Msaada wa kumpata mtu aliyenitapeli

Unakutana na mtu mara ya kwanza, unamuamini, unampa laki tano kiurahisi halafu unalalamika kutapeliwa? Jifunze kutokana na makosa hayo. Pili kuepuka hasara zaidi hesabu hiyo kama sadaka na Mshukuru Mungu kwa yote.
 
Polisi wetu uwajui Wewe, Huyo tapeli wanaweza wakampata na wasikuambie kua wamempata wakamkamua pesa na wakamuachia, kila ukifuatilia unaambiwa hajapatikana anafuatiliwa na wameshakukamua pesa hasara juu ya hasara
Pessimists have never been at the top of their game! Poor soul! This thing is 100% possible. Acheni kudhani kila askari wa jeshi la polisi ni mkosa-maadili. Overgeneralization is what kills your intelligence.
 
Very good advice. Kuna watu wengi sana wanakamatwa kila siku. Unatakiwa kukubalia kufuatilia100%, uwapatie ushirikiano na uwe mvumilivu pia. It takes time and some resources. I strongly advice him to move forward, atakuja kutupatia mrejesho wa mafanikio soon.

Kama anajiweza kifedha, afanye multiple tracking. Asitegemee sehemu moja tu ya ufuatiliaji. Haiwezi kuchukua zaidi ya wiki mbili, mtuhumiwa anakuwa ametiwa chini ya vyombo vya usalama.
 
Multiple tracking ndo nini mkuu
 
Very good point
 
Unakutana na mtu mara ya kwanza, unamuamini, unampa laki tano kiurahisi halafu unalalamika kutapeliwa? Jifunze kutokana na makosa hayo. Pili kuepuka hasara zaidi hesabu hiyo kama sadaka na Mshukuru Mungu kwa yote.
Mkuu sikufichi hakuna anayejua ya mbele, na wakati tatizo hili linapotaka kutokea au unapokuwa na tapeli kuna roho inakwambia kwamba huyu ni tapeli ila kuna nyingine inakuwa inataka kupingana nayo, yani roho zinakuwa 50% kwa 50% hivyo unashindwa kujua kwamba ipi inakwambia ukweli, kikubwa nilichochukuliwa ni mzigo una thaman ya laki 5, alinipigia simu nimpelekee yuko sinza kufika nikamkuta ofisini kwa mazingira anayoyatengeneza huyo mtu ni kujifanya kama anauzoefu sana na anajuana ama ni mwenyeji wa hapo ofisini nilivyokutana naye tukafanya mazungumzo mzigo ikabidi tuuhifadhi hapo ofisini ili twende tukachukue ela, tukatoka kama meter 300 na hapo ofisini tukafika mpk benk akaingia sehem ndani ya hyo bank akasema nimsubiri, machale yakanicheza wakat anaingia tu hyo sehem me nikasema nirudi nikauwai mzigo yawezekana huyu ni tapeli sababu kwann anaagiza mzigo na pesa hajajipanga , nikatoka haraka sana kwenda kuuwai mzigo, kumbe yeye alijipanga alivyotoka tu mlango mwingine alikuwa na pikpik akaenda kuchukua mzigo na piki piki kilichonifanya niukose ni kwamba mimi nilikuwa natembea sababu meter 300 sio mbali, kufika naambiwa kaondoka sasahv na pikipiki na hawamfahamu ila tu alionesha kuwachangamkia pale ofisini mpk wakawa wanamshangaa..... ndo nilikosa mzigo kwa namba hiyo
 
Nitakuona wa maana kama utamchangia mdau pesa isiyopunguwa laki mbili kwa ajili ya follow up ili muweze kuukamata huo mtandao na siyo unabwabwaja tu kama huna meno.
 
Duu mkuu pole sana asee maisha tu haya mkuu yatapita😞😞
 
Multiple tracking ndo nini mkuu
Anakupotezea muda wako tu bure, hana huruma na wewe, anataka uendelee kugawa pesa usawa huu wakati hizo line za kutapelia zikishatumika wanaflush chooni.

Wanaochonga line za kutapelia ni freelancer wa mitaani.
 
Sijaelewa Chief,ni Bank gani hiyo aliyoingia pale Sinza??BOA Bank au??na ina mlango mwingine wa kutokea au??mlipoondoka dukani kwenda Bank mlienda kwa Pikipiki au mlitembea kwa miguu??
 
Mbona haujaeleza alikutapeli vipi tuone ni uzembe umefanya au jamaa katumia akili nyingi
 
Sijaelewa Chief,ni Bank gani hiyo aliyoingia pale Sinza??BOA Bank au??na ina mlango mwingine wa kutokea au??mlipoondoka dukani kwenda Bank mlienda kwa Pikipiki au mlitembea kwa miguu??
kesi ya aliyetapeliwa gari imeishiaje, ume conclude vipi, em mwagika kule uzini tupate hatma kama mtoa mada alizingua au vipi
 
NIliwahi kutapeliwa kama wewe mkuu na nikamkamata mwizi wangu. Alinipiga laki 2.4 nikiwa High School kwa njia ya mtandao na nilimuona mara moja tu na sikuwa na simu wala namba yake.

ilikuwa mwezi wa 10 tukiwa tunafungua shule, nilienda central (mwanza hapa) nikafungua RB nikaenda shule.

Hio hela nilipigwa kwa njia ya Nmb Mobile. (Nilienda shule nikiwa na masikitiko makubwa sana) .. yani mtu nilietaka kumsaidia kwa moyo.moja ndio kaniumiza aisee.

nakumbuka nilipofika Bukoba kesho yake asubuhi tu niliwahi Voda shop nika renew line yangu.maana alibaki nayo yule tapeli.

Baada ya ku renew ikakaa siku 3 ikasaidia kurudisha muamala uliotolewa kwa NMB MOBILE. LAKI 2 IKARUDI.

hio hela ilini surprise sana mpaka nikatoroka kwenda benki kuomba ufafanuzi, wakanipa bamk statement ndio nikaona namba ya simu nyingine iliyotumiwa hela kutoka kwangu

Baada ya.miezi mitano tulipofunga shule, nilirudi central (tena nikiwa nimepoteza RB), Nikawakumbusha tarehe na mwezi nilipofungua malalamiko yangu, wakanipa rb No na wakanipangia mpelelezi.

Bahati nzuri nikakutana na Afande ambae ni mtu wa nyumbai kabisa huko nilikotoka.

Huwezi amini ile namba iliyofanya uhalifu, mwenyewe alishikwa ndani ya siku 3 tu!! Kumbuka enzi hizo hakukuwa na mambo ya NIDA (Miaka 10 sasa imepita).

matapeli wengi hawatumii namba zao za simu halisi. Tegemea kumkamata mtu ambae si sahihi twna asie na uwezo wa kukulipa hata mia.mbovu

sitakaa nimsahau huyu afande..
 
nilipata simu lakini baada ya kutumia laki na nusu kwa afande aliyenisaidia. nilimuahidi dau mapema
 
Ila sasa si kuna mambo ya nida pia kwa sasa pia niombee Mungu kwamba awe na number ambazo alijaribu kuwasiliana nao ndo utakuwa unafuu kwangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…