Msaada wa Kisheria kuhusu mahusiano na Mwanafunzi

Mtendaji ndiye anayetaka kumfunga na sio wazazi
 
Shahidi anayeharibu ushahidi kwa makusudi ni kweli anaweza kukutwa na hatia na huyo shahidi ni pamoja na huyo mtendaji.

Kwani kesi ipo polisi au Mahakamani maana ni kama kuna stori mbili tofauti hapa.
Kesi ilianzia Polisi wazazi waliitwa maana ni karibu waliweza kufika, na ni tarehe 16 mwezi uliopita, Jana ndo amewatumia summons ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Akawasomea na kuondoka akiwataka leo wafike mahakamani. Leo asubuhi kafika nyumbani kuwachukua na pikipiki kwenda mahakamani hajawakuta ila kaenda shuleni kamchukua binti kaenda naye mahakamani.

Binafsi nikiangalia hii kesi sioni wazazi wakihusika ndiyo maana nikaja hapa kuomba kwenu mnaoijua sheria.
 
Kosa liko wapi?
 
Mkuu kosa la ubakaji ni lazma LITHIBITISHWE PASIPO KUACHA SHAKA YOYOTE.
Unadai kuwa mliwapiga picha je hizo picha mliwapiga wakiwa mazingira gani? Isijekua mmewakuta watu wamekaa chumbani nyie mnawapiga picha.
Halafu mnapolazmisha wazazi wakatoe ushahidi ni ushahidi gani mnaoutaka kama mzazi hauwepo eneo la tukio?
Waende mtendaji na waliokuwepo eneo la tukio pamoja na huyo mwanafunzi ndio wakatoe ushahidi kama ukiwa na mashiko mahakama itamkuta jamaa na hatia na kama hautakua na mashiko basi jamaa ataachiwa
 
Naam, kwanza mimi sikuwa eneo la tukio, Binti hajabakwa na hawakuwakuta wanafanya tendo na picha zilizopigwa wapo kitandani wamekaa. Ndiyo maana nikajaribu kuhusisha hii kesi na wazazi wake ambao hawakuusika kabisa mpaka taarifa zimepelekwa polisi, na baadae Mahakamani ni Mtendaji wa kata ndo anaratibu na kusimamia mpango mzima. Shida imekuja baada ya kuwalazimisha wazazi wakatoe ushaidi na hawajui chochote kilichotokea na wenyewe walihadithiwa.
 
Kwanza kabisa ni kesi ya aina gani imefunguliwa?, sababu hapo inapaswa kuwa kesi ya jinai. Na ikishakuwa hivyo kuna ofisi ya muendesha mashtaka wa serikali (NPS) hawa ndio wanaosema nani awe shahidi kwenye hizo kesi dhidi ya Jamhuri.

Polisi wao ni kukusanya ushahidi na kuandikisha maelezo na kupeleka faili NPS na kumpeleka mtuhumiwa Mahakamani siku ya kwanza baada ya hapo kazi yao imeisha.

Kesi za hivi zinazohusu makosa ya mahusiano na wanafunzi plus ubakaji yanaenda Mahakama ya wilaya au hakimu mkazi sasa nikuulize hiyo kesi ipo Mahakama gani?. Kama ipo Mahakama ya mwanzo jua ni magumashi hayo hapo wahuni wanatafuta kuwatoa hela.

Swali lingine muhimu, mtuhumiwa yupo wapi na ni nani mtuhumiwa kwenye hiyo kesi?.

Kuna jambo halijakaa sawa Mkuu.
 

Sio sawa kumpeleka uyo kijana jela uyo mtendaji mpuuzi tuu, apo mnapaswa kumdefend uyo kijana kupitia uyo binti maana binti akisema uyo mvulana ni alikua ni mtu wake wakaribu kwajil ya masomo tu na sivinginevyo sizani kama mahakama itapinga.
 
Kesipo mahakama ya Wilaya na kijana amewekwa mahabusu kwa mujibu wa taarifa ya mtendaji
 
Sio sawa kumpeleka uyo kijana jela uyo mtendaji mpuuzi tuu, apo mnapaswa kumdefend uyo kijana kupitia uyo binti maana binti akisema uyo mvulana ni alikua ni mtu wake wakaribu kwajil ya masomo tu na sivinginevyo sizani kama mahakama itapinga.
Huyu binti alitishiwa na kupangiwa maneno ya kuongea kipindi maelezo yannachukuliwa polisi na inasemekana kijana naye leo amekiri kwamba ni kweli alikamatwa kweli.

Binafsi kijana sijihusishi naye sana afungwe asifungwe ni sawa ila kulazimisha wazazi kutoa ushaidi na hawakuwa kwenye tukio ndo kinachonipa wasiwasi
 


  • Kuna Mimba?
  • Mmemfumania wakilalana?

Kama hakuna hayo hapo muachen kijana wa watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…