Msaada wa Mawazo kwa wenye uzoefu wa kununua na kuuza mchele wa Jumla nataka nijiajiri mtoto wa kike

Msaada wa Mawazo kwa wenye uzoefu wa kununua na kuuza mchele wa Jumla nataka nijiajiri mtoto wa kike

Mambo yangekua marahisi hivyo ungeshakua milionea wewe mwenyewe,

@Mleta mada,za kuambiwa changanya na zako..

Mchele unatofautiana kuanzia mbegu,upandaji,eneo unapoulima na ardhi husika...

UFAFANUZI:Ref Magugu,Babati

Kuna aina nyingi

Super Kyela:Mzito kwenye mpunga na ukikobolewa,punje ndefu,harufu nzuri,huangalizi maradufu,kipato kizuri

Super Kula na Bwana:Mrefu,harufu,huota muda mfupi,hupungua kidogo @2kg kwenye kila kilo 80 zilizokobolewa

Super Mkomboz:Mzuri,sio mrefu sana kipato kidogo,harufu nzuri sana,haivumilii ukame wala furiko,bua zake nyepesi

Saro:Hizi unatupia ukipanda(yaani ndo kitalu na ndo jaruba),mfupi,hauna harufu,una kipato kwa maana ya uzalishaji,na bei yake ni chini(ndo huo wa 1000/kg alafu mkaupake mafuta(non sense kwa mfanyabiashara serious na anaefanya biashara endelevu).

Super kawaida :Huu ndo wengi tuna ula tukituma wasichana madukani.

Harufu wanayo ongelea sijui ya mafuta,utapaka tani 100?,hiyo harufu si ni ya mchele mzuri ndo mana huo unaopakwa wana "FAKE" ili ufananie na kunukia huo mzuri?

Nasisitiza:
Mchele unatofautiana na upo wenye harufu nzuri naturally
Saro inayolimwa Mbarali Mbeya inatoka vizuri na inanukia sana! Saro ya Morogoro inatoka tofauti sijui kwanini?

Everyday is Saturday......................... 😎
 
Saro inayolimwa Mbarali Mbeya inatoka vizuri na inanukia sana! Saro ya Morogoro inatoka tofauti sijui kwanini?

Everyday is Saturday......................... 😎
Ya huku kwetu ndo balaa(Mabonde ya Magugu,kisangaji mpaka Magara-Njia ya kwenda Mbulu)
 
Ha

Nilichokiona hapa ni ujuaji mwingi ambao ni kinyume kabisa na uhalisia. Mtu anasema mchele hukaangwa ili kuupa harufu....aisee hatari kabisa....!
Nimemsoma mchizi mpaka nkapata hasira,ana kaanga tani 500,1......,2.........,3..... kwa sauti ya "MAMVI".
 
Mkuu hongera na asante kwa elimu hii ya awali kwa mleta mada,kupaka mafuta na kutia mchanga ni mbinu ya siku nyingi ya wauza mchele wasio waaminifu.

Ila kitu ambacho huwa wanachemka,ni ile harufu OG ya mchele,ambao huwa lazimu wachanganye tu mpya na huo wa muda mrefu ili kuweka eq balance.
Mimi najua mafuta
Yanasaidia mchele usipate kuharibika na kuota vile vijidudu fulani vyeupe vyeupe.
 
We muungwana umepitiliza! Hongera Sana.....afu umenikumbusha ..kupaka mafuta mchele,niliona Same Kuna scheme fulani ya umwagiliaji kule juu!
Kile kitendo kilinichefua Sana!
Kijana amevaa bukta tu anajigaragaza kwenye mchele!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi najua mafuta
Yanasaidia mchele usipate kuharibika na kuota vile vijidudu fulani vyeupe vyeupe.
Of course ndio maana ya kuupaka mchele mafuta. Kuna ile vumbi yake baada ya kukobolewa inakuwa kama poda hivi, sasa ukiweka mchele kwenye mifuko na ukahifadhiwa muda mrefu chumba chenye unyevunyevu lazima itatengeneza uozo utakaozaa wadudu.

Ila kama ni unauzwa kwa haraka haukai store zaidi ya miezi 6 then haina haja ya kupaa mafuta....
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kwa ninachokiona hapa wadau mpo busy kumshauri bi dada namna ya kununua mchele ila balaa linakuja kwenye mauzo na kuuza.... Hapo ndipo kuna mziki..... Unaweza kuja na mchele wako paap na ukafika mjini na kuwekwa store /sehemu ya kuhifadhi bila shida. Balaa litaanza namna ya kuuza hapo ndipo mziki ulipo.....

Kuna dada alibeba lumbesa yake ya mchele, akafungua kishop akajaza pale mchele mzuri sana anauza jumla na reja reja...... Mziki ni kwenye mauzo.

So ukiwa unajiandaa kwenda kuchukua mzigo bi dada pay attention kwenye namna utauza hapa ndipo kuna uchawi......
 
Naunga mkono hoja nishawahi kufata mchele mlimba nikajikuta nakosa wateja nilinunua kg 1 tsh1000 ukijumlisha gharama za usafiri,ushuru,upakiaji na upakuaji ilitakiwa niuze 1700/kg ilinipate tsh 100 Kama faida kwa kila kg hapo ndio show ilopoanzia nikaachana na hii biashara nikarudi zangu kwenye ufugaji

Ukaamua urudi kufuga Kuku mzee tehee teeeeh wasalimie Mlimba ituhi
 
Naunga mkono hoja nishawahi kufata mchele mlimba nikajikuta nakosa wateja nilinunua kg 1 tsh1000 ukijumlisha gharama za usafiri,ushuru,upakiaji na upakuaji ilitakiwa niuze 1700/kg ilinipate tsh 100 Kama faida kwa kila kg hapo ndio show ilopoanzia nikaachana na hii biashara nikarudi zangu kwenye ufugaji
Mkuu, huwa nafikiri hyo biashara ni nyepesi kumbe sivyo.. kukaanga na kupaka mafuta tani kadhaa si mchezo. Kumbe ile harufu huwa ni bandia?!
 
Moro hakuna mchele mzuri
Morogoro kuna mchele mzuri sana tu, ila ni mkoa unaolima mbegu nyingi za mpunga ajabu, mbegu zote za majaribio hufanyiwa testing Morogoro kuliko maeneo mengine nchini...

Na kwa sababu hakuna mbegu 2-3 dominant, matokeo yake mashineni, mchele unakobolewa magunia mbegu ndefu, fupi na nene mchanganyiko!

Ila ukipata mchele wa mbawa 2 au berenge au fire au super Shinyanga pure! Waweza amini ni mchele wa Mbeya!

Everyday is Saturday........................... 😎
 
Mkuu kwani umilionea ni tsh ngapi si kuanzia milion 1 Sasa Mimi nakosa milion 1!!! .... Nimeongea based on my experience na ndio maana nimemwambia aende mwenyewe field asihadaike na maneno matam ya mtandaoni. Na nilielezea huo utofauti based kwenye Location za upatikanaji wa mchele.

Nimesema kupaka mafuta kwasababu ya mtaji wake wa milion 5 , wewe unaleta mambo ya Tani 1000 mkuu. Milion 5 inanunua Tani 1000. Nilitoa option ya njia hiyo ili akuze mtaji Kama akifikia kuwa na uwezo wa hizo Tani 1000 atatafuta njia nyingine bora. Ila kwa kuanza niliona ni vyema aanze na huo mchele wa kuuzwa elfu 1 ili aweze Ku-Upgrade na kuja kuuza mjini.

Wewe umezungumzia experience yako na uko sahihi. Mimi nimezungumzia experience yangu na ninafanya hivyo. Kama uko tayari njoo nikuuzie mchele mkuu Niko dar kilo 1700 nafanya delivery free.
Naomba mnitoe matongotongo ndugu zangu. Mchele unapakwaje mafuta? Ni mafuta ya aina gani wanapaka? Duniani kote wanafanya hili zoezi au ni exclusive kwa Bongo tu?
 
Back
Top Bottom