Utumishi wenyewe wanasoma Jamiiforums. Mkipatia maswali mkiotea maswali humu wanayasoma kisha wanachukua pepa B. We jisomee. Hakuna kitu kipya ni yale yale ya shuleni na yanayoendelea ktk jamii. Tatizo la kukoswa maarifa ni kwamba wengi baafa ya kumaliza masomo hawafuatili mambo waliyoyasoma katika uhalisia wake kimatumizi.
Mfano, taarifa za habari, vikao vya bunge, DIRA ya maendeleo ya nchi n.k vijana wengi hawana habari navyo. Wako bussy na mpira na betting. Mfano ukimuuliza kijana aliyesoma planning ni vitu gani vya kuzingatia unapoandaa mpango mkakati haujui, vipaumbele vya taifa ktk DIRA ya maendeleo, holla!