Namora
JF-Expert Member
- May 2, 2020
- 410
- 1,014
Wakuu naombeni mwongozo wenu tafadhali, nilikua nafatilia pasi ya kusafiria (International Passport) kidogo nimekumbsna na vikwazo. Mimi niko mkoani huku (Chuganian)
Nimejaribu kuulizia uhamiaji wa hapa nimeelezwa niwe na:
Barua ya Serikali za mtaa na barua yangu ya kuomba passport ni Muhimu au ni huku tu wa mkoani ndio tunaambiwa hivyo??
Kama ni lazima niandike barua ya kuomba, je inakuwa katika lugha gani??? Na mfumo wa uandishi wake upoje??
Kwenye site ya uhamiaji wanasema uwe na ushahidi wa safari au ushahidi wa Shughuli anayofanya mwombaji. Je ushahidi huo ni upi?? Na unapatikanaje?
Kama kuna waliowahi kupata passport kutokea huku mkoani nilipo basi naombeni uzoefu wenu tafadhali.
Nawasilisha
...
UPDATE
Nimefanikiwa kuipata nikiwa huku huku mkoani kwa muda wa siku 21. Mungu mwema
Maelezo haya ya mkuu Mosha yapo sahihi kwa 99%
Nimejaribu kuulizia uhamiaji wa hapa nimeelezwa niwe na:
- Cheti cha kuzaliwa (Ninacho)
- Namba za Nida (ninazo)
- Cheti cha kuzaliwa mzazi (Ninacho cha baba)
- Barua ya Serikali ya mtaa
- Barua mimi ya maombi ya Passport kwenda kwa afisa uhamiaji mkoa
Barua ya Serikali za mtaa na barua yangu ya kuomba passport ni Muhimu au ni huku tu wa mkoani ndio tunaambiwa hivyo??
Kama ni lazima niandike barua ya kuomba, je inakuwa katika lugha gani??? Na mfumo wa uandishi wake upoje??
Kwenye site ya uhamiaji wanasema uwe na ushahidi wa safari au ushahidi wa Shughuli anayofanya mwombaji. Je ushahidi huo ni upi?? Na unapatikanaje?
Kama kuna waliowahi kupata passport kutokea huku mkoani nilipo basi naombeni uzoefu wenu tafadhali.
Nawasilisha
...
UPDATE
Nimefanikiwa kuipata nikiwa huku huku mkoani kwa muda wa siku 21. Mungu mwema
Maelezo haya ya mkuu Mosha yapo sahihi kwa 99%
Ili kupata passport, unatakiwa uwe na.
1. Cheti cha kuzaliwa.
2. Cheti cha kuzaliwa cha mzazi mojawapo.
3. Kitambulisho cha Taifa.
4. Kitambulisho cha Kazi Kwa watumishi wa umma au barua ya utambulisho KUTOKA Serikali za mitaa Kama hujaajiriwa.
5. Barua ya maombi ya passport kama uko mkoani anapitisha kwa kamishna WA mkoa kwenda Kwa kamishna mkuu, anwani zao za posta unaweza kuzipata ofisini kwao.
6. Uthibitisho wa safari ukionyesha nchi unayokwenda.
7. Baada ya kuwa na vielelezo vyote utaanza kujaza form ya maombi online kupitia uhamiaji portal, kuna sehemu uta upload barua ya utambulisho na Cheti cha kuzaliwa.
Kama ombi limekamilika utapewa contral namba ya kulipia 20,000 ili uweze Ku print form.
Ukishaprint form utatafuta mashaidi waijaze na pia mwanasheria.
8. Baada ya hapo utaenda ofisi za uhamiaji ukiwa na hiyo form na vielelezo nilivyotaja hapo juu,
9. Ombi litapitiwa kama hakuna dosari, litapitishwa, utalipia 130,000 Kwa kutumia control namba, halafu utakamilisha ombi Kwa kupiga picha pamoja na kuchukuliwa alama za vidole.
10. Baada ya hapo utasubiri Kwa mwezi mmoja passport kuwa tayari.
11. Kama unahihitaji Kwa haraka na hauna baadhi ya vielelezo unaweza watumia vishoka, Ila utawalipa gharama za ziada almost 100-200k.