Msaada wa mawazo, nina 5,500,000 naweza kujenga nyumba ya aina gani?

Msaada wa mawazo, nina 5,500,000 naweza kujenga nyumba ya aina gani?

Nina 5,500,000 Tu. Kiwanja ninacho.
Sitaki tena kulipa Kodi miee. Nitafanikiwa kweli vyumba vitatu vya kulala na sebule? Vitatu Kwa Sababu Nina watoto wa kiume na kike. Au nijenge kibanda cha Aina gani? Maisha is not fair
Kwa vyumba vi3 utatumia tofali kama 3,500 - 4,000 hapo kila tofali ni tzs 1,000. Bado cement, mchanga n.k atleast endelea kujichanga uongeze pesa
 
Kwa vyumba vi3 utatumia tofali kama 3,500 - 4,000 hapo kila tofali ni tzs 1,000. Bado cement, mchanga n.k atleast endelea kujichanga uongeze pesa
WHAT!? Tofali 3500 hadi 4000 kwa nyumba ya vyumba vitatu? What!?

Wataalam wanasema chumba kimoja ni hadi tofali 400! Ongeza msingi, sijui na nini, sijui na nini, sijui na nini hufikii hayo matofali! Ngoja waje wenyewe.
 
WHAT!? Tofali 3500 hadi 4000 kwa nyumba ya vyumba vitatu? What!? Wataalam wanasema chumba kimoja ni hadi tofali 400! Ongeza msingi, sijui na nini, sijui na nini, sijui na nini hufikii hayo matofali! Ngoja waje wenyewe.
Binafsi nipo kwenye ujenzi na nimefikia hatua ya kupaua. Wakati naanza nilitaka msingi uendejuu kidogo kutokana na nature ya eneo na ulikula tofali 2,000 na wakati wa kupandisha ukuta hadi kwenye linta na kozi3 za juu nikatumia tofali 2,000 pia. Inategemea na aina ya nyumba yenye unataka.
 
Nina 5,500,000 Tu. Kiwanja ninacho.

Sitaki tena kulipa Kodi mie. Nitafanikiwa kweli vyumba vitatu vya kulala na sebule?
Ushauri unaweza kutoka kwa yeyote hapa jukwaani kwa kuzingatia yafuatayo...

1) Uko mkoa gani ? Ni mjini au kijijini?

2) kulingana na maelezo yako ati una kiwanja tayari , Je kuna vifaa vya ujenzi ambavyo unavyo tayari?

Jibu yafuatayo upate ushauri yakinifu.

Ushauri tu.

TEKERI.
 
Kwa vyumba vi3 utatumia tofali kama 3,500 - 4,000 hapo kila tofali ni tzs 1,000. Bado cement, mchanga n.k atleast endelea kujichanga uongeze pesa
Acha uongo . Nina nyumba ya room 4 na sebule, jiko na stoo na nimetumia tofali 2700 kwa nyumba ya room tatu za kulala na sebule atatumia fofali 1200 hadi 1500 kwa kujenga. Msingi ajenge na mawe
 
Acha uongo . Nina nyumba ya room 4 na sebule, jiko na stoo na nimetumia tofali 2700 kwa nyumba ya room tatu za kulala na sebule atatumia fofali 1200 hadi 1500 kwa kujenga. Msingi ajenge na mawe
Uongo kwako mkuu. Nipo najenga now.

Itategemea wapi anajenga, aina ya nyumba na size ya nyumba na msingi atatumia material gani ndio itadetermine kiasi cha tofali za kutumia.

Mleta mada kaomba ushauri kwa pesa yake atajenga nyumba ya aina gani.
 
20220112_141758.jpg
 
Banda ni nyumba, mbona umekuwa hivyo.
?
Wewe una ngapi kujifanya. Wacha kejeli na kubeza
Sasa mil.5.5 inaweza kujenga nyumba au Banda? Tatizo mnataka kudanganywa nakupewa matumaini kama wanawake wakati ukweli ndio huo..

Tuwekee hapa Nyumba ya mil.5.5
 
Mimi nataka kujenga taratibu maana Sina hela cash,
Nachoweza kupata Ni 500k cash kila mwezi kwa ajili ya hiyo nyumba,

Ntatumia muda gani? kujenga boma la yumba vinne, sebule, jiko, store na dining kuhusu kupaua na finishing ntatoboa mkeka.

Hii ndiyo njia nzuri ya kujenga kama ni mpambanaji!

Utajenga nyumba nzuri sana hata kama itakuchukua 2 years kama kila mwezi unaweka laki 5 kwenda kwenye nyumba!
 
Back
Top Bottom