Msaada wa jinsi ya kusamehe na kuachilia

Msaada wa jinsi ya kusamehe na kuachilia

Habari wana JF!

Mimi ni Muhanga wa hali hii nimevumilia sana lakini nimeshindwa. Juzi kuna jamaa yangu amekuja hapa kunihadithia kisa kilichomkuta maishani mwake ameshindwa kabisa kusamehe na kuachilia inagawaje anadai hana shida na watu waliomuumiza na kumpiga majungu.

Baada ya kunieleza kisa chenyewe akawa kama amenitonesha kidonda. Nakumbuka ilikuwa 2017 kazini (Naomba nisitaje kazi ninayofanya,ukiconnect dots naomba utulie tu). Ndipo nilipoona hamna maana ya kuwa na marafiki na kuwathamini sana na ndio kilichonifanya kutambua kuwa bado nina maumivu moyoni kama ya jamaa yangu huyu aliyenielezea kisa chake ambacho kwa leo nakiweka kipolo nieleze kisa changu kwanza.

Ilianza hivi,nilimpokea jamaa kazini akawa rafiki yangu wa karibu,alisema alishawahi kuwa mtumishi wa kada yetu huko sekta binafsi lakini akawa hakuna anachojua,nikawa msaada mkubwa kwake na tukaendelea na maisha vizuri tu,tukaendelea kupokea watumishi wengine tukawa tunaongezeka pale kazini pakachangamka sana.

Bahati mbaya Boss wetu akapata matatizo akawa kashushwa cheo,Jamaa yangu akapata kile cheo,alipopewa barua breki ya kwanza akaja kwangu akanionesha barua akaniomba nimsaidie niwe msaidizi wake namba mbili huku akirejea jinsi ambavyo tuliishi vema na msaada niliompa wakati wote. Nikakubali nikamwambia tupige kazi.

Akaja jamaa mwingine mtu mzima kama yeye! akaripoti pale kazini,kwa jinsi alivyoonekana alionekana ni Mtaratibu na mshika dini sana,basi jamaa akamchagua kuwa msaidizi chini yangu,hivyo tukawa watu watatu ndio tuna sauti pale kazini.

Sasa watumishi wenzetu wakawa wanamsema sana Boss! kuwa hajali watu anajiamuria mambo bila kushirikisha wengine,na wakati wanamsema hivyo wanasubiri mimi nikiwa nao ndio wanayasema hayo,na wengine wana sisitiza we si ndio msaidizi wake mwambie jamaa yako mambo huwa hayaendi ivo.

Basi nikajiridhisha kuwa kuna hoja ni za msingi na hoja zingine ni majungu tu! Nikamfuata ofisini nikamwambia tuongee kidogo,nikampasha nini kinaendelea pale kazini na nikamshauri kuwa mengine ni majungu lakini mengine ajaribu kuyatolea ufafanuzi wa kina kwa watumishi wenzetu ili kuondoa tashwishi na ili mambo yaendelee vizuri.

Basi jamaa akawa kama amenielewa akaniagiza niandike memo ya kuwataarifu kuwa siku flani kutakuwa na kikao,nikafanya hivyo kama alivyoagiza.

Hali ikanibadilika ghafla jamaa akaanza kunipiga vijembe, mara watumishi wengine wanalalamika kuwa ananipendelea sana mimi, mala mimi ni mzembe, mambo yakawa mengi sana.

Sikujua nifanye nini? Baada ya muda watumishi wengine wakaanza kunipa ubuyu,(Wanawake Mbarikiwe sana) Huyu Mdada tunafanya nae kazi akanieleza siku ambazo haujaja kazini jamaa yako anakusema vibaya sana,anadai humsaidii mara umebadirika sana hukuwa hivyo mwanzo,hasa baada ya kufunga ndoa umekuwa wa tofauti sana,Labda Ndoa inakusumbua?

Sikujali nikapuuza! Sasa pale ofisini jamaa sio mtaalam sana wa mambo ya mifumo ya Serikali, mimi ndie nilikuwa kilaka pale,akawa ananiagiza kufanya mambo bila malipo,nikaendelea kufanya bila shida.

Nikaja kupata taarifa kuwa yule jamaa aliyeteuliwa kuwa msaidizi wako na Boss ndie anayekufitini sana! Nikajiuliza sana,inamaana Boss hanifahamu kabisa mpaka anaamini kila anachoambiwa na Jamaa naomba hapa nimpe jina la Shemasi huyu Mfitini wangu.

Basi Shemasi akawa ndie mwandani wa Boss, sikujali sana, sasa wakaanza kuwa wana ni SIDELINE,yaani Kama wananiepuka vile,Ikawa Boss akiondoka kikazi ananiachia majukumu lakini kumbe shemasi kaagizwa anifautilie kwa ukaribu.

Hilo sikulipenda ila nikajikaza,lakini pia nikashidwa,ikabidi nimshirikishe Mke wangu!Mke wangu akaniambia fitina ni kawaida komaa nao! Usiache hiyo nafasi endelea kumsaidia jamaa ako.

Mimi Ni Mkristo nikaanza kusali na kuomba maarifa nifanyeje sasa! Ikafika kipindi hasira ikapanda sana nikasema sasa! Ngoja nikamripue huyu asinifanye mimi zuzu kwa kuwa najua anachonifanyia ila nimeamua kunyamaza tu! Nilipanga nikaseme ukweli wote na yanayoendelea kuwa najua asinifanye mie Mjinga,lakini Kabla sijafanya hiyvo nikaingia kwenye Maombi - Baada ya Kuomba nikasikia msukumo wa ajabu - Kuwa Nisiseme chochote nitulie tu! Basi nikaisikiliza ule msukumo nikatulia.

Mambo yakaendelea vile vile hakuna mabadiliko! Jamaa chuki ikazidi sana juu yangu,nikasikia anadai kuna mtumishi mwenzetu huko Chuo Kikuu akija tu! basi atanitoa na atampatia huyo Jamaa Nafasi yangu.

Kwa kweli nilipigwa majungu sana ambayo mengine siwezi eleza hapa ili kuendelea kuficha jina na Taasisi ninayofanyia Kazi.

Nikaona isiwe tabu sana! Nikamfuata Ofisini kwake kwa Upole sana! Nikamwambia Boss mi naomba nimpumzike sasa! Kama ni uzoefu wapo wengi wanaoweza kukusaidia! Mimi naomba nipumzike kwa Sababu kuna Mambo ambayo nataka kufanya yanaweza kuathiri utendaji wangu.

Hakuafiki! akaniambia unaweza kuendelea tu kunisaidia na ukaendelea na mambo yako pia! Nikakataa nikamwambia hapana kabisa.

Basi baada ya Muda Shemasi akapandishwa cheo akahama pale,na muda huo huo yule jamaa akarudi toka masomoni,Akamshawishi jamaa kuwa msaidizi wake, jamaa nae akakataa kabisa akidai wapo wakongwe na watu wenye Uzoefu mzuri kuliko yeye! inakuwaje ametoka masomoni tu afikie kushika nafasi.

Basi akaniiita akanieleza kuwa jamaa amekataa akawa amenishilikisha kuwa kati ya Hawa (Akawataja Majina) na nani anafaa? sikuweka neno la ziada zaidi ya kusema wote wanafaa,basi akachagua mmoja wa wale alionitajia majina nikamuunga mkono kuwa huyo aliyechangua ni mtendaji mzuri anafaa.

Muda si Mrefu Nikawa nimepata Nafasi ya kusimamia zoezi flani hivi lina pesa kiasi! Nikawa Boss kwa muda sikuwa na roho ya Kinyongo - Ingawaje nilipomshirikisha Wife alinishauri nisimchague kwenye hilo zoezi kabisa,lakini sikufanya hivyo nikamteua na kuteua na watu wake wa Karibu bila Kinyongo tukamaliza ile kazi,kila mtu akapata cha kwake,ingawaje yeye aliacha kabisa kunipa deal za pesa,akawa anawapa wale wanaomfurahisha tu.

Sasa Jamaa baada ya Kuja kunisimulia jinsi alivyo nyanyaswa na Mkubwa wake kazini, nimegundua kwamba nilishamsamehe jamaa lakini bado nina maumivu na mbaya zaidi nimegundulika kuwa na Matatizo ya kiafya ambayo sikuwahi kuwa nayo huko nyuma na ni imani yangu ya kuwa kwa namna moja ama nyingine huyu jamaa alivyonitendea ndio chanzo cha hypertension yangu.

Naomba msaada ndugu zangu! Sihitaji kulipa kisasi,nahitaji maisha yangu yaendelee! nawezaje kuachilia nahisi kama bado ipo hali ya kuumia kila wakati ninapokumbuka yaliyonisibu.

Asanteni.
wewe inaonyesha kuna mazingira hujawaii kuishi mimi naweza pishana na mtuu mwaka mzima na tuko sehemu moja huwa na tabia ya kutokujali hasa pale napo ona niko sahihi kwa upande wangu.

kwa maelezo yako kwanza una huruma sana na pia kuna maisha ambayo huja wai kuyaishi no maana unakuwa unapata matatizo madogo madogo ya msongo wa mawazo. japo una onekana uko vizuri kazini lakini bado una kasoro moja, kuishi wewe kama wewe.

mke wako aliogea ukweli usimpe hiyo deal wewe umetoa na pia kazini unajua yeye sio mfanisi juu na mzoefu kama wewe kwanini una nyenyekea kuna mda unakuwa mkaksi na kukataa kazi mfano kama ambazo hazina malipo.

kazini mwenye tatizo sio wewe bali ni yeye japo ukiingia ofisini unaona kama tatizo kubwa ni wewe cha msingi jenga uhusiano mzuri na wafanyakazi wengine kwa ukaribu zaidi na anza kumchukulia kama boss na sio rafiki tena maana sio kwa tabia anazo onyesha kuwa huru pale kwenye ukweli itakuwia vigumu kama huja zoea ni hayo tu... rafiki wa kweli ni muwazi na mkwelii

(sijaeleza kiundani ila nime jaribu)
 
Kama umeshindwa kumsamehe na muhusika haonekani kujutia kosa lake unatakiwa umchukulie hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumueleza jinsi ulivyochukia/kuathirika na vitendo vyake viovu kwako (hii itasaidia kukuletea afueni ndani ya roho yako)
Mhusika haonekani kujutia kosa lake kabisa...amefikia.hatua anataFut vibaka waje waniibie kwenye kaz zangu nilost..! Aliwah mwambia dada wa kazi wang aweke chumv kwa engine atamlipa🤨...yaan kosa halipo..
 
wewe inaonyesha kuna mazingira hujawaii kuishi mimi naweza pishana na mtuu mwaka mzima na tuko sehemu moja huwa na tabia ya kutokujali hasa pale napo ona niko sahihi kwa upande wangu.

kwa maelezo yako kwanza una huruma sana na pia kuna maisha ambayo huja wai kuyaishi no maana unakuwa unapata matatizo madogo madogo ya msongo wa mawazo. japo una onekana uko vizuri kazini lakini bado una kasoro moja, kuishi wewe kama wewe.

mke wako aliogea ukweli usimpe hiyo deal wewe umetoa na pia kazini unajua yeye sio mfanisi juu na mzoefu kama wewe kwanini una nyenyekea kuna mda unakuwa mkaksi na kukataa kazi mfano kama ambazo hazina malipo.

kazini mwenye tatizo sio wewe bali ni yeye japo ukiingia ofisini unaona kama tatizo kubwa ni wewe cha msingi jenga uhusiano mzuri na wafanyakazi wengine kwa ukaribu zaidi na anza kumchukulia kama boss na sio rafiki tena maana sio kwa tabia anazo onyesha kuwa huru pale kwenye ukweli itakuwia vigumu kama huja zoea ni hayo tu... rafiki wa kweli ni muwazi na mkwelii

(sijaeleza kiundani ila nime jaribu)

Wanaume wengi hawawezi kuishi hvyo...mm hata 5yrs napishana tu na ww kiroho safi..
 
Pole sana mkuu. Ni kweli hypertension inaweza kuchangiwa sana na hiyo stress ulitopitia kwa kipindi kirefu. Una alternatives 2:
1_ imani zote zinasisitiza juu ya msamaha. Unaweza kwenda kwa kiongozi wako wa dini kwa ushauri nasaha. Baada ya hapo akuombee. Ningekuwa wewe ningetoa na sadaka ya kumuachilia. Sadaka ina nguvu kubwa sana katika imani yako na nina hakika ingekusaidia (binafsi nilishawahi kumtolea sadaka mtu alienitesa sana kazini. Mungu alivyo muaminifu yule ndugu aliondolewa)

2_ Counseling. Kuna washauri nasaha ambao wanaweza kukusaidia kupambana na hii hali. Japo ina gharama kiasi lakini unahitaji kupona.

Kila la kheri. Kusamehe ni muhimu sana kwako. Usijiadhibu kwa makosa uliyotendewa, unajionea.

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Na kwa kusema hivyo anayefaidika zaidi na msamaha ni yule anayekosewa. Si yule anayekosea! Faida ya kusamehe toka moyoni ni kuondokana na maumivu yatokanayo na aliyekukosea au kukuumiza. Ukiijua siri hiyo hutabaki na wabaya wako na maumivu yao moyoni mwako.

Hata Mungu hutusamehe kwa faida yake Mwenyewe - kwa ajili ya utukufu wa jina lake. Hapendi aendelee kuumia kwa makosa na viburi vyetu kwake.

Achilia au yatupilie mbali makosa ya watu kwako ili upate amani moyoni. Kaa nao mbali moyoni na hata kimwili ikiwezekana!
Uhalisia wa msamaha uanzia ndani ya moyo wako,uwezi kumsamehe mtu kwa kusema tuu " eti nimekusamehe..! huo uongo ndio maana maumivu hayaishi ndani yetu kumuachilia mtu si jambo jepes kihivyo.unahitaji msaada wa Mungu ili aweze kukusaidia uweze kumsahau na kumwachilia yule aliyekutenda
 
Sahihi kabisa!
Pamoja na maelezo yako marefu, mimi nimegundua kuwa hujui kutofautisha kati ya neno "kusamehe" , "kinyongo" na "kupuuza" na binafsi naomba nikujuze maana ya maneno hayo mawili kwa jinsi ninavyoyafahamu kimwili na kiroho:-

Kusamehe ni hali ya kuachilia jambo fulani lenye kuumiza au kukwaza pale unapokuwa umekosewa na mtu kisha mtu huyo akatambua kosa lake na akaja kukuomba msamaha, hivyo ukaamua kumsamehe au kutomsamehe (maana kusamehe siyo lazima). Sasa unapoamua kumsamehe mtu aliyekukosea/kukukwaza hakikisha msamaha huo umetoka ndani ya roho yako (usisamehe kwa mashinikizo ya viongozi wa dini au mtu yeyote yule, itakugharimu kiroho). Ukisamehe kutoka rohoni, haitakuumiza.

Kinyongo Ni hali ya kulimbikiza chuki moyoni kwa mtu aliyekukosea au kukukwaza na ukashindwa kumwambia pengine kwa kuwa ni mkubwa kwako au unamuogopa, hali hii hupelekea kujihaidi kulipa kisasi bila kujali kama unauwezo wa kulipa kisasi hicho au la, hali hii hupelekea kuhatarisha afya ya mwenye kinyongo jambo ambalo siyo zuri hasa pale kisasi kinaposhindikana.

Kupuuza ni hali ya kuachilia jambo fulani lenye kukuumiza au kukukwaza pale unapokuwa umekosewa na mtu kisha ukagundua mtu huyo hajielewe wala kujitambua kama amekukwaza, au jambo lenyewe siyo la kukupotezea muda wako maana pengine ni dogo hivyo unaamua kuliacha lakini kwa tahadhari ya kumuepuka mtu huyo bila kumsahau na kutomuhusisha tena kwenye mambo yako muhimu (hasa kama alikuwa mtu wa karibu kwa namna yoyote)

Hivyo basi kwa usalama wa afya ya mwili na roho yako, ikiwa mtu amekukosea na akakuomba msamaha siyo vibaya ukimsamehe . Ila kabla ya kumsamehe chambua faida na hasara za kutoa msamaha na hakikisha mkosaji ameonyesha kujutia kosa lake na ameomba huo msamaha (Usisamehe eti kwa kuwa YESU alisamehe maana YESU ni YESU na WEWE ni WEWE, kila mmoja ana changamoto zake na kwa wakati wake na makosa hayafanani).

Ukiona huwezi kusamehe mchukulie hatua za kisheria utakazoona zinafaa kwa muda huo, kamwe epuka kusamehe kwa kufurahisha watu maana tunatakiwa kuwapenda wenzetu kama tunavyopenda nafsi zetu (inaanza na kujipenda sisi) na umwambie kwa uwazi kamwe usimfiche kama ni deni alipe na kama ni kosa kazini awajibishwe kwa faida yako na ya umma.

MWSHO JAPO SI KWA UMUHIMU. UKISAMEHE KUTOKA ROHONI HUTOJUTIA KAMWE MAANA YATAPITA NA UTASAHAU LAKINI UKISAMEHE KIMWILI ITAKUUMIZA MAANA ITABAKI ROHONI DAIMA.
 
Ushauri murua kabisa
Pole sana mkuu. Ni kweli hypertension inaweza kuchangiwa sana na hiyo stress ulitopitia kwa kipindi kirefu. Una alternatives 2:
1_ imani zote zinasisitiza juu ya msamaha. Unaweza kwenda kwa kiongozi wako wa dini kwa ushauri nasaha. Baada ya hapo akuombee. Ningekuwa wewe ningetoa na sadaka ya kumuachilia. Sadaka ina nguvu kubwa sana katika imani yako na nina hakika ingekusaidia (binafsi nilishawahi kumtolea sadaka mtu alienitesa sana kazini. Mungu alivyo muaminifu yule ndugu aliondolewa)

2_ Counseling. Kuna washauri nasaha ambao wanaweza kukusaidia kupambana na hii hali. Japo ina gharama kiasi lakini unahitaji kupona.

Kila la kheri. Kusamehe ni muhimu sana kwako. Usijiadhibu kwa makosa uliyotendewa, unajionea.

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Nimewahi andika juu ya kinyongo changu kwa Marehemu Sr. Mary Antony. Yaani toka primary mpaaka ule mwaka nilioleta kisa changu hapa. Hiyo ilikua ni early 2000s. Yaan kinyongo kiliendelea hata alipokufa. Lakini siku niliposimulia humu ndo siku niliachilia rasmi. Yaan sijawahi kuumia tena nikisia jina lake. Kuongea kunasaidia sana. Yaan hata kwenda kumuaga nilikataa kabisa nikiwa nimefika chuo hapo Luguruni hapo. Mpaka kesho sijisikii tena kumchukia. Natafuta siku niende convent kwao makaburini kuweka maua kbs. Nafurahi mno maana imenitesa sana zaidi ya 15 years. Kuongea kuna faida. Umefanya jambo jema sana. Utanambia after some time...

May you heal from this brother
 
Ndugu yangu nilisha samehe! ila nakumbuka na kuhisi tena maumivu.
Hakuna msamaha wa kweli pasipo kuweka wazi tatizo. Ulipaswa umwambie ukweli boss wako ndipo usamehe, lakini wewe mwenyewe uliamua ukae nalo and that's what has been eating you mpaka kuwa na hypertension.
Kwa boss wako ushachelewa Sana coz yaonekana mambo sasa ni shwari kwasababu ulichagua njia hiyo, ila ingekuwa shwari zaidi Kama boss wako angejua kuwa unajua kila kitu na majungu aliyokuwa akikupiga.
Kwasasa ongeza maombi na tafuta rehema za Mungu mwenyewe, vinginevyo utaingia kwenye Imani nyingine itakayokugarimu zaidi.
 
Nak
Nimewahi andika juu ya kinyongo changu kwa Marehemu Sr. Mary Antony. Yaani toka primary mpaaka ule mwaka nilioleta kisa changu hapa. Hiyo ilikua ni early 2000s. Yaan kinyongo kiliendelea hata alipokufa. Lakini siku niliposimulia humu ndo siku niliachilia rasmi. Yaan sijawahi kuumia tena nikisia jina lake. Kuongea kunasaidia sana. Yaan hata kwenda kumuaga nilikataa kabisa nikiwa nimefika chuo hapo Luguruni hapo. Mpaka kesho sijisikii tena kumchukia. Natafuta siku niende convent kwao makaburini kuweka maua kbs. Nafurahi mno maana imenitesa sana zaidi ya 15 years. Kuongea kuna faida. Umefanya jambo jema sana. Utanambia after some time...

May you heal from this brother
Nakumbuka kisa chako. Hopeful now you're ok
 
Nak

Nakumbuka kisa chako. Hopeful now you're ok
I am very good aisee. Yaan siku hizi hata umtaje je.. siumii zaidi naona kama nammiss. Yule sista ilibidi akasomee jeshi. Halaf enzi hizo walikua wanapitia jeshini. Maana amepanda hewani balaa halaf ana mkono wa kutosha. Wanawake wa kibosho ni wakorofi in general. Nilipoelewa hili ilikua rahisi zaidi kusamehe
 
Nimewahi andika juu ya kinyongo changu kwa Marehemu Sr. Mary Antony. Yaani toka primary mpaaka ule mwaka nilioleta kisa changu hapa. Hiyo ilikua ni early 2000s. Yaan kinyongo kiliendelea hata alipokufa. Lakini siku niliposimulia humu ndo siku niliachilia rasmi. Yaan sijawahi kuumia tena nikisia jina lake. Kuongea kunasaidia sana. Yaan hata kwenda kumuaga nilikataa kabisa nikiwa nimefika chuo hapo Luguruni hapo. Mpaka kesho sijisikii tena kumchukia. Natafuta siku niende convent kwao makaburini kuweka maua kbs. Nafurahi mno maana imenitesa sana zaidi ya 15 years. Kuongea kuna faida. Umefanya jambo jema sana. Utanambia after some time...

May you heal from this brother

Hahaa umenikumbusha luguruni..lol
 
Kama bado anaendelea kukupiga majungu,kaa nae chini,ongea nae Kama rafiki wa mwanzo,ongea nae kwa upendo na hekima,yeye ni binadamu naamini atakuelewa ,unamwambia ukweli.kukaa kimya itamfanya aone unajipanga kulipiza kisasi juu yake,kwa kuwa anajua aliyokufanyia.rafiki yako alishindwa kukabiliana na mazingira ya hapo kazini kwenu,na inavyoonekana ni ofisi imejaa watu wa manenomaneno,wewe ndo ulipaswa uwe mwalimu na ndg kwake.labda nikuulize je Kama angelikuwa ni Kama,au mdogo wako,ungelikaa kimya!?? jibu ni hapana ,Basi hapo ndipo ulipokosea ndg yangu mleta mada.kukaa na kitu moyoni kinachokuumiza ni dhambi ,sawa na dhambi nyingine,pia ni unafiki sawa na unafiki mwingine.sorry kwa kutumia lugha Kali kidogo bt my hope u get me.
 
Back
Top Bottom