Msaada wa kumpata mtu aliyenitapeli

Ila sasa si kuna mambo ya nida pia kwa sasa pia niombee Mungu kwamba awe na number ambazo alijaribu kuwasiliana nao ndo utakuwa unafuu kwangu
Hakuna tapeli anayetumia namba yake aliyosajili kwa ID yake.

Ingekuwa ni hivyo basi wale matapeli wanaopigia watu simu na kujifanya ni Tigo customer care wasingekuwepo.

Mimi huwa haipiti mwezi lazima wanipigie kwa namba tofauti nimeripoti tigo mpaka sasa nimechoka, wakinipigia wanakoga matusi ya kutosha na wao wanarudishia matusi halafu unawauliza wewe ndio customer care? Mimi mwenyewe natafuta mtu wa kumtapeli saa hizi.
 
Pole Sana ...chukulia Kama funzo na songa mbele utapata zaidi

Kama kumpata kwakua ushafungu kesi Basi tulia tu siku bahati ikiwa upande wako utamdaka naturally Ila usiweke akili kwenye kumtafuta utapoteza zaidi ya hapo na utajuta zaidi.
 
Pole sana. Mimi kawaida yangu simuamini mtu ambaye simfahamu kabisa na kibaya zaidi anaonekana kunichangamkia ghafla.
 
Ila sasa si kuna mambo ya nida pia kwa sasa pia niombee Mungu kwamba awe na number ambazo alijaribu kuwasiliana nao ndo utakuwa unafuu kwangu
Hio namba angalia mapema imesajiliwa kwa majina yapi maana usajili huwa unafutwa baada ya siku 2-3
 
Ila sasa si kuna mambo ya nida pia kwa sasa pia niombee Mungu kwamba awe na number ambazo alijaribu kuwasiliana nao ndo utakuwa unafuu kwangu
Exactly.... Zile recent communication ndo zitakusaidia. ... Gharama ya kutrace kwa police ni Kama 50000 hivi. ...mi nishawahi kutrace simu yangu kwa njia ya IMEI , na nikaipata ...kikubwa upate Askari mwenye ako na ubinadamu tu
 
Yan katika vitu ambavyo watu wengine wanakosea ni kumuamini mtu usiyemfahamu,,,na mpaka unampa hela dah na wengine utakuta kakutana na mtu mara 2 bar kashakua rafiki yake na nyumbani anamkaribisha,Acha huyo uliyekutana nae njiani Hata mtu unayefanya nae kazi ofisi moja tu hutakiwi kumuamini,jiamini mwenyew you won’t hurt yourself!!!
 
Pole sana. Mimi kawaida yangu simuamini mtu ambaye simfahamu kabisa na kibaya zaidi anaonekana kunichangamkia ghafla.
Hii siyo sehemu ya mjadala. Tunafokasi kumshauri mhanga nini afanye. Akili huna? Who solicited for your troubles even?
 
Exactly.... Zile recent communication ndo zitakusaidia. ... Gharama ya kutrace kwa police ni Kama 50000 hivi. ...mi nishawahi kutrace simu yangu kwa njia ya IMEI , na nikaipata ...kikubwa upate Askari mwenye ako na ubinadamu tu
This is really helpful for him.
 
Unataka uendelee kutapeliwa tena? huyo hatapatikana,labda kama ungesema alikuwa na Bunduki,basi polisi wangempata kwa sababu ya hiyo silaha.ila laki 5 yako siyo kitu kikubwa sana.unaweza kuombwa za mafuta ndogo ndogo mpaka ikafika laki 4 zingine.so ukiipata hiyo lak 5 inakuwa na thamani ya laki 1
 
Sasa mkuu si useme umetapeliwaje ili na wengine wajue huo mtego.
 
Mkuu hapo andika maumivu tu.
Labda hiyo namba abaki nayo kwenye simu (kwa kuwa amekupiga hatoathirika kuidamp, chip ya Tzs 2000 - 5000) ukilinganisha chenchi alizokwapua kwako.Halafu hivi kusajili kwa NIDA kuna faida gani ikiwa kila siku watu wanalizwa?!!!🙄
 
Wakati unaendelea na mchakato wa kumtafuta mbaya wako, basi ungetusimulia na sisi namna ulivyo tapeliwa! Ili na sisi Watanzania wenzako tupate somo.

Maana kuna kila dalili huo utapeli ulikuwa siyo wa kitoto! Kukutana na mtu usiye mfahamu na kumkabidhi kitita cha laki 5 ndani ya huu mwezi mgumi wa January! Haikuwa rahisi bila shaka.
 
Hiyo ni kweli aisee, Mie mwenyewe mwaka jana niliibiwa smartphone, nilvoenda polis nikakamuliwa 60,000 alafu baada ya hapo kila nikiulizia naambiwa mwizi hajawahi kupatikana, kwamba hajahi kuingiza cm hewani, huu ni uwongo mwizi gani wa kuiba cm alafu aishie kutunza ndani? najutia kwenda polis maana niliingia hasara zaidi!
nashauri serikali ingeruhusu wananchi kujitafutia cm wao wenyewe pindi wanapoibiwa wakishampata mwizi ndipo polis wataarifiwe! Huu utaratiu wa sasa unatoa mwanya kwa polis kupiga pesa bnadala ya kutoa msaada!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…