Msaada wa mawazo kuhusu pesa za mkopo

Msaada wa mawazo kuhusu pesa za mkopo

co fm

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Posts
1,541
Reaction score
2,487
Habari za muda huu wadau, hapa kazini kwetu kuna watu wamekuja wanataka kutupa mikopo kwa riba ndogo sana kiasi kwamba kwa mshahara wangu ninaweza kupata mpaka million 50 kwa miaka mitano.

Sasa naombeni msaada wa mawazo jinsi ya kutumia hizo million 50 kwa faida.

Sina gari wala nyumba
 
Habari za muda huu wadau, hapa kazini kwetu kuna watu wamekuja wanataka kutupa mikopo kwa riba ndogo sana kiasi kwamba kwa mshahara wangu ninaweza kupata mpaka million 50 kwa miaka mitano.Sasa naombeni msaada wa mawazo jinsi ya kutumia hizo million 50 kwa faida. Sina gari wala nyumba
kama huna au haujawai kuwa na mpango iwe wa uwekezaji au biashara, usichukue hiyo 50.. labda kama unataka kujenga..
 
Chukua kisha jenga nyumba kwa 35millions ambayo itakua na shelf 1, bed room 1, washroom 1, dining, seating, kitchen na utaweka uzio.
Baada ya hapo tafuta Suzuki Jimmy ya 15millions.
Na maisha yatakua poa tu kwasababu utakua umeachana na malipo ya kodi na usaafiri wako utakua unakula mafuta kidogo na utafurahia maisha huku ukibaki na mshahara wa kula na bills.
 
Chukua kisha jenga nyumba kwa 35millions ambayo itakua na shelf 1, bed room 1, washroom 1, dining, seating, kitche na utaweka uzio.
Baada ya hapo tafuta Suzuki Jimmy ya 15millions.
Na maisha yatakua poa tu kwasababu utakua umeachana na malipo ya kodi na usaafiri wako utakua unakula mafuta kidogo na utafurahia maisha ukibaki na mshahara wa kula na bills.
Pesa ya kodi ndio hiyo atakayokuwa anayokatwa kwemye mshahara kwa ajili ya mkopo aliochukua.

So utaona kwamba ukijenga na ukipanga ni kama vitu vinaendana hivi na tofauti ni ndogo sana.
 
Chukua kisha jenga nyumba kwa 35millions ambayo itakua na shelf 1, bed room 1, washroom 1, dining, seating, kitchen na utaweka uzio.
Baada ya hapo tafuta Suzuki Jimmy ya 15millions.
Na maisha yatakua poa tu kwasababu utakua umeachana na malipo ya kodi na usaafiri wako utakua unakula mafuta kidogo na utafurahia maisha huku ukibaki na mshahara wa kula na bills.
Sawa mkuu nimekusoma
 
Habari za muda huu wadau, hapa kazini kwetu kuna watu wamekuja wanataka kutupa mikopo kwa riba ndogo sana kiasi kwamba kwa mshahara wangu ninaweza kupata mpaka million 50 kwa miaka mitano.Sasa naombeni msaada wa mawazo jinsi ya kutumia hizo million 50 kwa faida. Sina gari wala nyumba
Chukua hiyo 50 halafu peleka UTT kama ilivyo. Baada ya hapo anza sasa kujitafakari mdogomdogo. Ukichukua usitumie hata 100 ipeleke kama ilivyo UTT kama una mpango wa kuimega hata laki acha usichukue kabisa
 
Chukua Mil 50 ununue bajaji 2 na gari aina ya IST 1 ufanye biashara ya usafiri ikiwemo uber, bolt nk.

Baada ya miaka 3 tu, utakuwa ushamaliza deni na biashara yako inaendelea kama kawa.
UBer yenyewe inategemea na yeye yuko mkoa gani?

Bajaj za kuwakabidhi vijana bado anaongeza risk kubwa na wakati huo mtaji wenyewe bado ni risk
 
Habari za muda huu wadau, hapa kazini kwetu kuna watu wamekuja wanataka kutupa mikopo kwa riba ndogo sana kiasi kwamba kwa mshahara wangu ninaweza kupata mpaka million 50 kwa miaka mitano.Sasa naombeni msaada wa mawazo jinsi ya kutumia hizo million 50 kwa faida. Sina gari wala nyumba
"riba ndogo sana", yani hi sentesi tu inaonesha uko tayari hata kabla ujaomba ushauri humu ndani. Mi nikushauri tu kua hakuna Riba ndogo, riba ni riba tu, ndiomana zimeharamishwa(Haram)
 
Back
Top Bottom