Msaada wa jinsi ya kusamehe na kuachilia

Unaweza kabisaaa kulimaliza hiki ndani kwako,uamuzi wote unabaki juu yako.
Mkeo alikushauru vizuri sana,ila hukutaka kuuchukua. Naona tatizo la kupenda ukamilifu kwenye kila kitu linakusumbua, jitahidi kukubaliana na kila kitu katika maisha. Hiyo jamaa yako m-face na mchane ukweli.
Umeweka kinyongo ambacho kitakiusumbua maishani mwako for life.
Jifunze kusamehe,kuachilia na kupuuza ukishindwa lipa kisasi,ila hii iwe option ya mwisho.
 
Hakuna kitu kibaya kama kuhifadhi chuki inauma sana na mbaya zaidi unaumia sana wewe kuliko aliekukosea

Mimi kuna namna mbili tu nazitumia kuzitoa chuki

1:- KUSAMEHE
Hapa ili nisamehe ni mpaka huyo alienikosea aje akili mbele yangu kuwa kakosea na aniombe msamaha ndipo nitasamehe, asipo omba msahaha siwezi kusamehe maana huenda hajui kama kanikosea. Sasa nitamsamehe vipi mtu ambaye yeye anadhani hajanikosea, na asipofanya kuomba msamaha itaniongezea chuki zaidi itanifanya niamni kuwa jamaa ana kiburi na hapo ndipo nitaitumia njia ya pili ambayo ni.

2:-KULIPIZA KISASI
Ili niyatoe maumivu itabidi nilipize kisasi, hapa nitahisi kutulia maana maumivu yatakuwa yamehama kutoka kwangu na kuhamia kwa huyo alienikosea.

Kusema nijifanye nimesamehe bila kuombwa nisamehe nikujindanganya bure na siwezi, mbaya zaidi huyo alienikosea aendelee kuniudhi siwezi aiseeeeeeee
Ukilipiza kisasi, wote mtakuwa mmekoseana. Ngoma droo
 
Nina roho moja ya huruma sana, ila mtu ambae huwa sina kifua nikisikia nasemwa au unanisema vibaya na nikaumia ni lazima nikuite nikupashe nilichokisikia ili nibalance pande zote nikitoka hapo nina aman zoote maaana ninapokuuliza n lazima nikupe maneno makali yatakayokuumiza tena kwa busara na kukuonyesha kuwa najua kila kitu unachonifanyia, hata tutakapo achana utabaki unanifikiria halafu tukionana tena mm nina aman zoote ila lazima nikuachie jeraha na ukose amani kila unaponiona

Amani yangu ni wewe ujue kuwa malengo yako mabaya juu yangu nimeyapata na ninajua kila kitu hapo hata usipoomba msamaha mm sijaliiiii!!!!! Tena hata nikikuona nakuchekea haswa [emoji28][emoji28][emoji28] ubaya wako utabaki unakutafuna mwenyew
 
Kuna mbwa mmoja anaitwa Godfrey. Mbwa huyu nilimtoa jalalani na kanipigia MAGOTI mpaka nikaona ngoja nimsaidie. Alivyokuja Mara ya kwanza mabosi walimkataa lkn nilimpigia debe mpaka akaajiriwa. Lunch nikawa nampeleka za nguvu huyu mbwa kwa hela zangu. Bar na hotel asizojua tulienda nae ili apate uzoefu wa kuwa wa mujini. Eeeh bwanaeh.

Alipojua udhaifu wa big boss, alijipenyeza na majungu ya Khali ya juu mpaka kwa hiari yangu nikaacha kazi.

NEVER WAKE A SLEEPING DOG. IT WILL WAKE UP AND BITE YOU.

Na Ninyi wanawake msipende sana ku wa introduce marafiki zenu wa kike kwa boyfriend zenu au Waume zenu.
Wengi wamelia.
NEVER WAKE A SLEEPING DOG. IT WILL WAKE UP AND BITE YOU. Hii point nimeikubali. Waswahili nao wana msemo: USIMWAMSHE MTU ALIYELALA, AKIAMKA UTALALA WEWE
 
Ndugu yangu nilisha samehe! ila nakumbuka na kuhisi tena maumivu.
Acha huo ujinga wa kushikiria watu moyoni!!! wateme kabisa haya mambo ya chuki yalianzia mbinguni kitambo wewe!!!! hata iweje haiepukiki hii!!! huyo mkeo anae muamini, nalala nae aweza pia kukugeuka akala na Boss wako utalia lia mpaka Yesu arudi!!!

Kamata hiro richeo umepewa Bure!! na Boss wewe. unariachia kweli kiulaini kweli lina nafasi zuri hivo? hata Yesu akija leo watu watajaribu kukupiga majungu usiende Mbinguni!! unavoonekana dhaifu utashindwa kujitetea!!

Watu tumeuguza wake zetu wagonjwa kabisa hawatembei wamelala tu!! lkn bado walitukimbia!! wengi wazazi wenzetu tumewapa kazi nzuri still wakatufitini tukafukuzwa lkn bado tunawapa mpunga bila kinyongo!! sembuse hao!

unasikiliza wanawake kazini?? komaa nahuyo rafiki yako kazi usiache kama una Mungu wa kweli sali sana tena sana!! km huna Mizizi ninayo Tele! piga chini wote hao ikibidi wachinje live!!! usiwe padri!!! kinyume na hapo hata mbinguni huendi!!!
 
Na kwa kusema hivyo anayefaidika zaidi na msamaha ni yule anayekosewa. Si yule anayekosea! Faida ya kusamehe toka moyoni ni kuondokana na maumivu yatokanayo na aliyekukosea au kukuumiza. Ukiijua siri hiyo hutabaki na wabaya wako na maumivu yao moyoni mwako.

Hata Mungu hutusamehe kwa faida yake Mwenyewe - kwa ajili ya utukufu wa jina lake. Hapendi aendelee kuumia kwa makosa na viburi vyetu kwake.

Achilia au yatupilie mbali makosa ya watu kwako ili upate amani moyoni. Kaa nao mbali moyoni na hata kimwili ikiwezekana!
Naam iko hivi ukisamehe unakuwa umeutua mzigo wa sonona ... Samehe kwaajili ya kuepuka kujiumiza
 
Mimi roho ya kusamehe niliiacha mwaka 2012 ( nilikua sijawah huru kiuchumi. Ivo ikawa inanilazimu kua Mpole )

Siku hizi roho yangu ni ya visasi tu .. Ukinifanyia ufedhuli, kama unahitaj nikulipue hapo hapo ,nakulipua, kama unahitaj twende kichwa kichwa tunaenda

Kikubwa Nilichofanya, Ni kutokuchukulia kwa uzito , Yaan Unanifanyia ubaya. Nachukulia poa, lkn ukae ukitambua dawa yako ipo jikoni inakwiva na utainywa tu.

Haya maisha yamenipa Amani sana !!

Kwa jambo kama lako, kwa sheria yangu, mimi sio mtu sahihi wa kukushauri hapa.
Safi sana Mkuu upo kama Mimi, hakuna kusamehe kwa mtu aliedhamiria kabisa kukuharibia future yako. Unachukulia poa huku ukisubiri chance ya kulipiza kisasi itokee hata iwe imepita miaka 5.
 
Habari wana JF!

Mimi ni Muhanga wa hali hii nimevumilia sana lakini nimeshindwa. Juzi kuna jamaa yangu amekuja hapa kunihadithia kisa kilichomkuta maishani mwake ameshindwa kabisa kusamehe na kuachilia inagawaje anadai hana shida na watu waliomuumiza na kumpiga majungu.

Baada ya kunieleza kisa chenyewe akawa kama amenitonesha kidonda. Nakumbuka ilikuwa 2017 kazini (Naomba nisitaje kazi ninayofanya,ukiconnect dots naomba utulie tu). Ndipo nilipoona hamna maana ya kuwa na marafiki na kuwathamini sana na ndio kilichonifanya kutambua kuwa bado nina maumivu moyoni kama ya jamaa yangu huyu aliyenielezea kisa chake ambacho kwa leo nakiweka kipolo nieleze kisa changu kwanza.

Ilianza hivi,nilimpokea jamaa kazini akawa rafiki yangu wa karibu,alisema alishawahi kuwa mtumishi wa kada yetu huko sekta binafsi lakini akawa hakuna anachojua,nikawa msaada mkubwa kwake na tukaendelea na maisha vizuri tu,tukaendelea kupokea watumishi wengine tukawa tunaongezeka pale kazini pakachangamka sana.

Bahati mbaya Boss wetu akapata matatizo akawa kashushwa cheo,Jamaa yangu akapata kile cheo,alipopewa barua breki ya kwanza akaja kwangu akanionesha barua akaniomba nimsaidie niwe msaidizi wake namba mbili huku akirejea jinsi ambavyo tuliishi vema na msaada niliompa wakati wote. Nikakubali nikamwambia tupige kazi.

Akaja jamaa mwingine mtu mzima kama yeye! akaripoti pale kazini,kwa jinsi alivyoonekana alionekana ni Mtaratibu na mshika dini sana,basi jamaa akamchagua kuwa msaidizi chini yangu,hivyo tukawa watu watatu ndio tuna sauti pale kazini.

Sasa watumishi wenzetu wakawa wanamsema sana Boss! kuwa hajali watu anajiamuria mambo bila kushirikisha wengine,na wakati wanamsema hivyo wanasubiri mimi nikiwa nao ndio wanayasema hayo,na wengine wana sisitiza we si ndio msaidizi wake mwambie jamaa yako mambo huwa hayaendi ivo.

Basi nikajiridhisha kuwa kuna hoja ni za msingi na hoja zingine ni majungu tu! Nikamfuata ofisini nikamwambia tuongee kidogo,nikampasha nini kinaendelea pale kazini na nikamshauri kuwa mengine ni majungu lakini mengine ajaribu kuyatolea ufafanuzi wa kina kwa watumishi wenzetu ili kuondoa tashwishi na ili mambo yaendelee vizuri.

Basi jamaa akawa kama amenielewa akaniagiza niandike memo ya kuwataarifu kuwa siku flani kutakuwa na kikao,nikafanya hivyo kama alivyoagiza.

Hali ikanibadilika ghafla jamaa akaanza kunipiga vijembe, mara watumishi wengine wanalalamika kuwa ananipendelea sana mimi, mala mimi ni mzembe, mambo yakawa mengi sana.

Sikujua nifanye nini? Baada ya muda watumishi wengine wakaanza kunipa ubuyu,(Wanawake Mbarikiwe sana) Huyu Mdada tunafanya nae kazi akanieleza siku ambazo haujaja kazini jamaa yako anakusema vibaya sana,anadai humsaidii mara umebadirika sana hukuwa hivyo mwanzo,hasa baada ya kufunga ndoa umekuwa wa tofauti sana,Labda Ndoa inakusumbua?

Sikujali nikapuuza! Sasa pale ofisini jamaa sio mtaalam sana wa mambo ya mifumo ya Serikali, mimi ndie nilikuwa kilaka pale,akawa ananiagiza kufanya mambo bila malipo,nikaendelea kufanya bila shida.

Nikaja kupata taarifa kuwa yule jamaa aliyeteuliwa kuwa msaidizi wako na Boss ndie anayekufitini sana! Nikajiuliza sana,inamaana Boss hanifahamu kabisa mpaka anaamini kila anachoambiwa na Jamaa naomba hapa nimpe jina la Shemasi huyu Mfitini wangu.

Basi Shemasi akawa ndie mwandani wa Boss, sikujali sana, sasa wakaanza kuwa wana ni SIDELINE,yaani Kama wananiepuka vile,Ikawa Boss akiondoka kikazi ananiachia majukumu lakini kumbe shemasi kaagizwa anifautilie kwa ukaribu.

Hilo sikulipenda ila nikajikaza,lakini pia nikashidwa,ikabidi nimshirikishe Mke wangu!Mke wangu akaniambia fitina ni kawaida komaa nao! Usiache hiyo nafasi endelea kumsaidia jamaa ako.

Mimi Ni Mkristo nikaanza kusali na kuomba maarifa nifanyeje sasa! Ikafika kipindi hasira ikapanda sana nikasema sasa! Ngoja nikamripue huyu asinifanye mimi zuzu kwa kuwa najua anachonifanyia ila nimeamua kunyamaza tu! Nilipanga nikaseme ukweli wote na yanayoendelea kuwa najua asinifanye mie Mjinga,lakini Kabla sijafanya hiyvo nikaingia kwenye Maombi - Baada ya Kuomba nikasikia msukumo wa ajabu - Kuwa Nisiseme chochote nitulie tu! Basi nikaisikiliza ule msukumo nikatulia.

Mambo yakaendelea vile vile hakuna mabadiliko! Jamaa chuki ikazidi sana juu yangu,nikasikia anadai kuna mtumishi mwenzetu huko Chuo Kikuu akija tu! basi atanitoa na atampatia huyo Jamaa Nafasi yangu.

Kwa kweli nilipigwa majungu sana ambayo mengine siwezi eleza hapa ili kuendelea kuficha jina na Taasisi ninayofanyia Kazi.

Nikaona isiwe tabu sana! Nikamfuata Ofisini kwake kwa Upole sana! Nikamwambia Boss mi naomba nimpumzike sasa! Kama ni uzoefu wapo wengi wanaoweza kukusaidia! Mimi naomba nipumzike kwa Sababu kuna Mambo ambayo nataka kufanya yanaweza kuathiri utendaji wangu.

Hakuafiki! akaniambia unaweza kuendelea tu kunisaidia na ukaendelea na mambo yako pia! Nikakataa nikamwambia hapana kabisa.

Basi baada ya Muda Shemasi akapandishwa cheo akahama pale,na muda huo huo yule jamaa akarudi toka masomoni,Akamshawishi jamaa kuwa msaidizi wake, jamaa nae akakataa kabisa akidai wapo wakongwe na watu wenye Uzoefu mzuri kuliko yeye! inakuwaje ametoka masomoni tu afikie kushika nafasi.

Basi akaniiita akanieleza kuwa jamaa amekataa akawa amenishilikisha kuwa kati ya Hawa (Akawataja Majina) na nani anafaa? sikuweka neno la ziada zaidi ya kusema wote wanafaa,basi akachagua mmoja wa wale alionitajia majina nikamuunga mkono kuwa huyo aliyechangua ni mtendaji mzuri anafaa.

Muda si Mrefu Nikawa nimepata Nafasi ya kusimamia zoezi flani hivi lina pesa kiasi! Nikawa Boss kwa muda sikuwa na roho ya Kinyongo - Ingawaje nilipomshirikisha Wife alinishauri nisimchague kwenye hilo zoezi kabisa,lakini sikufanya hivyo nikamteua na kuteua na watu wake wa Karibu bila Kinyongo tukamaliza ile kazi,kila mtu akapata cha kwake,ingawaje yeye aliacha kabisa kunipa deal za pesa,akawa anawapa wale wanaomfurahisha tu.

Sasa Jamaa baada ya Kuja kunisimulia jinsi alivyo nyanyaswa na Mkubwa wake kazini, nimegundua kwamba nilishamsamehe jamaa lakini bado nina maumivu na mbaya zaidi nimegundulika kuwa na Matatizo ya kiafya ambayo sikuwahi kuwa nayo huko nyuma na ni imani yangu ya kuwa kwa namna moja ama nyingine huyu jamaa alivyonitendea ndio chanzo cha hypertension yangu.

Naomba msaada ndugu zangu! Sihitaji kulipa kisasi,nahitaji maisha yangu yaendelee! nawezaje kuachilia nahisi kama bado ipo hali ya kuumia kila wakati ninapokumbuka yaliyonisibu.

Asanteni.
Mimi nitakua kinyume na wachangiaje wengine , sawa kusamehe ni jambo jema na la kiujasiri sana, ila nikuambie mkuu mimi siwezi kuishi na jambo linalonitesa moyoni, huwa nalimwaga kama mbwai na iwe mbwai, silei chuki nafunguka vibaya mno ili kuufanya moyo wangu uwe safi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa ya moyoni utawaogopa watu mpaka lini, mfuga maradhi kifo humuumbua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kuna mtu aliwahi kuniumiza sana nikaamua kumpotezea ninaendelea na mishe zangu safi kabisa. Lakini kusema nae nimeshindwa kabisa maana tuko ofisi moja na sina kinyongo nae ila ndio hivyo kinywa kinakuwa kizito kabisa kusema nae.

Unatakiwa kinywa kiwe chepesi usifuge panya wanaokula nguo zako hutabaki na kitu, teketeza wenye chuki ili moyo uwe safi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unatakiwa kinywa kiwe chepesi usifuge panya wanaokula nguo zako hutabaki na kitu, teketeza wenye chuki ili moyo uwe safi

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa nitateketezaje mpendwa nguvu ya kulipiza kisasi sina nimeamua kusamehe maisha yasonge sema kuzungumza nae ndio siwezi kwakweli kinywa kimekuwa kizito ajabu tunapishana kama hatuonani vile😀
 
Nina roho moja ya huruma sana, ila mtu ambae huwa sina kifua nikisikia nasemwa au unanisema vibaya na nikaumia ni lazima nikuite nikupashe nilichokisikia ili nibalance pande zote nikitoka hapo nina aman zoote maaana ninapokuuliza n lazima nikupe maneno makali yatakayokuumiza tena kwa busara na kukuonyesha kuwa najua kila kitu unachonifanyia, hata tutakapo achana utabaki unanifikiria halafu tukionana tena mm nina aman zoote ila lazima nikuachie jeraha na ukose amani kila unaponiona

Amani yangu ni wewe ujue kuwa malengo yako mabaya juu yangu nimeyapata na ninajua kila kitu hapo hata usipoomba msamaha mm sijaliiiii!!!!! Tena hata nikikuona nakuchekea haswa [emoji28][emoji28][emoji28] ubaya wako utabaki unakutafuna mwenyew
Wewe ni kama mimi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom