Msaada wa kumpata mtu aliyenitapeli

Msaada wa kumpata mtu aliyenitapeli

Ila sasa si kuna mambo ya nida pia kwa sasa pia niombee Mungu kwamba awe na number ambazo alijaribu kuwasiliana nao ndo utakuwa unafuu kwangu
Hakuna tapeli anayetumia namba yake aliyosajili kwa ID yake.

Ingekuwa ni hivyo basi wale matapeli wanaopigia watu simu na kujifanya ni Tigo customer care wasingekuwepo.

Mimi huwa haipiti mwezi lazima wanipigie kwa namba tofauti nimeripoti tigo mpaka sasa nimechoka, wakinipigia wanakoga matusi ya kutosha na wao wanarudishia matusi halafu unawauliza wewe ndio customer care? Mimi mwenyewe natafuta mtu wa kumtapeli saa hizi.
 
Habari wakuu pia poleni kwa majukumu na migangaiko ya kila siku.

Dhumuni la kuleta uzi huu ni kwamba siku ya juzi Jumapili, niliweza kutapeliwa pesa na mtu ambaye nilikutana naye kwa ajili ya biashara ndipo aliweza kunitapeli karibu laki 5 taslim, kwa sura huyo mtu namfahamu na ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kukutana naye na kuna number alitumia kunitafuta ambayo iliweza kupatikana hiyo juzi na jana ila leo haipatikani, kesi ya huyo mtu iko central police

SWALI JE.
Huyo mtu anaweza kupatikana kwa kupitia hiyo namba ya simu kana kwamba juzi na jana ilikuwa hewani ila leo haipatikani?

Nimefuatilia Polisi wamesema wako kwenye utaratibu wa kufuatilia hiyo number. Na kuna gharama za kutoa kwenye ishu kama hiyo .

Swali je?

KUNA ALIYEWAI KUMPATA MTU AMA MTUHUMIWA WAKE KWA KUPITIA NUMBER YA SIMU?

MWENYE experience naomba aweze kunieleza kama alifanikiwa na ilikuwaje?
Pole Sana ...chukulia Kama funzo na songa mbele utapata zaidi

Kama kumpata kwakua ushafungu kesi Basi tulia tu siku bahati ikiwa upande wako utamdaka naturally Ila usiweke akili kwenye kumtafuta utapoteza zaidi ya hapo na utajuta zaidi.
 
Mkuu sikufichi hakuna anayejua ya mbele, na wakati tatizo hili linapotaka kutokea au unapokuwa na tapeli kuna roho inakwambia kwamba huyu ni tapeli ila kuna nyingine inakuwa inataka kupingana nayo, yani roho zinakuwa 50% kwa 50% hivyo unashindwa kujua kwamba ipi inakwambia ukweli, kikubwa nilichochukuliwa ni mzigo una thaman ya laki 5, alinipigia simu nimpelekee yuko sinza kufika nikamkuta ofisini kwa mazingira anayoyatengeneza huyo mtu ni kujifanya kama anauzoefu sana na anajuana ama ni mwenyeji wa hapo ofisini nilivyokutana naye tukafanya mazungumzo mzigo ikabidi tuuhifadhi hapo ofisini ili twende tukachukue ela, tukatoka kama meter 300 na hapo ofisini tukafika mpk benk akaingia sehem ndani ya hyo bank akasema nimsubiri, machale yakanicheza wakat anaingia tu hyo sehem me nikasema nirudi nikauwai mzigo yawezekana huyu ni tapeli sababu kwann anaagiza mzigo na pesa hajajipanga , nikatoka haraka sana kwenda kuuwai mzigo, kumbe yeye alijipanga alivyotoka tu mlango mwingine alikuwa na pikpik akaenda kuchukua mzigo na piki piki kilichonifanya niukose ni kwamba mimi nilikuwa natembea sababu meter 300 sio mbali, kufika naambiwa kaondoka sasahv na pikipiki na hawamfahamu ila tu alionesha kuwachangamkia pale ofisini mpk wakawa wanamshangaa..... ndo nilikosa mzigo kwa namba hiyo
Pole sana. Mimi kawaida yangu simuamini mtu ambaye simfahamu kabisa na kibaya zaidi anaonekana kunichangamkia ghafla.
 
Ila sasa si kuna mambo ya nida pia kwa sasa pia niombee Mungu kwamba awe na number ambazo alijaribu kuwasiliana nao ndo utakuwa unafuu kwangu
Hio namba angalia mapema imesajiliwa kwa majina yapi maana usajili huwa unafutwa baada ya siku 2-3
 
Ila sasa si kuna mambo ya nida pia kwa sasa pia niombee Mungu kwamba awe na number ambazo alijaribu kuwasiliana nao ndo utakuwa unafuu kwangu
Exactly.... Zile recent communication ndo zitakusaidia. ... Gharama ya kutrace kwa police ni Kama 50000 hivi. ...mi nishawahi kutrace simu yangu kwa njia ya IMEI , na nikaipata ...kikubwa upate Askari mwenye ako na ubinadamu tu
 
Yan katika vitu ambavyo watu wengine wanakosea ni kumuamini mtu usiyemfahamu,,,na mpaka unampa hela dah na wengine utakuta kakutana na mtu mara 2 bar kashakua rafiki yake na nyumbani anamkaribisha,Acha huyo uliyekutana nae njiani Hata mtu unayefanya nae kazi ofisi moja tu hutakiwi kumuamini,jiamini mwenyew you won’t hurt yourself!!!
 
Pole sana. Mimi kawaida yangu simuamini mtu ambaye simfahamu kabisa na kibaya zaidi anaonekana kunichangamkia ghafla.
Hii siyo sehemu ya mjadala. Tunafokasi kumshauri mhanga nini afanye. Akili huna? Who solicited for your troubles even?
 
Exactly.... Zile recent communication ndo zitakusaidia. ... Gharama ya kutrace kwa police ni Kama 50000 hivi. ...mi nishawahi kutrace simu yangu kwa njia ya IMEI , na nikaipata ...kikubwa upate Askari mwenye ako na ubinadamu tu
This is really helpful for him.
 
Habari wakuu pia poleni kwa majukumu na migangaiko ya kila siku.

Dhumuni la kuleta uzi huu ni kwamba siku ya juzi Jumapili, niliweza kutapeliwa pesa na mtu ambaye nilikutana naye kwa ajili ya biashara ndipo aliweza kunitapeli karibu laki 5 taslim, kwa sura huyo mtu namfahamu na ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kukutana naye na kuna number alitumia kunitafuta ambayo iliweza kupatikana hiyo juzi na jana ila leo haipatikani, kesi ya huyo mtu iko central police

SWALI JE.
Huyo mtu anaweza kupatikana kwa kupitia hiyo namba ya simu kana kwamba juzi na jana ilikuwa hewani ila leo haipatikani?

Nimefuatilia Polisi wamesema wako kwenye utaratibu wa kufuatilia hiyo number. Na kuna gharama za kutoa kwenye ishu kama hiyo .

Swali je?

KUNA ALIYEWAI KUMPATA MTU AMA MTUHUMIWA WAKE KWA KUPITIA NUMBER YA SIMU?

MWENYE experience naomba aweze kunieleza kama alifanikiwa na ilikuwaje?
Unataka uendelee kutapeliwa tena? huyo hatapatikana,labda kama ungesema alikuwa na Bunduki,basi polisi wangempata kwa sababu ya hiyo silaha.ila laki 5 yako siyo kitu kikubwa sana.unaweza kuombwa za mafuta ndogo ndogo mpaka ikafika laki 4 zingine.so ukiipata hiyo lak 5 inakuwa na thamani ya laki 1
 
Sasa mkuu si useme umetapeliwaje ili na wengine wajue huo mtego.
 
Labda loss report🤣
1643102934437.png
 
Mkuu hapo andika maumivu tu.
Labda hiyo namba abaki nayo kwenye simu (kwa kuwa amekupiga hatoathirika kuidamp, chip ya Tzs 2000 - 5000) ukilinganisha chenchi alizokwapua kwako.Halafu hivi kusajili kwa NIDA kuna faida gani ikiwa kila siku watu wanalizwa?!!!🙄
 
Habari wakuu pia poleni kwa majukumu na migangaiko ya kila siku.

Dhumuni la kuleta uzi huu ni kwamba siku ya juzi Jumapili, niliweza kutapeliwa pesa na mtu ambaye nilikutana naye kwa ajili ya biashara ndipo aliweza kunitapeli karibu laki 5 taslim, kwa sura huyo mtu namfahamu na ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kukutana naye na kuna number alitumia kunitafuta ambayo iliweza kupatikana hiyo juzi na jana ila leo haipatikani, kesi ya huyo mtu iko central police

SWALI JE.
Huyo mtu anaweza kupatikana kwa kupitia hiyo namba ya simu kana kwamba juzi na jana ilikuwa hewani ila leo haipatikani?

Nimefuatilia Polisi wamesema wako kwenye utaratibu wa kufuatilia hiyo number. Na kuna gharama za kutoa kwenye ishu kama hiyo .

Swali je?

KUNA ALIYEWAI KUMPATA MTU AMA MTUHUMIWA WAKE KWA KUPITIA NUMBER YA SIMU?

MWENYE experience naomba aweze kunieleza kama alifanikiwa na ilikuwaje?
Wakati unaendelea na mchakato wa kumtafuta mbaya wako, basi ungetusimulia na sisi namna ulivyo tapeliwa! Ili na sisi Watanzania wenzako tupate somo.

Maana kuna kila dalili huo utapeli ulikuwa siyo wa kitoto! Kukutana na mtu usiye mfahamu na kumkabidhi kitita cha laki 5 ndani ya huu mwezi mgumi wa January! Haikuwa rahisi bila shaka.
 
Hiyo ni kweli aisee, Mie mwenyewe mwaka jana niliibiwa smartphone, nilvoenda polis nikakamuliwa 60,000 alafu baada ya hapo kila nikiulizia naambiwa mwizi hajawahi kupatikana, kwamba hajahi kuingiza cm hewani, huu ni uwongo mwizi gani wa kuiba cm alafu aishie kutunza ndani? najutia kwenda polis maana niliingia hasara zaidi!
nashauri serikali ingeruhusu wananchi kujitafutia cm wao wenyewe pindi wanapoibiwa wakishampata mwizi ndipo polis wataarifiwe! Huu utaratiu wa sasa unatoa mwanya kwa polis kupiga pesa bnadala ya kutoa msaada!
 
Back
Top Bottom