Msaada wa kimawazo

Msaada wa kimawazo

Habari yako mwana jf

Baba yangu alibahatika kuwa na mali nyingi sana na kwetu tumezaliwa wachache watu wa nne tu,

Sasa mzee ili kuondoka utata ameamua kugawa mali ingali yupo hai Mimi nimepata mgao wa nyumba ya kuishi pamoja na kiasi kama million 50

Kwa upane wa elimu nina degree ya agribusiness kutokea SUA
Pia binafsi sina background yoyote ya kufanya biashara maana mda mwingi nimetumia shuleni

Niliwaza hii pesa niiweke UTT baada ya kuisoma na kuifatilia Sana lakini changamoto inakuja nahofia usalama wa pesa yangu huko UTT hasa hasa kwenye nchi yetu hii ambayo kiongozi anaweza amua chochote mda wowote.

Naombeni ushauri je naweza anzia wapi katika uwekezaji.
Na je UTT ni salama mathalani kwa miaka 30 ijayo. Umri wangu ni miaka 25.

Pia ningeomba Kwa wenye kujua zaidi ni mkoa gani au eneo gani Tanzania ni zuri Kwa mtu mwenye mtaji kuanza biashara na biashara ipi inaweza kuwa na rejesho zuri.
Asanteni


Nunua trekta tu litakulipa
 
Ndio maana tunaomba mchango wa kimawazo mkuu
Ni kweli kabisa wakati mwamba Mimi napambana, ili nipate mtaji wa 4m Kuna mwingine ana 50m na anawaza Cha kufanya.

Okay weka UTT AMIS ni salama huko. Mkuu kupo poa mno. Kama unataka mwongozo zaidi ni PM nikupatie kitabu kinachohusu UTT upate mwongozo sahihi.
 
Nyumba ipo eneo lipi? Strategic Area?

Sasa angalia condition ya nyumba ikiwezekana ifanyie REHABILITATION then ipangishe. Kama mwanzo ilikuw unapata 300k kwa mwezi ukifanya REHABILITATION ya 20m una uwezo wa kupata 600k.

Kitu ambacho kwa UTT huwez pata hiyo hela (300k) per mwezk
Kwa 50m utt anapata Tena ni 300+ Kwa mwezi
 
Back
Top Bottom