Msaada wa namna vyeti vya kuzaliwa vinajazwa siku hizi

A
Cheti cha kuzaliwa hakitolewi na nesi hospitali, hilo ni 'tangazo' peleka RITA kapate cheti huko ndo utajaza majina yako…. hongera kwa kupata mtoto mkuu.
Asante sana mkuu lakini ni cheti cha kuzaliwa kabisa
 
Kama kwa data zao inawatosha kutambua nani ni nani basi wacha wafanye kazi yao
 
Sasa si kuna sehemu ya jina la Baba au napo hapajajazwa
 
Baada ya kuambiwa vile, ungesikiliza maelekezo zaidi kuhusu nini cha kufanya….. sio kukaza fuvu.
We nae kaa upumzike kama nilivyo kwambia mwanzo na sio kuweka kauli zako za kejeli na kuonyesha jamii ni kwa kiasi gani hauko sawa kwenye kutoa maoni
 
Maelezo yako yana ukakasi kwa kiasi fulani, kuna vyeti vinavyotolewa na RITA na vyeti ambavyo kwa sasa ni program maalum kwa baadhi ya mikoa ambavyo vinatolewa kituo cha afya na ofisi za watendaji kata, Lakini vyeti vyote lazima viwe na taarifa zote, jina la mtoto, majina ya wazazi wote, umri nk. Nakushauri km unaona utata fika ofisi za RITA zipo ofisi za Wakuu wa Wilaya ukiwa na hicho cheti ulichopewa kwa ufafanuzi.
 
Hili 👇 ndilo jibu kuntu, fanyia kazi hili mengine yote ni umbea tu!
Cheti cha kuzaliwa hakitolewi na nesi hospitali, hilo ni 'tangazo' peleka RITA kapate cheti huko ndo utajaza majina yako…. hongera kwa kupata mtoto mkuu.
 
Hicho cheti anachopewa hapo hospitali huwa kinajazwa kila kitu. Baada ya hapo utaenda RITA kuchukua cheti original.
 
Maelezo yako yanajichanganya! Jibu lilishatolewa huko juu na ncha Kali!
 
Asante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…