Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
Wakuu naombeni mwongozo wenu tafadhali, nilikua nafatilia pasi ya kusafiria (International Passport) kidogo nimekumbsna na vikwazo. Mimi niko mkoani huku (Chuganian)
Nimejaribu kuulizia uhamiaji wa hapa nimeelezwa niwe na..
Wamesema pia Nikishakamilisha vitu vitatumwa Dar ambapo itachukua kama mwezi hivi hadi kupata passport sasa naomba kuuliza kwq mliofuatilia passport kipindi cha hivi karibuni.
- Cheti cha kuzaliwa (Ninacho)
- Namba za Nida (ninazo)
- Cheti cha kuzaliwa mzazi (Ninacho cha baba)
- Barua ya Serikali ya mtaa
- Barua mimi ya maombi ya Passport kwenda kwa afisa uhamiaji mkoa
[emoji117]Barua ya Serikali za mtaa na baraua yangu ya kuomba passport ni Muhimu au ni huku tu wa mkoani ndio tunaambiwa hivo????
Kama ni lazima niandike barua ya kuomba he inakua katika lugha gani??? Na mfumo wa uandishi wake upoje????
Kwenye site ya uhamiaji wanasema uwe na ushahidi wa safari au ushahidi wa Shughuli anayofanya mwombaji. Je ushahidi huo ni upi?? Na unapatikanaje???
Kama kuna waliowahi kupata passport kutokea huku mkoani nilipo basi naombeni uzoefu wenu tafadhali.
Nawasilisha
Kwenye uzia penyeza rupia mkuu.
Wewe unasubiri mwezi mzima, funga safari njoo Dar ndani ya masaa 4 biashara imekwisha