Mimi nitashauri kama anatumia Canon angenunua Canon zile ulizokuwa unauza kama ile Canon 400D uliyoiuza na lens zake kwani kwa ile bei ni afadhali aingenunua hiyo kuliko Point and Shoot ambazo bei yake ni karibu na hiyo .Nimeona huku uswahilini wengi hutumia Point and Shoot hasa kwa ajili ya kupiga passport size photos na pia hununua zile printer zake kama za pixer kwa laki 200000 na kitambaa .Nafikiri anaweza anzia hapo na akaendelea kidogo kidogo.
wabongo bwana tuna matatizo kweli,ni mtu kweli ana shida ya kununua vitu,alitaka mawazoNaona mnajitangaza biadhata kwa namna ya majibiziano hakuna ishu ya studio hapa mzee
...laki 200000... = 20,000,000,000
Nashukuru sana mkuu kwa ushauri wako ntaufanyia kazi vema,Kwenye mitandao ni sawa ila usisite kufikiria kuwa mpiga picha wa kujitegemea kwenye maharusi na shughuli mbalimbali maana matukio hayo ni mengi ni wewe tu kuijitangaza pamoja na kazi zako..Kazi ianze..
Nimekupata vyema mkuu asante sana,Kwasasa kupiga picha tu haitoshi. Inakupidi uongeze na kitu cha ziada, ambacho ni Graphics design.
Eidha ujue kutumia Adobe photoshop au software zinazohusu picha.
Watu wengi kwasasa wana camera nzuri na simu zenye uwezo mkubwa wa camera. Inabidi uwe na kitu cha ziada kuwakamata hawa watu. Picha zako ziwe tofauti na wao wanavyopiga.
Asante!
Mkuu hongera sana.. Tafuta camera nzuri kama Nikon nk usitumie camera ya simu au tablet inapunguza reputation yako kwa anayekutazama au kwa mteja, nenda na class kidogo, utapata mbinu nyingi na tofautitoufati, pia usideal na picha za watu pekee angalia na upande kama wanyama nk..tembelea huko mbugani, ndege, Maua nkHabari Wakuu, kiukweli huwa navutiwa sana na kazi hii ya kupiga picha na nadhani nina kipaji hiki kwa kuwa nawapiga watu picha nzuri sana hadi wanapenda hivyo natamani kuifanya kazi hii kama fursa ya biashara ambayo inaweza kunipatia kipato hasa katika mitandao Tafadhalini naombeni ushauri na uzoefu nifanye nini ili kufanikisha wazo langu hili. Asanteni,
Nina Uzoefu Wa Hizo Kazi 3 Yearz
Tools Zinazohitajika
1. Camera {kwa uzoefu wangu Tafuta Canon Eos 7D, au 5D Au DSLR YOYOTE. Hapa Utapata Picha Yenye Autofocus Kubwa Na Clear}
2. Utahitaji Photo Printer {Kama Huko Vizur Chukua Kubwa Za 30M Lakin Pia Utahitaji Printer Ndogo Kwa Ajil Ya Express Services! Au Ndogo Za Epson L800! Hiz Ni Econom Hazitumii wino mwingi! Na Pia Ni Ngumu}
3. Studio Lighting Tool
Kwa Indoor Hapa Utahitaji Taa Za Studio Kawaida Auto Ambazo zinadetect Mwanga Zenyewe! Utahitaji Reflector Kwa Classic Photograph Hii Itatumika Hata Outdoor! Pia Utahitaji Umbrella Photo Lighting Kwa Indoor Shots. External Flash! Kwa Ajil Ya Kukupa Mwanza Safi Katika Outdoor Shot. Usisahau Background. Ingawaje PS imerahisisha Now Days
4. Photo Editing Software
Kwa Ulimwengu Wa Sasa Editing Software Ni Kitu Cha Muhimu Hapa Napendekeza Adobe Photoshop CS5! Photoshine! Na Photoscape.
4. Photo Materials
Hapa Namaanisha Photo Frame! Bahasha! Mikasi! Make Up Tools!
5. Storage Devices
Kila Kaz Unayofanya Lazima Uhifadh! Ingawaje Utakuwa Na Editing Computer Usisahau Kutenga External Hard Disk Za 1TB Kwa Usalama zaid wa Kumbukumbu za wateja.
6. Scanner
Hii Ni Kitu Muhimu Sana Na Pesa Ipo Hapa Kwan Watu Weng Wanakuja Na Picha Zao Za Zaman Kutaka Zitolewe Upya! Nying Za Marehemu.
Vipo Ving Mkuu Ila Kama Utahitaji Mpiga Picha Nipo Hapa Mkuu Sina Dili!!
0786143441
asante sana mdau kwa ushikiano wako.Mkuu hongera sana.. Tafuta camera nzuri kama Nikon nk usitumie camera ya simu au tablet inapunguza reputation yako kwa anayekutazama au kwa mteja, nenda na class kidogo, utapata mbinu nyingi na tofautitoufati, pia usideal na picha za watu pekee angalia na upande kama wanyama nk..tembelea huko mbugani, ndege, Maua nk
Halafu ziwekee copyright picha zako kwa water mark, halafu post mtandaoni, fungua website na account kwenye mitandao ya kijamii, angalia waliofanikiwa wamepitia wapi, wapo wengi sana mtandaoni,
Yaani mkuu picha moja inakutoa kimaisha ikipata umaarufu mitandaoni,mfano kuna picha ya mtoto ilipigwa Uganda na mwanafunzi wa kimarekani ilimuingizia pesa ya maana, namaanisha uniqueness ya picha,siyo kila picha..
Hata mm napenda sana kupiga picha najua baadae nitaifanya
Nawatakia pasaka njemaaa....!
Naomba ushauli nataka kufungua photo studio ya kawaida kabisa sasa sijuinianzie wapi na sijui vifaa vyakevina ghalimu pesa ngapi naomba msaada wa mawazo na akili iliniweza kufanikisha hilo.asanteni