Msaada wa mawazo, nina 5,500,000 naweza kujenga nyumba ya aina gani?

Sawa lakini hiyo ramani na hizo BOQ ni pesa! Ambazo atazitoa kwenye hiyo 5.5m!?
 
Kwa vyumba vi3 utatumia tofali kama 3,500 - 4,000 hapo kila tofali ni tzs 1,000. Bado cement, mchanga n.k atleast endelea kujichanga uongeze pesa
We Jamaa nimuongoo balaa yaani Nyumba shule ya vyumba vitatu itumie tofali zote hizo
 
Nikikumbuka kupaua tu nilitumia 5.5 na nikaongezea kidogo nachoka[emoji2359][emoji2359][emoji2359][emoji2359], Jamani ujenzi mh!!!!
 
Ndugu yangu acha tu Ujenzi shughuli pevu, ila Jamaa hiyo 5.5 anaweza kutoboa ila kwangu naona ngumu maana mh!!!!!
 
Uongo kwako mkuu. Nipo najenga now. Itategemea wapi anajenga, aina ya nyumba na size ya nyumba na msingi atatumia material gani ndio itadetermine kiasi cha tofali za kutumia.
Mleta mada kaomba ushauri kwa pesa yake atajenga nyumba ya aina gani.
Uko sahihi ujenzi gharama na suala la tofari inategemea na uitaji wa nyumba uweje
 
Mkuu ulifanikiwa kuanza ujenzi? Me siyo fundi wala sijawahi kujenga lakini kwa pesa yako unaweza kuanza ujenzi wa nyumba yoyote. Kumbuka Nimemanisha kwa pesa hiyo unawezakuanza ujenzi. Soon nitaanza pia ujenzi maana nimechoka kupanga
 
WHAT!? Tofali 3500 hadi 4000 kwa nyumba ya vyumba vitatu? What!? Wataalam wanasema chumba kimoja ni hadi tofali 400! Ongeza msingi, sijui na nini, sijui na nini, sijui na nini hufikii hayo matofali! Ngoja waje wenyewe.
Mkuu nimejenga vyumba vitatu viwili master, jiko store choo Cha public, dining na sitting room umebeba tofari kama 4000
 
Inatosha na chenji inabaki kama ukijenga ya TEMBE mkuu.
 
Vyumba 3 siyo nyumba ndogo mzee,maana ukiweka jiko,choo,sebule kunaongeza ukubwa....jenga chumba na sebule na choo ndani hapo kidogo utafanya jambo.
 
Nina 5,500,000 tu. Kiwanja ninacho.

Sitaki tena kulipa Kodi mie. Nitafanikiwa kweli vyumba vitatu vya kulala na sebule?

Vitatu Kwa Sababu Nina watoto wa kiume na kike. Au nijenge kibanda cha aina gani?

Maisha is not fair
Kwa iyo ela vyumba vitatu niongo kutoboa may be Kwa msingi unaweza kufikia Marengo kihasi flan ila unaweza kutengeza nyumba ya kuanzia ya vyumba ata viwili pamoja na sebre na choo tofar 1500 cement 35 plus nondo na ela ya kazi apo unaweza kutoboa Kwa boma ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…