Msaada wa mawazo, nina 5,500,000 naweza kujenga nyumba ya aina gani?

Msaada wa mawazo, nina 5,500,000 naweza kujenga nyumba ya aina gani?

Mleta Mada husemi ni nyumba ya aina gani, ya tope, tofali za kuchoma, tofali za udongo au siment ?
km ni block na upo ndani ya Mipango Miji au Jiji yatarisha tofali 4000
kuna vyumba vitatu, karo na choo safi, vingine polepole nyumba ya mbele mpaka fence ni baadae
 
Jenga nyumba style ya mgongo wa tembo, wenye vyumba viwili vidogo na sebule., madirisha ya kawaida na sio aluminium, mabati ya kizamani na sio ya tailand or msauzi, tofali fyatua mwenyewe, kila mfuko fyatua tofali 35 atleast tofali 1500 zipatikane....jibane sana sana kwa bajeti hiyo, pia onana na fundi atakushauri, awe mwaminifu maana asilimia kubwa ya mafundi wetu ni waongo/wezi.
 
Mimi nataka kujenga taratibu maana Sina hela cash,
Nachoweza kupata Ni 500k cash kila mwezi kwa ajili ya hiyo nyumba,

Ntatumia muda gani? kujenga boma la vyumba vinne, sebule, jiko, store na dining kuhusu kupaua na finishing ntatoboa mkeka.
18 months.
 
18 months.
18 months ntakuwa nimetumia 9m tu ndo itoshe boma lote?

Location sio town msingi mawe, tofari za choma kifupi vifaa vyote ambavyo sio vya dukani mfano mchanga, mawe, tofari bei Chee hela fundi na vibarua haijachangamka ila ukienda dukani ndo vitu vyote bei kubwa.
 
Hao wanaokuambia ata vibanda sa zingine hawana
 
18 months ntakuwa nimetumia 9m tu ndo itoshe boma lote?

Location sio town msingi mawe, tofari za choma kifupi vifaa vyote ambavyo sio vya dukani mfano mchanga, mawe, tofari bei Chee hela fundi na vibarua haijachangamka ila ukienda dukani ndo vitu vyote bei kubwa.
Boma?
Inatosha.
 
Acha uongo . Nina nyumba ya room 4 na sebule, jiko na stoo na nimetumia tofali 2700 kwa nyumba ya room tatu za kulala na sebule atatumia fofali 1200 hadi 1500 kwa kujenga. Msingi ajenge na mawe
Duuh hii naifanyia tafiti tunapgwa parefu sana , kumbe utopolo sio yanga tu
 
Nina 5,500,000 Tu. Kiwanja ninacho.

Sitaki tena kulipa Kodi mie. Nitafanikiwa kweli vyumba vitatu vya kulala na sebule? Vitatu Kwa Sababu Nina watoto wa kiume na kike. Au nijenge kibanda cha aina gani?

Maisha is not fair
5.5 ni hela lakini ni kiwango kidogo sana kwa ujenzi wa nymba ya vymba vitatu. ningekushauri fanya yafuatayo

1. tafuta ramani ya nymba unayoitaka. fanya juu chini upate mchanganuo wa garama za ujenzi ( BOQ)- hii itakusaidia kupangilia ujenzi wako ki phace au awamu
2. kutokana na pesa yako kuwa ndogo unaweza jenga msingi wa nyumba nzima bt ukaamua kupandisha sehemu ya nyumba labda vymba viwili tu. ukaishi humo huku ukikusanya nguvu ya kumalizia nyumba zima.
3. ukishapata mchanganuo wa idadi ya material yanayohitajika kulingana na phase unayotaka kujenga nenda hardware lipia material km cement, tofali, bati n.k chukua risiti ukishapata material kulingana na phase unayotaka kujenga mtafute fundi jenga kwa awamu
 
Mleta Mada husemi ni nyumba ya aina gani, ya tope, tofali za kuchoma, tofali za udongo au siment ?
km ni block na upo ndani ya Mipango Miji au Jiji yatarisha tofali 4000
kuna vyumba vitatu, karo na choo safi, vingine polepole nyumba ya mbele mpaka fence ni baadae
Thanks, Kuna bwana m1 kaniambia tofali 4,000 hazifiki.
 
Binafsi nipo kwenye ujenzi na nimefikia hatua ya kupaua. Wakati naanza nilitaka msingi uendejuu kidogo kutokana na nature ya eneo na ulikula tofali 2,000 na wakati wa kupandisha ukuta hadi kwenye linta na kozi3 za juu nikatumia tofali 2,000 pia. Inategemea na aina ya nyumba yenye unataka.
Senteso ya mwisho hapo juu ndiyo KIGEZO MUHIMU.
 
Uongo kwako mkuu. Nipo najenga now. Itategemea wapi anajenga, aina ya nyumba na size ya nyumba na msingi atatumia material gani ndio itadetermine kiasi cha tofali za kutumia.
Mleta mada kaomba ushauri kwa pesa yake atajenga nyumba ya aina gani.
Basi jamani mpeni USHAURI, acheni KUBISHANA, yeye ameomba ushauri, MPENI JAMANI!
 
Back
Top Bottom