Msaada wa mawazo juu ya biashara ya photo studio & photo printing services

bwegebwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2010
Posts
1,072
Reaction score
186
Wana JF;
Sisi tuna-own Kampuni inayojshughulisha na Secretarial Services, Printing (Cards, Posters, Business Cards, Invitation Cards, Fliers etc). Tunazamia ku-expand business ili tufungue small Photo studio yenye uwezo ku kupiga passport sizes na picha nyinginezo pamoja na kusafisha (Digital Printing Services) kwa muda mfupi (Express Services)

Kama kuna mtu mwenye ujuzi/ufahamu kuhusu mashine nzuri za kudevelop na kuprint photos anipe specifications na kama inawezekana namna gani naweza kuzipata!

Kuna aliyenieleza kuhusu KODAK PHOTO KIOSK, lakini siifahamu na sijui inafanyaje kazi, kwa maana hiyo nahitaji ushauri mashine hizi (na nyinginezo) na pia kwa ujumla ni ipi muhimu kuanza nayo kwa small- medium size business.
Mwenye ideas ini-PM au anijibu kwenye post hii. Nakaribisha pia mtu mwenye nia ya kufanya biashara hii kwa UBIA
Ahsanteni

SIMILAR CASES
===============


============================================================

MAWAZO MBALIMBALI YA WADAU



 
Hello!
Ninafanya research nahitaji kuanzisha biashara ya kuendesha photo studio nje ya mkoa wa dar es salaam,kwani nimegundua kuwa eneo ninalotaka kuanzisha biashara hiyo lina wateja wengi lakini studio hazizidi 5 na huduma zao ni za kubabaisha na hazina ubora.tatizo ni kwamba sina taarifa za kutosha juu ya hii biashara.nahitaji kujua
1.printer bora zinzoweza kusafisha picha za digital na zile za kawaida za film
2.aina bora ya kamera
3.vifaa vinavyohitajika ndani ya studio
4.software(kama zipo) ambazo zitasaidia kutoa picha zenye ubora,ii niweze kumudu ushindani wa biashara
5.karatasi zinazotumika kusafia picha zinaitwaje na zinapatikana wapi na bei gani.
6.mengineyo(taarifa zozote za ziada zinazoweza kunisaidia kuboresha au kufanikisha hili)
natanguliza shukrani wadau!!asanteni sana na mungu awabariki
 
wadau msaada wenu bado ninauhitaji,tafadhali naomba msaada wa mawazo na muongozo wenu
 
Biashara ya Studio ya picha inahitaji uwe na yafuatayo:
1. Ufahamu wa picha
2. Mtaji mkubwa. kuanzia USD 10,000 na kuedelea.
3. Technical knowhow ili usidanganywe kirahisi.
4. Sehemu nzuri ya biashara hiyo. Pasiwe na ushindani usio na maana.
Je unavyo hivyo?
 
Utasafisha na negative pia au? Dar zipo printa unachomeka memory card ,unachagua picha,unaprint hapo hapo una aja ya computer.ila ukiwa na computer unaitaji kuwa na software kama vile adobe photoshop kwa ajiri ya manjonjo.kamera yeyote yenye megapixel nyingi ni poa. Bajeti uwe kama na 2 million au 3.vifaa vyote vipo Dar
 
@chipukizi,asante mdau,mtaji si tatizo kwangu.yes nitasafisha na negative pia...please let me know jina la hizo printer,kuna mdau hapa amenisaidia kupata adobe photo shop,nashukuru sana
 
@nguvu moja,asante mdau katika ulivyotaja hapo juu,hyo namba 3 ndio ina upungufu kidogo,nina uelewa japo sio mkubwa,nafikiria kuajiri mtaalamu wa masuala ya picha kwa muda ili niweze kujifunza kupitia kwake.
 
bwegebwege unaweza kutoa update ulipofikia na idea yako?
 
biashara ipo sehemu gani , ninayo idea kiasi fulani ktk masuala ya picha .pia niko interested na kuwa mbia
 
hiyo biashara inalipa sana kutoka na eneo k=ukifanikiwa hili ndio utanunua mashine kubwa
 

Attachments

  • 321-565.jpg
    20.2 KB · Views: 872
hiyo mashine nimeiona south Africa, bei yake ipo kwenye USD 10,000
 
Nataka kufungua ka studio ka kupiga passport size pictures nahitaji vitu gani,camera gani,na kitu gani cha kusafishia picha,na ni brand gani inafaa na bei zake?nitashukuru kwa ushauri wenu
 
Nataka kufungua ka studio ka kupiga passport size pictures nahitaji vitu gani,camera gani,na kitu gani cha kusafishia picha,na ni brand gani inafaa na bei zake?nitashukuru kwa ushauri wenu

Ah kaka mbona hivyo vifaa unavyouliza unaviuza mwenyewe,nenda pale Mlimani City kuna studio waombe wafanyakazi wa hiyo studio watwakwambia vitu vya kununua.Vipo vyabei kubwa na ndogo muhimu ni uwe na camera na fast lens,soft box ,reflector,flash na kitambaa cha nyuma,kwa camera canon 7d kwa kuanzia ni poa na lens unaweza anzia hizi za Canon EF-S lakini kama una mkwanja nunua za EF na full frame camera moja kama vile canon 6d au 5D2or 3.Camera na lens zake ni vifaa aghali sana ,yataka moyo.Hizo printer nafikiri unazijua vizuri kwa kuwa unauza mwenyewe.Kwenye lens na camera naona nikon wapo bei poa kulinganisha na Canon.Pia hapo kenya kuna maduka ya camera na vifaa vyake wanauza bei si ghali sana,check FB wanaitwa Snap Shot na Kenya camera kama sijakosea
 
Nashukuru kwa majibu yako,kwa ukweli sio vyangu ni mtu kaniuliza ni hajui ni vitu gani anahitaji,ila yeye anataka vya budget ndogo unaweza ukanipa zaidi,maana sidhani ni mtu anayeweza kununua 7D si unajua bei zake,asante kwa ushauri
 
Nashukuru kwa majibu yako,kwa ukweli sio vyangu ni mtu kaniuliza ni hajui ni vitu gani anahitaji,ila yeye anataka vya budget ndogo unaweza ukanipa zaidi,maana sidhani ni mtu anayeweza kununua 7D si unajua bei zake,asante kwa ushauri

Mimi nitashauri kama anatumia Canon angenunua Canon zile ulizokuwa unauza kama ile Canon 400D uliyoiuza na lens zake kwani kwa ile bei ni afadhali aingenunua hiyo kuliko Point and Shoot ambazo bei yake ni karibu na hiyo .Nimeona huku uswahilini wengi hutumia Point and Shoot hasa kwa ajili ya kupiga passport size photos na pia hununua zile printer zake kama za pixer kwa laki 200000 na kitambaa .Nafikiri anaweza anzia hapo na akaendelea kidogo kidogo.
 
Naona mnajitangaza biadhata kwa namna ya majibiziano hakuna ishu ya studio hapa mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…