Msaada wa muda wa kufuturu na kula daku kanda ya Shinyaga

Msaada wa muda wa kufuturu na kula daku kanda ya Shinyaga

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
Kichwa cha habari chahusika naomba mwenye ratiba ya mwezi mzima ya muda wa kufuturu na kula daku alfajir kwa kanda hii ya Shinyanga.

Nafanya kazi ya uchimbaji porini huku hakuna kanisa wala msikiti hakuna hata adhana.
adhan.png
 
Mkazi WA Dar na WA Kigoma hawawezi futuru muda Mmoja kutokana na kuchelewa kuzama Kwa jua.

Jambo la muhimu chunguza hapo ulipo jua halionekani machoni kwenye mgongo WA ardhi,futuru

N.B, Pasitokee Huko uendako kuzama jua pakawa na mlima ambao utakuzuia kulipna jua ukafuturu,zingatia mda.
 
We ukiona jua limezama futuru hapohapo, unasubiri adhana ndio ufuturu?
ahsante bro kwa ushauri ila ukiwa shimoni jua utalionaje? nimesema niko mgodini huko chini ni dunia ingine huwezi kujua usiku wala mchana na hata mvua ikinyesha huwezi jua hata kibla huwezi jua ni wapi ila bahati tunachofanya tunatumia compass kutuongoza
 
Kimbembe kitakuja siku ya kuhitimisha funga ya mwezi mzima eti mpaka kiongozi wa dini aseme mwezi umetoka wafungue wakati mwezi upo juu unaonekana
 
Ahsante sana Dr Mambo Jambo kwa msaada wako mkubwa bila kusita nimeamini kweli maneno ya mtu flani rafiki yangu mkristo ameniambia wewe una shida? ingia jamii forum utapata jibu hata dakika5 hazipiti waislam mna umoja na kupendana sana.Ameniambia muislam anaweza nunua ugomvi wa kidini mahali anaona muislam mwenzake anadhulumiwa hasa issue ya kidini na hiyo ni kweli

Umenipa ratiba ni ya Africa Mashariki hebu tuchukulie mtu aliyeko Lamu Kenya au Zanzibar halafu tumchukulie mtu aliyeko Kigoma.
Mimi hapa nilipo saa 12.39 ambapo ni tarehe ya leo kufuturu jua bado unaliona tena linawaka kwa nguvu bado kweli nitaweza kukaa na kufuturu? nitaona aibu.
Ndio maana nikaomba ya Shinyanga.Ila yako ni msaada wangu mkubwa hasa wakati wa daku ahsante tena MUNGU akujazie zaidi
 
Kumbe mnaabudu jua na mwezi aiseee si muweke muda mmoja tu wa kufuturu yaani saa moja kamili jioni imetosha
 
Safi sana mkuu ila kwa sasa mimi Sina uislamu wala ukristo japo Nimezungukwa na watu hao..

Kuhusu Concern yako Jibu ni Jepesi sana fuata Quran na Sunna..

Hakuna sehemu Qurani imetaja Ikifika Muda fulani ufturu ila imetaja ikifika magharibi unatakiwa kufturu..

Kwa mujibu wa Sunna Magharibu kweny Shinyanga hufika sangapi??

Shinyanga ni moja ya miji ambao ipo karibu sana na Magharibi mwa Nchi za E.Africa kwa hiyo Lazma uangalie anga kwa mujibu wa Sunna..
Hizo saa ni makadirio ya Masaa na sio masaa halisi..

Kwa mfano unaweza ukaona Saa 12 na dakika 21 lakini unaona Wingu jeusi limeanza kutanda na wingu jekundu limeanza kuonekana bado unataka kuendelea kufunga Usubiri Adhana???

Kula daku Hata kama Saa yako itasoma saa 10 usiku lakini kama Anga linaonyesha kumeshaingia Alfajiri huruhusiwi kula daku..
Hayo ni maagizo ya Mtume
 
Kichwa cha habari chahusika naomba mwenye ratiba ya mwezi mzima ya muda wa kufuturu na kula daku alfajir kwa kanda hii ya Shinyanga.

Nafanya kazi ya uchimbaji porini huku hakuna kanisa wala msikiti hakuna hata adhana.
View attachment 2936998
Ndugu yangu fanya kazi zako lakini kama unautaka uisilamu fanya utafute mwalimu akusomeshe baada ya kazi zako,kama ujui muda wa kufungua na kula Daku je utaweza kufahamu jinsi ya kuswali hiwapo utakuwa pekee yako?
 
Uislam ni upole, huruma na kusaidiana.
Elimu Haina mwisho hata wewe waweza kua mwl wake
 
ahsante bro kwa ushauri ila ukiwa shimoni jua utalionaje? nimesema niko mgodini huko chini ni dunia ingine huwezi kujua usiku wala mchana na hata mvua ikinyesha huwezi jua hata kibla huwezi jua ni wapi ila bahati tunachofanya tunatumia compass kutuongoza
Nimekubali adhma yako, Mungu akufanyie wepesi wa kumwabudu
 
Ndugu yangu fanya kazi zako lakini kama unautaka uisilamu fanya utafute mwalimu akusomeshe baada ya kazi zako,kama ujui muda wa kufungua na kula Daku je utaweza kufahamu jinsi ya kuswali hiwapo utakuwa pekee yako?
Kwa taarifa yako mimi ni msomi mzuri sana wa dini nimesoma mwaka1975 sidhani kama ulikuwa umezaliwa au pengine hata wazazi wako walikuwa hawajaoana.

Dini ya uislam ina utaratibu wake usije dhani kula au kufuturu ni muda mtu anaotaka
Mtu kuuliza muda sio kuwa hajui dini yake mtu wa dar na Kigoma hawawezi futuru muda mmoja.

Nikupe mfano mwingine au taarifa kwenye uislam wakati wa kusali sio kusalia upande wowote kuna direction inaitwa Kibla sasa anaweza akaja sheikh kutoka nchi flani na asijue kibla ni wapi hadi apewe maelekezo utasema huyo hajui uislam?
.Ukitaka kujua swali nililouliza lina maana gani angalia mwenzako reymage alivyonijibu juu.

Nashukuru kwa ushauri ila usidandie mada ambayo huna uhakika nayo.
 
Kumbe mnaabudu jua na mwezi aiseee si muweke muda mmoja tu wa kufuturu yaani saa moja kamili jioni imetosha
Numbisa hatuabudu Jua na mwezi.Nikupe mfano hivi unajua Kalenda hii tunayotumia inaitwa kalenda ya Gregory imeasisiwa na papa Gregory na ndio inatumiwa karibu na dunia nzima na inatumia mzunguko wa dunia inavyolizunguka Jua? unaweza sema wakristo wa dunia nzima wanaabudu Jua?.
Kalenda ya Kislam yenyewe inafuata mzunguko wa mwezi haiamanishi waislam wanaabudu mwezi.

Na kwa taarifa yako kalenda ya kislam ndio kalenda sahihi zaidi kuliko kalenda zote na ndio maana kwenye uslam tarehe za idi au kufunga sio constant sababu zinakwenda sawia lakini kwa kalenda ya Gregory kuna mahali wanafanya marekebisho kuweka mambo sawa mfano mzuri pale mwaka mrefu unapokuwa na siku 29 mwezi wa pili ili kufidia ile robo ya dunia kuwa inazunguka jua kwa siku 365 na robo sasa hiyo robo ndio wanazidisha mara nne inakuwa kitu kizima ndio maana miaka yote inayogawanyika kwa nne ndio wanaongeza siku moja ya 29 mwezi wa pili.
Pia miaka yote yenye 00 mwishoni mfano 1800,1900 japo inagawanyika kwa 4 lakini haina miaka mirefu illa sharti mwaka kama una 00 mfano ilivyokuwa 2000 sharti ugawanyike kwa 400 ndio utakuwa mwaka mrefu na ndio maana mwaka 2000 ukawa mwaka mrefu.
Mahesabu yote haya yamewekwa ili dunia isipoteza majira yake.
Nimejaribu tu kueleza haya kuwa hawa watu wa dini hawakufanya haya ajili eti wanaabudu Jua au mwezi
 
Kumbe mnaabudu jua na mwezi aiseee si muweke muda mmoja tu wa kufuturu yaani saa moja kamili jioni imetosha
Ungejua jua na mwezi angani vipo kwa kazi gani usingeandika huu ujinga
1709186041672.jpg

"Yeye Ndiye Aliyelifanya jua
kuwa angavu na mwezi kuwa wenye
kumetameta, na Akaupimia vituo ili
mjue idadi ya miaka na hesabu.
Mwenyezi Mungu Hakuviumba hivyo
ila kwa haki. Huzieleza Ishara kwa watu
wanaojua."

10:7 Qur'an
 
Back
Top Bottom