAPO SI KWA UMUHIMU. UKISAMEHE KUTOKA ROHONI HUTOJUTIA KAMWE MAANA YATAPITA NA UTASAHAU LAKINI UKISAMEHE KIMWILI ITAKUUMIZA MAANA ITABAKI ROHONI DAIMA.
 
Mimi ameniumizaga dada yangu ..nna 2yrs natafuta kisasi km naona vyote vyepesi ..yaan kabla corona haijapita na mimi lazima nimalizane naye kiroho safi kbs..ana kamwili kadogo kama jd bas nawazaga sijui nikambebe tu nilibwage road usk!
Just forget her, time will heal you.

Ndugu yangu aliniumiza sana 2018 nikajisemea sitakaa niongee nae. Lkn after three years japo siongei nae kihivyo lkn bifu limeisha.
 
Just forget her, time will heal you...
Ndugu yangu aliniumiza sana 2018 nikajisemea sitakaa niongee nae. Lkn after three years japo siongei nae kihivyo lkn bifu limeisha.
Nashindwa


Unamsaidia mtu had kulipa fees lakini kumbe anataka kukuharibia biashara zako..ili iwaje..naona wazazi wake wamemshindwa mm ntamalizana naye..mm pia siongei naye 2yrs nw .anahaha tu kujua leo niko wapi...wanaye watanisamehe...na wananipenda ajabu
 
Mimi ameniumizaga dada yangu ..nna 2yrs natafuta kisasi km naona vyote vyepesi ..yaan kabla corona haijapita na mimi lazima nimalizane naye kiroho safi kbs..ana kamwili kadogo kama jd bas nawazaga sijui nikambebe tu nilibwage road usk!
Hahaha dah haya maisha yana mambo! Msamehe tu uendelee na maisha bila kinyongo ila ikishindikana kusamehe basi mlipue tu hakuna jinsi.
 
Namshukuru sana aliyenifundisha KUPUUZA japo nae aliingia kwenye mnyoyoro wa wakoseaji😂😂😂 nikampuuza nae maisha yangu yamekuwa mepesi sana tangu niijue siri ya kupuuza, inaendana sana na ubinafsi Yani sijali kabisa siku hizi na inawezekana wapo niliowaumiza kwa haka katabia ka kupuuza🤣🤣🤣 ila ndo siwazi kabisa Ni km mtu nimetangaziwa kifo chake ndivyo nafuta mtu kichwani kwangu
 
Vitu vya kawaida SANA! Unapataje hypertension?

Unatakiwa kuiacha ofisi ofisini, ukitoka mlangoni. Wewe unaibeba ofisi mpaka huku duniani??
Una kinyongo kibaya sana, usipoangalia diabetes inakuja pia.

Jichanganye na mambo mengine ya kijamii, tafuta marafiki nje ya ofisi, ofisi iwe ofisi tu, mkimaliza kunywa chai bye bye.

Utakufa mdogo, wenzako wanakula life!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kama umeshindwa kumsamehe na muhusika haonekani kujutia kosa lake unatakiwa umchukulie hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumueleza jinsi ulivyochukia/kuathirika na vitendo vyake viovu kwako (hii itasaidia kukuletea afueni ndani ya roho yako)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…