Msaada wa mawazo kuhusu pesa za mkopo

Msaada wa mawazo kuhusu pesa za mkopo

Habari za muda huu wadau, hapa kazini kwetu kuna watu wamekuja wanataka kutupa mikopo kwa riba ndogo sana kiasi kwamba kwa mshahara wangu ninaweza kupata mpaka million 50 kwa miaka mitano.Sasa naombeni msaada wa mawazo jinsi ya kutumia hizo million 50 kwa faida. Sina gari wala nyumba
Mbona husemi wanatoka wapi au Taasisi gani?, hizo mambo ya "riba ndogo sana, mtakuja kuleta mabandiko humu riba imechange juu kwa juu mnaomba ushauri...
 
Tafuta wataalam wa mambo ya fedha wakushauri vizuri,maana mkopo wa 50M na marejesho yake ni Kwa kipindi Cha miaka mitano,basi Kuna uwezekano riba ikawa juu.
 
Kwann mkuu?
Utapigwa na kitu kizito. Jiulize maswali haya kwanza.:-
1. Watoa mikopo (Hiyo Taasisi inayokopesha) wamekupendea nini? Chukua Tahadhari. Mikopo ni biashara. Ukichukua Mkopo wao, manake ww ni Mteja wao. Je, marejesho na riba kwa muda mtakaokubaliana vinaendana? Usije ukakopa mil 50 halafu ukarejesha mil 70+ bila maumivu.
2. Je, Watoa mikopo na masharti yao wanaonekana kuwa ni Taasisi iliyokubalika kisheria (inatambulika), ni endelevu(Sustainable) au ni hao wakausha damu? Mwajiri wako anasemaje i.e. ameridhia kuhusu ww Kukopa kwenye Taasisi hiyo?
 
Brother chukua hiyo hela nenda sehemu ambayo haijachangamka kama kiwangwa ama chanika..nunua shamba kwa say 10m, lirasimishe kisha chukua hati peleka bank, vuta pesa ndefu, fanya maisha siku moja utaniahukuru.
Mmmh! Huu ushauri unafikirisha. Akinunua shamba na kulirasimisha say jumla ni 15m atabaki na 35m. Ataliendeleza au? Halafu aende bank na Hati (Title deed) akakope tena pesa ndefu? Mbona naona kama ni duplication ya madeni? Ukizingatia Hana wazo au hajasema kama anakusudia kuufanyia nini huo Mkopo wa Kwanza.
 
Pesa ya kodi ndio hiyo atakayokuwa anayokatwa kwemye mshahara kwa ajili ya mkopo aliochukua.

So utaona kwamba ukijenga na ukipanga ni kama vitu vinaendana hivi na tofauti ni ndogo sana.
Nyumba ya kupanga huwezi iuza siku ukikwama,Wala huwezi iwekea dhamana,chako ni chako no matter how,na Hiyo ndo kazi ya huo mkopo.
 
UBer yenyewe inategemea na yeye yuko mkoa gani?

Bajaj za kuwakabidhi vijana bado anaongeza risk kubwa na wakati huo mtaji wenyewe bado ni risk
Amasema yupo Dar. Hapo anatakiwa yeye akabe na Uber, Bolt. Alaf bajaj awakabidhi wadogo zake au ndugu zake awe anawalipa kwa siku, week au mwezi.
 
Habari za muda huu wadau, hapa kazini kwetu kuna watu wamekuja wanataka kutupa mikopo kwa riba ndogo sana kiasi kwamba kwa mshahara wangu ninaweza kupata mpaka million 50 kwa miaka mitano.

Sasa naombeni msaada wa mawazo jinsi ya kutumia hizo million 50 kwa faida.

Sina gari wala nyumba
Hakuna mafanyakazi mwenye uwezo wa kukopa 50M hajui cha kufanya,iwe serikalini ama private
 
Una mshahara mkubwa Sana, maana kwa mkopo huo si chini ya laki 9 mpaka milioni rejesho kwa kila mwezi. Mkuu kwa mshahara huo kwanini hauna Nyumba wala gari mpaka leo?
 
Chukua kisha jenga nyumba kwa 35millions ambayo itakua na shelf 1, bed room 1, washroom 1, dining, seating, kitchen na utaweka uzio.
Baada ya hapo tafuta Suzuki Jimmy ya 15millions.
Na maisha yatakua poa tu kwasababu utakua umeachana na malipo ya kodi na usaafiri wako utakua unakula mafuta kidogo na utafurahia maisha huku ukibaki na mshahara wa kula na bills.
Shelf moja ya kuwekea nini?
 
Back
Top Bottom