Msaada wa namna ya kukabiliana na ugumu wa maisha.

Msaada wa namna ya kukabiliana na ugumu wa maisha.

Mynd177

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2022
Posts
2,817
Reaction score
5,141
Habari za leo wanajukwaa, poleni na majukumu...

Maisha siku za karibuni yameniwia magumu, tafadhali mwenye mbinu za kukabili hali hii anisaidie..

Biashara ndogo ninayofanya ambayo siku za nyuma ilikuwa ikinitunza sasa imeyumba.. Kuna muda naishiwa nguvu nakata tamaa..

Naona Msongo wa Mawazo unaninyemelea, tafadhal mbinu zinahtajka kwa hali na mali..

Natanguliza shukrani..
 
Hauko peke yako mkuu,hali ya uchumi imebadilika sana,hapo kwenye nini cha kufanya nadhani ni kuangalia tu vipaumbele na kuishi kutokana na kipato ulichonacho...lakini ngoja kwanza mwenza uliyenae sio kichomi?
 
Habari za leo wanajukwaa, poleni na majukumu...
Twende kwenye mada..
Maisha siku za karibuni yameniwia magumu, tafadhali mwenye mbinu za kukabili hali hii anisaidie...biashara ndogo ninayfanya ambayo siku za nyuma ilikuwa ikinitunza sasa imeyumba.. kuna muda naishiwa nguvu nakata tamaa.. naona msongo wa mawazo unaninyemelea, tafadhal mbnu zinahtajka kwa hali na mali..
Natanguliza shukrani..
NB: si mwandish mzur saana.
Andika message kwa Nabii Mkuu Geodavie akupe hela uko mkoa gani au mtafute Mchungaji Mashimo akuunganishe direct kwake ungejua mapema ungeongozana na wale Mashekh Jumapili iliyopita walipewa laki tano tano
 
Kwa jinsi ulivyo andika hakuna mtu anaweza kukupa ushauri wa maana. Kwa sababu hujaeleza uko wapi, unafanya biashara gani na changamoto zipi ambazo unakumbana nazo hadi kusababisha biashara kuwa ngumu.
 
Sababu za kuyumba kwa biashara yako labda zinaweza kutoa muongozo wa utatuzi wa tatizo lako
Hauko peke yako mkuu,hali ya uchumi imebadilika sana,hapo kwenye nini cha kufanya nadhani ni kuangalia tu vipaumbele na kuishi kutokana na kipato ulichonacho...lakini ngoja kwanza mwenza uliyenae sio kichomi?
Kaka bado sijaoa. nawaza kama ningekua nimeoa sijui ingekuwaje!
 
Andika message kwa Nabii Mkuu Geodavie akupe hela uko mkoa gani au mtafute Mchungaji Mashimo akuunganishe direct kwake ungejua mapema ungeongozana na wale Mashekh Jumapili iliyopita walipewa laki tano tano
Sometimes muwe mnaacha utoto kwenye mambo ya msingi sio kila anayekuja hapa anataka kujibiwa upumbavu

Kama hauwezi kutoa ushauri Bora ukapita kimya kimya halafu unakuta watu Kama wewe inaishi kwa mama yako Pumbavu.
 
Sababu za kuyumba kwa biashara yako labda zinaweza kutoa muongozo wa utatuzi wa tatizo lako
Kaka ni vile tu biashara haiendi.. nazungusha maziwa mtaani sku za nyuma mambo yalikuwa yanaenda kiasi lakini sasa... unazungusha lakin wapi... kaz mtaani hakuna... ukifanya wanadhulumu... nipo bukoba.
 
Sometimes muwe mnaacha utoto kwenye mambo ya msingi sio kila anayekuja hapa anataka kujibiwa upumbavu

Kama hauwezi kutoa ushauri Bora ukapita kimya kimya halafu unakuta watu Kama wewe inaishi kwa mama yako Pumbavu.
Brother mbona una matusi sana ..Kuishi Kwa Mama kuna kosa Gani? Mzee siku zote tunashauriwa ukiona ngoma imeshindikana rudisha mpira kwa kipa vinginevyo utapewa ushauri ambao anayekupa huo ushauri hajawahi kufanya hicho kitu zaidi ya kukisoma kwenye mitandao...

Kwani wanaoandika ujumbe wa business plan kwa Nabii Mkuu ni mapunguani? Mfano wewe unaweza kuta ni wale mtu anashida unamuita mnakutana Bar unamwambia ebu agiza unachokunywa kwanza halafu akishalewa unaanza kumsimanga na kumuitia mademu. Ifike mahala tuishi ukweli siyo kutoa ushau ambao hata wewe ukifanyacho hakitokani na huo ushauri wako unaoutoa
 
Ushauri wangu jaribu kupunguza matumizi kwenye hiyo biashara yako yaani Kama ulikuwa unakula elf5 kwa siku tumia elf3

Ela nyingine save jibane hivi kwa miezi 6 then hiyo pesa utakayoipata kwa mfano unaweza kuwa unaweka elfu 4 kwa siku mpesa au tigo pesa.

Wakati huo ikiwezekana zima simu za mizinga home na girls usitoe msaada kwa watu wenye uwezo miguu na mikono ya kutafuta pesa wakupumzishe kwanza kwa miezi 6

Baada ya miezi 6 fungua mgahawa mdogo tafuta watu wa kukusaidia kusimamia wewe uwe unapita pale kula then unaenda home

Usipike chochote then katika mgahawa wako anza kuweka angalau elf 10 kwa siku baada ya mwaka utanishikuru lazima utafungua biashara ya 3

Mimi nilishapitia huko ninapokwambia financial freedom inahitaji uwe risk taker asantee
 
Kwa jinsi ulivyo andika hakuna mtu anaweza kukupa ushauri wa maana. Kwa sababu hujaeleza uko wapi, unafanya biashara gani na changamoto zipi ambazo unakumbana nazo hadi kusababisha biashara kuwa ngumu.
Kaka biashara ni kuzungusha maziwa nipo bukoba...biashara ni vile tu haiendi nazungusha maziwa lakini wapi...
 
Kama ulikuwa umetoka katika imani yakumuabudu Muumba wa mbingu na dunia basi rudi ukiwa umenyenyekea na ujitakase na kila aina ya maovu na uzidishie kutoa sadaka kwa wahitaji hata kama nikidogo kwa kufanya hivyo utakuwa umejitengenezea njia na mambo yako yatafunguka kwa uwezo wa Mwenyez Mungu.
 
Ushauri wangu jaribu kupunguza matumizi kwenye hiyo biashara yako yaani Kama ulikuwa unakula elf5 kwa siku tumia elf3...
Nashukuru kaka kwa mawazo haya nitayafanyia kazi .. nashukuru sana..
 
Wewe una ujuzi gani na unaishi mkoa gani tuanzie hapo
 
Kwa jinsi ulivyo andika hakuna mtu anaweza kukupa ushauri wa maana. Kwa sababu hujaeleza uko wapi, unafanya biashara gani na changamoto zipi ambazo unakumbana nazo hadi kusababisha biashara kuwa ngumu.
Sema huna tu namna ya kumsaidia Mkuu usipindishe maelezo,km ni namna ya utafutaji ziko nying na zinapatikana kila mahali
 
Kaka bado sijaoa. nawaza kama ningekua nimeoa sijui ingekuwaje!
Pambana mwanzo mwisho kijana! Wanaume tumeumbiwa mateso. Hivyo hakuna kukata tamaa. Hela mtaani kwa sasa imekosa kabisa thamani kutokana na mfumuko wa kutisha wa bei kwenye bidhaa muhimu.

Hivyo hata usaidiwe leo, bado matatizo yatendelea tu kukuandama.
 
Sina ujuzi wowote japo nilifka form 6 ila sikumaliza kutokana na changamoto za kiafya.
Mmmh 🤔🤔

Ok yaani kuanzia umetokea hapa duniani huna unalolifahamu hata moja???...

Daaaah ok upo mkoa gani
 
Back
Top Bottom