Msaada wa mawazo na uzoefu kuhusu biashara ya kukopesha pesa (Microfinance)

Msaada wa mawazo na uzoefu kuhusu biashara ya kukopesha pesa (Microfinance)

Mzee Wa Republican

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2013
Posts
1,666
Reaction score
847
Ndugu wananchi, wanabodi na great thinkers wa humu JF Salaam !!

Tayari mwaka 2023 umeanza kwa kasi na kama ilivyo ada tumeendelea na pilika pilika za kusaka maisha kona mbali mbali.

Katika harakati za kujikwamua kiuchumi nimefikiria kufanya biashara ya kukopesha pesa (Microfinance). Kiufupi ni biashara ambayo kwa sasa ina sheria nyingi kali na hata leseni yake kwa sasa hutolewa na benki kuu wenyewe (BOT).

Moja ya masharti yake makali ni kwamba ni lazima uwe na mtaji usiopungua milioni 20, na pesa hiyo isiwe ya kukopa.

Kibongo bongo kwa sharti hili wengi ni ngumu kuanzisha biashara hii (labda uwe mfanyabiashara) au kama ni mtumishi basi ni lazima uwe umefanya saving kwa muda mrefu sana au uuze asset yako mf kiwanja na kadhalika.

Sanjari na hayo masharti yake, nimekuja mbele zenu kuomba ushauri na uzoefu kuhusu biashara husika kwani humu ndani naamini kuna watu wenye uzoefu wa biashara mbali mbali ikiwemo na hii.

Nitafurahi kama nitapata mrejesho kuhusu changamoto za biashara hii, fursa zake, namna ya kuiendesha, tabia za wakopaji na mazingira mengine anuai yanayoizunguka sekta hii kwa sasa.

Ni imani yangu ya kwamba nitapata mwangaza zaidi baada ya kuleta wazo langu mbele yenu.

Uchumi wa Tanzania utajengwa na watanzania wenyewe.

Naomba kuwasilisha mbele zenu wakuu . . . . . .!
 
Nilikuw naangalia hp... wameandika proof... na sio km ile ya kuandikaga tu😂😂.
Ila there must be a way..
I hv subscribed this thread
 

Attachments

Kazi ya nidhamu, heshima, na inayoitaji discipline ya hali ya juu ili taasisi ikue!
 
Kila la kheri na ngoja waje kukupa muongozo...
 
Achana na habari ya kufungua kampuni. Kopesha wamama wajasiriamali mtaani kwako alaf hakiiisha una polisi mshikaji wako wa kuwatia jamba jamba wale wasiolipa. Utanishukuru baadaye
Kopesha wanachuo mimi nashirikiana na mzee pamoja na mwanangu yeye pia ni poti kanda flani hiv biashara inaenda bila longo longo
 
Tafuta biashara you fanye mfano chinja ng'ombe then unakopesha baadae ya MUDA mliokubaliana unapitia ela zako

Wabongo wanapenda MAKOPO kuliko kitu chochote nakuakikishia baadae ya MUDA utapiga ela balaa
 
Back
Top Bottom