Msaada wa Mawazo kwa wenye uzoefu wa kununua na kuuza mchele wa Jumla nataka nijiajiri mtoto wa kike

Saro inayolimwa Mbarali Mbeya inatoka vizuri na inanukia sana! Saro ya Morogoro inatoka tofauti sijui kwanini?

Everyday is Saturday......................... 😎
 
Saro inayolimwa Mbarali Mbeya inatoka vizuri na inanukia sana! Saro ya Morogoro inatoka tofauti sijui kwanini?

Everyday is Saturday......................... 😎
Ya huku kwetu ndo balaa(Mabonde ya Magugu,kisangaji mpaka Magara-Njia ya kwenda Mbulu)
 
Ha

Nilichokiona hapa ni ujuaji mwingi ambao ni kinyume kabisa na uhalisia. Mtu anasema mchele hukaangwa ili kuupa harufu....aisee hatari kabisa....!
Nimemsoma mchizi mpaka nkapata hasira,ana kaanga tani 500,1......,2.........,3..... kwa sauti ya "MAMVI".
 
Mimi najua mafuta
Yanasaidia mchele usipate kuharibika na kuota vile vijidudu fulani vyeupe vyeupe.
 
We muungwana umepitiliza! Hongera Sana.....afu umenikumbusha ..kupaka mafuta mchele,niliona Same Kuna scheme fulani ya umwagiliaji kule juu!
Kile kitendo kilinichefua Sana!
Kijana amevaa bukta tu anajigaragaza kwenye mchele!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi najua mafuta
Yanasaidia mchele usipate kuharibika na kuota vile vijidudu fulani vyeupe vyeupe.
Of course ndio maana ya kuupaka mchele mafuta. Kuna ile vumbi yake baada ya kukobolewa inakuwa kama poda hivi, sasa ukiweka mchele kwenye mifuko na ukahifadhiwa muda mrefu chumba chenye unyevunyevu lazima itatengeneza uozo utakaozaa wadudu.

Ila kama ni unauzwa kwa haraka haukai store zaidi ya miezi 6 then haina haja ya kupaa mafuta....
 
Reactions: amu
Kwa ninachokiona hapa wadau mpo busy kumshauri bi dada namna ya kununua mchele ila balaa linakuja kwenye mauzo na kuuza.... Hapo ndipo kuna mziki..... Unaweza kuja na mchele wako paap na ukafika mjini na kuwekwa store /sehemu ya kuhifadhi bila shida. Balaa litaanza namna ya kuuza hapo ndipo mziki ulipo.....

Kuna dada alibeba lumbesa yake ya mchele, akafungua kishop akajaza pale mchele mzuri sana anauza jumla na reja reja...... Mziki ni kwenye mauzo.

So ukiwa unajiandaa kwenda kuchukua mzigo bi dada pay attention kwenye namna utauza hapa ndipo kuna uchawi......
 
Naunga mkono hoja nishawahi kufata mchele mlimba nikajikuta nakosa wateja nilinunua kg 1 tsh1000 ukijumlisha gharama za usafiri,ushuru,upakiaji na upakuaji ilitakiwa niuze 1700/kg ilinipate tsh 100 Kama faida kwa kila kg hapo ndio show ilopoanzia nikaachana na hii biashara nikarudi zangu kwenye ufugaji
 
Ukaamua urudi kufuga Kuku mzee tehee teeeeh wasalimie Mlimba ituhi
 
Mkuu, huwa nafikiri hyo biashara ni nyepesi kumbe sivyo.. kukaanga na kupaka mafuta tani kadhaa si mchezo. Kumbe ile harufu huwa ni bandia?!
 
Moro hakuna mchele mzuri
Morogoro kuna mchele mzuri sana tu, ila ni mkoa unaolima mbegu nyingi za mpunga ajabu, mbegu zote za majaribio hufanyiwa testing Morogoro kuliko maeneo mengine nchini...

Na kwa sababu hakuna mbegu 2-3 dominant, matokeo yake mashineni, mchele unakobolewa magunia mbegu ndefu, fupi na nene mchanganyiko!

Ila ukipata mchele wa mbawa 2 au berenge au fire au super Shinyanga pure! Waweza amini ni mchele wa Mbeya!

Everyday is Saturday........................... 😎
 
Naomba mnitoe matongotongo ndugu zangu. Mchele unapakwaje mafuta? Ni mafuta ya aina gani wanapaka? Duniani kote wanafanya hili zoezi au ni exclusive kwa Bongo tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…